MAAJABU NA STAREHE YA SERIKALI ILIYOVAA CHUPI
>> Wednesday, March 07, 2007
Kama unaamini biblia basi unaamini tokea Eva aonje tunda ,halafu na kumuonjesha tunda Adamu , basi hapo ndio mahitaji ya chupi yalipozaliwa.Kwa sababu inasemekana ndio michakaliko yote ya kibinadamu ikaanza.Maisha ya kula kwa kutoajasho na ....
Mambo yote yafunikayo mimi hupenda kuyaita chupi. Hivyo kunachupi za aina nyingi sana. Katika baadhi ya vitu tusivyoviona ni sheria, na ... Kusema ukweli mfumo mzima wa jinsi serikali yetu iendeshwavyo umevaa chupi.
Na kwa bahati mbaya vitu kama sheria ambazo zinatakiwa kutulinda zimevaa chupi, na naamini ni muhimu sana tuzijue.
Kabla sijaendelea kulonga hebu cheki hapa....
Swali:
Hivi unapomlalamikia Rais, unamlalamikia Kikwete au Ofisi nzima?
Hivi akiwa matembezini ughaibuni nani anashikilia ofisi?
Narudi kwenye chupi...
Wengi wetu tumezaliwa tumejikuta tumesitiriwa na kanepi. Halafu baadaye chupi ikafuata.Na kama kawaida ya mazoea kubadili kisitiri hatukujua katika hatua ya mwanzo.Lakini baadaye tukajifunza kubadili kisitiri na tukajua umuhimu wa jambo hili.
Sasa ....
..mimi nafikiri kuwa ni muhimu Watanzania wakafundishwa mfumo uwazungukao.
Naamini hii itasaidia sana kuweka mambo wazi . Itasaidia kujua wapi twende. Kikubwa itaondoa moshi utufunikao macho hawa watendaji wautumiao kututuliza kwa sababu hatujui nini kinaendelea.Kumekuwa na mambo mengi ambayo ukweli wake watendaji wamejaribu tu kutufurahisha kwa kuleta vitu ambavyo vinafurahisha macho kumbe vinatunyonya, kutuumiza nk.Unasikia eti barabara imejengwa halafu ukipita mwezi , haipo mvua imeichukua. Unasikia meli imenunuliwa halafu ghafla haifanyikazi haina spea.Rada, nk.. Haya yote ni moshi tu .
Samahani narudi kwenye chupi....
Jambo kubwa alijualo mvaa chupi ni kwamba hatuvioni vilivyo ndani.Lakini anajua kuwa tunajua kuwa vipo pale kunako. Vingine visafi, vingine vinanuka. Vipo baadhi vidogo, na vingine vikubwa kuliko.Ukiachana na aina ya vilivyositiriwa ni kwamba vyote vinaaina yake yakuathiri. Na kwa sasa hivi tusivyo vijua vinatuathiri na tuvijuavyo vinatuathiri vibaya.
Matokeo ya kufunika mambo , mara nyingi ni kuyafanya yawe yanaathari kubwa zaidi.
Nafikiri serikali ingekuwa haijavaa chupi:
- Hongo nyingi zinge kufa.
- Mikataba mingi ya holelaholela isingewezekana kufanyika.
- Tungejua kwa uhakika kazi ya Rais wetu ni nini
- Tungejisikia na sisi ni sehemu ya serikali
- nakadhalika.......kadhaa
Kutokana na ukweli wengi wetu hatujui nini kinaendelea, ni kidogo sana tunaweza kuchangia mabadiliko ya muelekeo.Tunabaki kulalamika wakati tunajua kuwa wahusika wanajua dua la kuku halimpati mwewe.
Chakusikitisha ni kwamba tusipo chukua hatua yeyote, starehe ya serikali iliyovaa chupi mojawapo ni jinsi inavyoweza kuficha fangasi bila kustukiwa. Basi ndio hivyo tena kila siku tutaendelea kusikia tu jinsi mambo yanavyokwenda kiholela. Na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuta kuwa na ujanja wowote zaidi ya kulalamika tu. Lakini ukweli ni kwamba kulalamika tu hakutoshi. Tunahitaji mikakati ya kuivua chupi serikali.
Unakumbuka Black Panther walivyokuwa wanajaribu kuchukua hatua pale kwa Kichaka?Jikumbushe basi kutoka kwa huyu aliyekimbilia Tanzania....
Swali:
Ushastukia Tanzania hatuhitaji mtutu wa bunduki kutatua matatizo yetu?
.....Naamini tukiivua chupi serikali tutaona mazuri yake na uozo wake. Hili litawezekana tu tuwezapo kujua serikali yetu inafanyaje kazi.Naamini hili tunaweza kulijua tukifundishana ya kweli sasa hivi.Kuna kipindi nilidhani najua mfumo wa serikali ya Tanzania. Lakini naamini nyadhifa na kazi kama zitajwavyo katika katiba na miongozo mingi tu, hazifanyiki hivyo Tanzania. Naamini hata Rais Kikwete siku nyingine hufanya kazi za waziri wa mambo ya nje. Au hata katibu wa wizara ya mambo ya nje.
Napenda kutoa changamoto kwa wanablogu wajuao mfumo kujaribu kutuelimisha. Tujaribu kujaribu kuweka wazi sehemu hasa ambazo zinatuponza hivi sasa.Tushirikiane kufunzana.
Duh!Samahani kidogo....
Ni vizuri kuanza na Raisi lakini nafikiri mfumo mzima unawalakini nyingi tu. Kama hatuwezi kufanya la zaidi basi angalau tujue sehemu gani , wahusika gani, na kujaribu kushauri ni nini kifanyike. Naamini itafikia siku wanablogu watakuwa wanasikika Tanzania.
Haya baadaye....
Lakini ngoja nikuache tena na Miriam Makeba atukumbushe mapambano.....
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Bila shaka njia mbadala itakayotufanya watz tuzijue haki zetu ni pamoja na kuijua katiba ya nchi. Sasa hili litawezekana pale ambapo somo la SIASA NA KATIBA litafundishwa mashuleni.
Kwa kufanya hivyo yawezekana kabisa kuivua hiyo chupi.
Binafsi nilikuwa sijui lolote kama aliyeua bila kukusudia anaruhusiwa kupatiwa dhamana. Lkn kumbe hili jambo lipo na linaruhusiwa kwenye vifungu vya sheria. Yapo mengi tusiyoyajua!
Kweli kabisa Mtanzania. Lakini nahisi hakuna atakaye tufunza haya mambo. Ni sisi wenyewe inabidi tuchukue majukumu.Lakini kazi ipo!
Post a Comment