Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukiitazama Dar kama Kioo cha Tanzania

>> Thursday, March 29, 2007

Inasemekana Michael Jackson alipofika Dar kikubwa alichokuwa anakilalamikia ni kuwa pananuka.

Mvua ikinyesha Dar ni rahisi tu kustukia jinsi gani mifereji ya kusafirisha maji ilivyo na mapungufu.





DAR-ES-SALAAM(Picha kwa hisani ya MICHUZI)







Leo nimekumbuka jinsi nilivyoshangaa kusikia kwa mara ya kwanza jinsi Kipindupindu kilivyokuwa kinasumbua London, Uingereza. Kutokana na ukweli kuwa mara nyingi nilipokuwa nasikia habari za ulaya na kuonyeshwa picha , hata siku moja nilikuwa siambiwi ni wapi miji hii ilikotokea.Nilikuwa naonyeshwa nakusimuliwa mazuri tu na jinsi inavyopendeza.

Swali:
Hivi kwanini wamagharibi wakiwa Afrika hupenda kupiga picha za sehemu mbovu na Waafrika wakiwa magharibi hupenda kupiga picha sehemu babu kubwa?

Basi baada ya kusikia maswala na kuanza kufuatilia miji hii nilishangaa sana.Hapo ndipo nilipoelewa msemo Roma haikujengwa kwa siku moja.

Mji wa London ukifuatilia hata jinsi ilivyokuwa vigumu kwa wanasiasa kukubali kugharamia gharama za kujenga mfumo wa kuondoa maji machafu unaweza ukamsamee diwani mtoto wa mjini Dar ambaye hata mifereji ipitayo kwake anaiziba.

Lakini tukumbuke huu mfumo wa London ulimalizika mwaka 1865.Mfumo wa Bazalgette kama ujulikanavyo kwa kufuata jina la injinia aliyesimamia shughuli, pamoja na kasheshe zote ulimalizika kwa muda wa miaka saba.Na mpaka leo hii kiini cha utokaji wa maji machafu mjini London.Inasemekana yeye ndiye aliyeshauri kuwa uchafu uelekezwe mtoni Thames hadi baharini badala ya kuupeleka ndani ya nchi.

Nacho jaribu kusema ni kuwa labda tusikate tamaa kwa hali halisi ilivyo sasa. Lakini kama Dar ndio kielelezo na ndio iko hivi basi kazi tunayo. Lakini kama London naamini mara nyingine mtu mmoja na mtazamo wake ambao akaweza kuutetea vizuri kuna wakati unaweza kuzaa matunda. Lakini kikubwa ni kwamba sisi ndio ni maskini labda ni vigumu kugharamia mifumo mbalimbali ihitajikayo nchini , lakini je tunaipa kipaumbele?Je masta plani inafuatwa?
Angalia hii picha chini....






Picha kwa hisani ya Mjengwa













Hali kama hizi kweli katika mji ambao ni kielelezo au hata mji wowote ule zinakubalika kweli?.Utaona tu hapo kirahisi jinsi gani watu wanaweza kuugua kipindupindu,malaria na bila hata ya kuwepo hapo unajua kuwa pananuka.

Nimependa kuuzungumzia mji wa London kuwa nao ulikuwa unanuka watu wakafanyia kazi. Hapo juu kwenye picha kuna mfereji hivyo inamaanisha kuna watu walifikiria kufanyia kazi hiki kitu. Tofauti ni je mfumo mzima unafanyiwa kazi? Nani anafuatilia?

Kila siku hizi tunaona jinsi majengo mapya yanavyojengwa. Lakini nasikia kunabaadhi ya sehemu imekuwa kawaida kunyea kwenye mfuko wa plastiki halafu kuutupa kinamna. Sasa tunavyojenga haya majengo mapya au tutoavyo vibali au tununuapo radar uchwara ..........
Sawa nisilalamike sana !Lakini nadhani ni muhimu kukumbushana kuangalia hii picha katika kona zote. Kwa maana sehemu yenye jengo zuri lakini linukalo laweza lisiwe na maana vilevile.


Tunaonyeshwa picha ya mambo mengi ambayo yanabadilika Dar. Natumaini mambo yatabadilika nchi nzima.Safari bado ni ndefu. Lakini kwa sasa bado Dar inanuka.
AU?

Rafiki yangu mmoja aliyoko Lagos ananiambia kuna sehemu hazikaliki kwa harufu. Hivyo hili tatizo liko Afrika nzima. Lagos inasemekana ndio mji wa wajanja kuliko yote Afrika.Sasa sijui!
Kazi ipo!Lakini tusikate tamaa.
Ngoja nikuache na BANTU akikupa Lagos Jump

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP