Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Namzimia Mbu, Simba kapendelewa tu....

>> Saturday, March 31, 2007

Mbu yuko mawazoni leo!

Unajua kuna watu kibao humsifia Simba.
Huwa pia nashangaa sana jinsi nchi za magharibi pia zitumiavyo sana Simba wa Afrika kama alama yao ya mambo mengi tu mpaka hata katika baadhi ya bendera zao. Lakini ukifikiria, mara nyingi hutumia alama ya Simba dume.
Lakini Simba dume ukimfuata porini mara nyingi yeye siye afanyaye maswala yampayo simba jina.
Au?
Ni simba jike ambaye huwinda zaidi.
Ni simba jike ambaye ni mkali zaidi.
Ndio Simba dume ananguvu. Lakini huwa anakuwa mkuu wa familia ya simba kwa muda usiozidi miaka miwili halafu anapigwa chini na simba dume mwingine. Hivyo nguvu za simba dume ambaye husifiwa sana iko kwa miaka miwili tu.Katika uwindaji pia , ukifuatilia utakuta kuwa Mbwa mwitu(wild dogs) huwa wanafanikisha kudaka wamtakaye mara nyingi kuliko afanikiwavyo simba.

Sasa turudi kwenye mbu. Huyu kijana ingawa maisha yake ni mafupi lakini mambo yake katika muda huo si utani. Kitu nimzimiacho ni jinsi tokea miaka milioni mia moja sabini asadikikavyo amekuwepo duniani mpaka kesho anabadilika kutokana na mazingira. Kila dawa utumiayo kumuua hakawi kuigeuza kuwa mzaha. Amefanikiwa kutuletea magonjwa nakutuua kwa miaka maelfu hata katika kipindi ambacho hatukuwa tumemstukia. Ukimlinganisha umbo lake na awawindao , hapo utakoma. Maana anamvaa kijeba mkubwa kwake mara milioni .

Duh!
Sawa basi nimekubali!Mbu hafikirii hilo swala la ukubwa wa amfyonzaye.

Lakini binadamu inabidi tumuige huyu kijana.

Kinachosikitisha ni kwamba watu wengi hatumjui mbu. Hatumfuatilii hata ni kwasababu gani ni mbu jike tu afyonzaye damu.

Basi ngojea tukumbushane.Mbu jike hufyonza damu kutafuta protini ambayo huitumia katika uzazi- ukuzaji wa mayai yake. Hivyo mbu akikuuma lazima ujue huyo mbu alishafanya ngono hivyo anatafuta tu protini kwa ajili ya mayayi. Na hii ndio maana ni mbu jike afyonzaye damu.

Lakini unakumbuka mzunguko mzima wa maisha ya mbu?Tukikumbuka haya tunaweza sana kuwapunguza kwa kuondoa maji yaliyo simama.Kumbuka yale makopo yaliyojaa maji pale kwenye shimo la takataka.Lile kopo pale nje utakalo kulitumia kupanda maua. Lakini usilisahau lile kopo uliloliacha pale nje baada ya kuamua kuwa hutalitumia msalani. Duh! Na haya madibwi ya maji nayo bomba la hospitali ya uzazi?

Mbu kiboko!
Eti anatemea mate kabla hajafyonza. Halafu kwa kusafirisha vidudu vya Malaria anatuua kuliko wadudu kibao.
Eti halafu twamuogopa Simba!
DUh!
Usitishike!Tunakumbushana tu!
Ngoja nikukumbushe Lambada basi.Unawakumbuka Kaoma?
Pata Lambada basi!Wikiendi njema!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 3:30 pm  

Simon,
Mimi kama msomi, nimegundua kuna maana mbili katika nakala hii. Kuna fumbo au unaongelea Simba na mbu? Sijui kama msomi mwingine atagundua nazungumzia nini.

Simon Kitururu 6:41 pm  

Miriam Duh!Simchezo mzuri kustukia:-)Nimekuzimia miriam......Duh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP