Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Staili ya kumfuata Mwanadada Kisimani!

>> Friday, March 02, 2007

Binadamu anaasili ya uvivu.
Karibu kila kitu anachojivunia ugunduzi wake, ni kitu kirahisishacho mambo ilikumwezesha kuishi aishivyo bila kutoka jasho sana.

Lakini pia binandamu huyo huyo si mvivu akiwa na kitu akiwaniacho, akilini mwake anaushuhuda kuwa atajitamba akikipata.

Hivyo mambo mengi binadamu akwepayo kufanya ni kwasababu tu akilini mwake hajajihakikishia kuwa apatacho kitalingana au kuzidi utoaji jasho wake.

Kutokana na hili...........

  • Wanafunzi wengine watakimbia hisabati, lakini hao hao hawatakosa mazoezini.
  • Wengine watakimbia mazoezi ya viungo lakini hawatakosa somo la ulimbwende.
  • Viongozi wengi, watakimbia kazi walizonazo ofisini, lakini hawatakwepa kutumia gari la ofisi na hata vitu vingine vya ofisi , ikiwemo kumuonja sekretari , mesenja au hata dereva.
  • Wengine watakwepa ngazi kwani wamestukia kuna lifti
  • Na kadhalika....kadhaaa
Sasa kigumu kinachojitokeza ni jinsi ya kumfanya binadamu huyu astukie mwisho wa kutoa jasho kuna utamu kunoga.

Kingine kichanganyacho ni jinsi kila mtu atafsirivyo utamu kunoga.

Hivyo kwetu sisi wenye uume, staili ya kumfuata mwanadada kisimani mara nyingi si tatizo mara tujuapo mwanadada , ambaye vichwa vyetu vyote viwili vimetuhakikishia analipa yuko kisimani. Mwenye kutambaa, atatambaa,wakukimbia ,atakimbia. Kama mashabiki wa mwanadada ni wengi, basi wengine tutamkatizia denge.

Duh!
Nimestukia sijui sana staili za akinadada za kumfuatilia mwanakaka kijiweni!

Sasa ukichukua jinsi binadamu asivyotabirika naamini wengi tumeacha kuangalia ni nini kinampamotisha.Katika semina , kuna watu wakagundua kuwa, ukitaka kumfanya mtu aende kusoma iliaelimike, basi mwambie kuna posho, na ubwabwa. Halafu mwisho wa semina kutakuwa na bomba la sherehe ambalo litakuwa na kilaji bwelele.

Duh! Lakini hivi hizi semina ni za kumfaidisha aendaye kwenye semina au aandaaye?

Duh !

usistuke!Sijui jibu.

Sijui anayeandaa kwanini anafanya hivyo, ikiwa itabidi awalipe awapao elimu.

Chakusikitisha ni kwamba , najua hizi posho hazisaidii kumpamotisha mtu atakekuelimika. Naamini zinamfanya aende kwenye semina, lakini sinauhakika kuwa zinaondoa hamu yake ya kusubiri hivi chakula saa ngapi.

Tukirudi katika kumfanya Mtanzania , Muafrika, mwanadamu apatemotisha , inabidi ajifunze kuangalia jinsi gani alipofikia hapatoshi.Ajifunze kujua alopofikia hapana tafsiri moja.

Kuna watu nimesikia kuwa wameridhika. Kitu kama hiki nikisikia huwa nashangaa sana!Kwa sababu sidhani kuwa mwanadamu katika maisha haya mafupi anaweza kuridhika. Leo ya mwanadamu ni tofauti sana na kesho ya mwanadamu, na hapo ni bila ya kuidharau jana.

Swali:
Hivi unahisi kwanini Bill Gates anaamka asubuhi kwenda kazini?







Hivi unahisi ni motisha gani inamfanya Bill Gates amfuate mwanadada kisimani?










Nachosema ni kwamba, yale mambo ya kusema naona jamaa karidhika, siumeona kaota kitambi? Sikubaliani nayo. Jamaa kaota kitambi kutokana na staili yake ya maisha na mlo uendao na hicho.Au pia anawezekana akawa mgonjwa.

Kazi nzuri haiwezi ikakuridhisha kwa yote.Itakuridhisha katika takwa lako lakua na kazi nzuri. Kuna kitu tu ambacho katika maisha ya binadamu muda wowote anatakiwa akifanye. Na akiamini kuwa ndio siri ya utamu kunoga atakifanya kwa bidii.

Kuhusu Watanzania , naweza kusema kwa uhakika , kuwa sisi wote, kunakanamna ubongo wetu haujakuwa na uhakika kuwa uhangaikaji wetu ambao inabidi tuuzidishe utaleta matunda ambayo yanazidi jasho tutoalo na ambalo inabidi tulitoe.

Unaweza ukanibishia! Na utakuwa na sababu nyingi ambazo zinatoa ushahidi kuhusu.....

  • Kwanini sisi ni maskini
  • Tunamagonjwa mpaka ya kipindupindu, beriberi ,nk mpaka leo hii.
  • Umeme , hata jinsi ya kupata jenereta kwa nchi ni vigumu.
  • Ujanja ni kulia ofisini.

Meseji kwa mshikaji:
Duh!
Mshikaji usipojenga mwaka huu basi tena.Si unajua mshikaji ,naona uko jikoni!


Tukirudi katika hoja
:........Usistuke nakukubalia kuwa uko sahihi, kuhusu sababu uzihisizo zinatuweka hapa tulipo.

Lakini ukiniuliza mimi nitakuambia kuwa , bado elimu yetu, tamaduni zetu, aina ya malengo yetu ,hayatupimotisha kujitupa katika kuhangaikia ile hatua ya pili, ya tatu, nne....nk.Haitupi tafsiri nyingine ya maisha , maendeleo ,jitihada, na cha zaidi haitupi mwanga wa hatima ya yote.

Asilimia yetu kubwa kutokana nakukabiliana na umaskini , mafanikio kwetu ni pesa tu. Lakini ubinadamu ni zaidi ya pesa.

  • Muulize Warren Buffett kwanini anagawa pesa zake.
  • Muulize Bill Gates kwanini anasema anamzimia Warren Buffet.
Sasa tufanyeje?
Jibu ni moja tu. Inabidi tuende kinyume na asili yetu ya kibinadamu ya kuoanisha mafanikio na kupunguza kutoka jasho. Hili linawezekana tu pale tutakapokubali kujifunza aina mpya ya kupima utamu kunoga. Litafanikiwa pale tutakapo badili uzani ili uweze kutuhakikishia kuwa pamoja na kwamba tunatoa jasho sana sasa hivi , hii si lazima itafsiriwe kama shida. Inawezapia ikatafsiriwa kuwa ni njia mojawapo ambayo inatupa uwezo wakujijua kama binadamu na pia italipa hapo mbeleni?

Swali:
Lakini kutoka jasho kunalipa kweli?

Jibu :
Si lazima.

Lazima uwe na magoli na ujue unakokwenda, la sivyo utatoka sana jasho na mwisho wa siku utamu kunoga hupati.

Unajua usipojua kisima kiko wapi, staili zako zote za kumfuata mwanadada kisimani hazita kusaidia.

Haya basi ...
Akinadada mnajua mwanakaka yuko kijiwe gani?

Samahani akinadada kwa kumtumia mwanakaka katika ndoano. Najua wengine wenu kama mngekuwa samaki mwanakaka angekua bado hawezi kuwavuta kudakwa kwenye ndoano.

Tukiachana na hilo.......

Basi tuendeleze kuufundisha ubongo kustukia lawalawa nyama tusizoziona. Tuufundishe kukubali ladha nyingine za maisha katika haya maisha ambayo ni ya mpito tu na mafupi. Tukifanya hivyo tutapata tu peremende mwishoni, katikati na mwanzoni.

Ijumaa njema!
Lakini nawaacha Still Cool........


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 12:40 am  

Kitururu!
Bila shaka ww ni mzee wa Psychology. Lakini hayo ndio mambo ya silka na hulka ya mwana-adam Big up.

Ulinipa changamoto kwenye lile bandiko langu la "wataiva.....". kwamba kuna kitu sikukigusia. Please ukinigusia juu ya kitu hicho nitafurahi sana.

Simon Kitururu 12:30 am  

@Mtanzania:Sikutanii kuhusu kuwa Mimi nimfanyabiashara. Hatasitaki kujiita mchumi. Lakini uchumi ndio mzizi, halafu nikahamia biashara. Lakini sijui kwanini siongelei mambo niliyosomea kwenye blogu yangu.Lakini nahisi ni kwasababu nikizungumzia mambo mengine najisikia kama niko kazini.Lakini zamani kwawanaonikumbuka nilikua nasumbua kwenye sayansi pia.Au kuna mtu ana bisha?:-)

MTANZANIA. 4:52 am  

Simon!
Nimecheka kweli.
Basi una kipaji ktk elimu ya saikolojia.

Prof.mmoja wa Jiografia-UDSM, alipata kutuambia kuwa alisoma hesabu mpaka J.K.T-Makutupora na pia alikuwa mkali kwa masomo mengine ya sayansi. Ila anasikitika kuingia kwenye masomo ya ARTS na hatimaye kuwa Prof.

Kwa kesi yako si mbaya kujiingiza kwenye elimu hii though ww ni mfanyabiashara. Kazi njema.

Maisha 1:49 pm  

simon si unazishe kipindi kabisa redioni?TV hainogi redio ndio bomba maana naona skillz sio za kawaida katika uchambuzi huu.

i would changia lakini muda sina wa kutosha.

Simon Kitururu 11:43 pm  

@Maisha:Kipindi redioni,duh!
@Mtanzania: asante kwa kunipa moyo.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP