Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

kwa mara nyingine; ''BWANA ASIFIWE!!''

>> Wednesday, September 30, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda kiasi hasa kama wewe ni Mkristo!:-(]


Kibinadamu sina uhakika na nafasi katika changamoto UMUHIMU ichukuayo SIFA,...
.....ingawa nastukia MIMTU inavyojisikia vizuri na kuridhika kwa kuwa IMESIFIWA.

Na Libinadamu kwa kupenda SIFA,...
.... labda kweli hata kwa kulidanganya linahitaji KUSIFIWA.:-(


Lakini nasita kuunganisha ya MUNGU na SIFA,....
....kwa kuwa kama ndiye aliyeumba vyote mpaka hiyo sifa na ndiye ampaye mtu nguvu ya kusifia,SONA UHAKIKA kama naye anahitaji kweli kutoka kwa Binadamu wanyao na kubanja KUSIFIWA.:-(

Sipingi wafuatao maandishi ya vya kwao vitabu vitakatifu ambavyo kwa tafsiri zao Mwenyezi inabidi umpe SIFA,....
.... lakini basi kunauwezekano umuhimu wa sifa ni mkubwa sana hata kwa Binadamu kwa Limtu ikiwa kama tukiachana na ya mtu kwa limtu, kwa Wakristo mpaka BWANA anahitaji KUSIFIWA!:-(


NI WAZO tu MHESHIMIWA Muungwana na HAKI YA NANI TENA SIJARIBU kuingilia IMANI YAKO KABAMBE!

SWALI:

 • Unafikiri WAKRISTO wengi wasalimianao mara kibao ''BWANA ASIFIWE!''huwa hawamaanishi tu kwa tafsiri fulani'' Kijeba Mambo!'' ?

 • Unauhakika lakini kweli BWANA anahitaji kusifiwa?


NIMEACHA na samahani kama NIMEKUKWAZA kinjonjoli MHESHIMIWA na ukipenda niombee IMANI IKUE!


Hebu basi twende Kenya ili Enomizizi and The Rarewatts watusaidie kubadili hali ya hewa KIJIWENI kwa kumzungumzia tena kwa miondoko ya CHAKACHA-BABA MANYORA


Au tu tubaki hapa hapa Kenya katika miondoko hiyo hiyo ya CHAKACHA Safari Sound Band warudie tena kitu chao-Mama lea mtoto wangu

Read more...

KWA kuongea unachofikiria unaweza kuumiza ROHO mtu!

Na kuacha kuongea unachofikiria,....
.... anaweza akaumia mtu!:-(


Kwa bahati mbaya hata ujaribu kwa kunuia kukwepa kuongea unachofikiria,...
.... mengi bado unayaongea kila siku NA NI ukweli ni kwamba bado HATA SASA HIVI uliyoongea LABDA NAYO KWA MARA NYINGINE hujayafikiria na labda umuumizaye hajakwambia lakini KASHAUMIA angalau roho mtu!:-(

Swali:
 • AU?
 • Ushawahi kukaa kimya ili usimuumize mtu roho na kustukia BAADAYE kwa kuwa ulikaa kimya kaumia mtu?

NI wazo tu KIJEBA usitishike!:-(

Hebu UB 40 wabadili tena kwa kitu -BURDEN of SHAMEAu tu THEM MUSHROOMS watekenye kwa zilipendwa

Read more...

Asilimia ya HAMU yako kwa mtu wakati umtamaniye KIUTU ni MWANAMKE!

>> Tuesday, September 29, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]


Usipokuwa makini unaweza kufikiri tofauti zinajulikana,...
.... kati ya mwanamme na MWANAMKE!:-(

Na ni mpaka uanze kufuatilia nini hasa kinajulikana,...
....kisababishacho hata mpaka DUNIA ya leo bado INATOFAUTISHA HAKI za mwanamme na zile za MWANAMKE.

Na haki ya nani tena ukitafiti yanayojulikana,...
..... utastukia wengi hawajui nini hasa humtofautisha manamume na mwanamke ukiachilia mbali vionekanavyo kama AFANDE WA CHINI kwa mwanamume na TITI kibonge, chuchu pana na ile kitu UKE kwa MWANAMKE!:-(


Na unaweza hata kukana hata kama inajulikana ,.....
.... ingawa ukweli UKO PALEPALE UMENG'ANG'ANIA kuwa katika jamii kuna MIDUME inajisikia MIANAMKE na WADADA WASAGAJI ambao kati yao kuna ajisikiaye MWANAUME ingawa hana uume a.k.a KITOMASIO kwa kuwa yeye ni mwanamke ingawa avutiwao nao kuwavulia chupi nao ni WANAWAKE!

Na tukiendelea na yadhaniwayo yanajulikana,...
..... nikuulize katika WA BINADAMU USAWA unafikiri ni ASILIMIA NGAPI ya MTU ambayo iko sawa ndani ya MWANAMKE NA MWANAUME kabla hujajazia vikorombwezo vingine kama UUME na UKE viletavyo tofauti ikufanyayo ustukie kuwa unayekerana naye MTU , ni MWANAUME au MWANAMKE?


Ndio kumbuka inasemekana ni kitu kinachojulikana,....
.... kuwa kama umuwazaye ni NDUGU YAKO mara zote kama wewe sio WALE wamtamanio angalau binamu nyama ya hamu, HAMU yako KWA NDUGU huwa haiathiriwi au kupewa changamoto kwa KUJUA uwamisio a.k.a ANGALAU KUWA NA HAMU YA KUWAONA TENA, walicho nacho maeneo ni UUME au UKE.

Kumbuka tu kuwa ingawa labda siku hizi inajulikana,...
..... si kila umuonaye sura nyororo TITI mwanana , chuchu pana, na tako mtikiso SINGIDA-DODOMA ni MWANAMKE.:-(


Na usishangae baada ya muda ikijulikana,....
.... kuwa baadhi ya binadamu watanunua KISAYANSI kuzaa MBWA badala ya BINADAMU baada ya kufanikisha tendo la UASHERATI kwa kuwa WANAPENDA SANA MBWA kuliko WATU au kwa kuwa ni FASHENI TU hasa ukikumbuka sasa hivi TUMESHAFIKIA ukitaka kama WEWE DUME NA UMECHOKA UUME na UNAPESA waweza kununua wakukate kidude na kukutengenezea UKE kwa kuwa TU siku hizi ukimuona KHAMISI dume zima HUTAKI TU AWE RAFIKI YAKO TU WAKAWAIDA kwakuwa eti KIDUME unajisikia NAWE kumpa kidume mwenzio UKE !:-(

Swali:
 • Unauhakika hauna rafikiyako ambaye hujui tu lakini labda ana U-CASTER SEMENYA?[samahanni lakini kama unisomaye nakukwaza kwakuwa una U-CASTER SEMENYA!:-(]

 • Unafikiri ni asilimia ngapi ya HAMU YAKO kwa UMPENDAYE MTU inapewa changamoto na yake JINSIA?

 • Au unafikiri mapenzi yako karibu kwa wote uwapendao HAYAATHIRIWI na jinsia yako tu kwakuwa una UUME au tukiachilia chuchu muruwa basi una UKE?

 • Kwani unafikiri kimfanyacho mtu awe ni mwanamke ni NYONYO yakutosha na SUPA K kwa chini kidogo na kwa mwanamume ni Madevu kama UFAGIO WA CHELEWA na yule AFANDE wa chini kwa chini kidogo tu?


NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA na kumbuka ni wazo tu hili MUUNGWANA Banangenge!

Hebu basi turudi tena Tanzania SHAKILA adai-Moyo unalia macho yanacheka.Au tu MAXWELL adai-Ever Wanting to Want You toAU tu MAXIWELL arudie tena kitu-LIFETIME[live]

Read more...

Kuhusu POOZEO!

Poozeo,....
......hupooza njaa KWA KUIWA ingawa WAKATI LINALIWA huwa halichukuliwi kama ni kikuu CHAKULA.

Na hata ubishe kuna wahalalishao matumizi ya poozeo,....
....ingawa mahitaji hayo yanaweza yakaletwa na uvivu wa kuhangaikia chakula kikuu kiive au tamaa NA SIO LAZIMA ni kweli hukimbilii kula msosi mkuu kwa kuwa kimeshachacha kwa kuwa ni cha zamani kikuu CHAKULA.

Na waliohamasishika na poozeo,...
.... hudai wakijisikia vibaya huhamasishika na nyumbani kula kwa juhudi kikuu CHAKULA!.Ingawa kuna ambao baada ya kupooza na poozeo,...
...inazidi kusikitisha kwa kuwa husahau kula KABISAAA NYUMBANI ingawa nyumbani kimeiva na tayari kimeandaliwa CHAKULA!:-(

Kumbuka kisaikolojia waweza kuathirika na poozeo,...
....NA hata kama kwa vitendo umekwepa kufikia KUPOZA bado laweza kufanya matatizo yako binafsi ya Limke, Limme, Limchumba au watoto na ndugu ,mtu ufikiriaye anakuelewa NA UMSIMULIAYE YAKUSIBUYO ni poozeo ingawa hahusiki hata katika swala la kwanini hunogewi na kikuu CHAKULA.:-(

Lakini wapo ambao wanahitaji kikuu chakula na pia poozeo,...
...kwa kuwa wanadai utamu wa poozeo unaletwa na kujua ukitaka tena hata tu kwa kujisikia vibaya unaweza ukajikuta UNACHAKUFANANISHIA UTAMU au TU unanguvu sana baada ya KUPOZA na poozeo, kula cha nyumbani kikuu CHAKULA.:-(

Swali:
 • Unafikiri kimada kama aina moja ya POOZEO huwa anavutia vilevile KIMNOGO akishakuvunjia ndoa?
 • Hivi umestukia kuwa takwimu zinadai ni asilimia kubwa ya walioko kwenye ndoa ndio wapatao kwa wingi magonjwa ya zinaa kwa msaada wa poozeo?

NI wazo TU MUUNGWANA na LABDA sikuongelei wewe!:-(

Hebu Vybz Kartel abadili kwa kitu- ImagineAu jikumbushe muda sio mrefu uliopita kabla ya Obama baadhi ya Wamarekani WEUSI walipofikia ki self-esteem kwa kumsikiliza Blowfly akiku-Funk YOU[Tahadhari:Sio video yako kama ni mtoto na msikilizaji wa LYRICS na kama muungwana unaweza kukwazika au kama unatabia nzuri jua tu aimbacho asilimia kubwa ni matusi na sikushauri usikilize!:-(]

Read more...

Tangazo/UJUMBE kwa WATANZANIA ambao ghafla wamejikuta wanaondoa ujinga, wanaishi au wamelowea FINLAND!

>> Monday, September 28, 2009

Hello kaka,

Mambo vipi,
sasa ile network ya watanzania waishio Finland iko hewani rasmi.
Anuani ni:

http://www.bongosurprise.com/wabongosuomi

Please sign up, pia fahamisha na wadau wengine ili libeneke lianze.

Read more...

Mheshimiwa Mzee , TOKA CHOONI BASI na wengine waingie!:-(

[Tahadhari: Neno tamu CHOO halina maana ya CHOO katika taralila hii!:-(]


Kwako MWANASIASA MKONGWE wa Tanzania!


Wadai we' mzoefu
Twajua we' maarufu
Wasahau udhaifu
Ni choo kung'ang'ania


Ukiingia utoke
Kung'ang'ana usitake
Damu mpya ndio pake
Unapopang'ang'ania

Usilale TU chooni
Kunya wengine makini
Twasali madhabahuni
Toka tu basi chooni!


Ukipitwa na wakati
Umepitwa na wakati
Achia TU madhubuti
Nao pia wathubutu!


Swali:
 • Hivi kwanini unafikiri kuna wanasiasa VIKONGWE ambao hawataki kuachia wengine nao wajaribu hasa ukizingatia hata kama kunakipindi mchango wao ulikuwa unaonekana basi kipindi hicho kishapitwa na wakati?

 • Unauhakika mbunge wako sio walewale waingiao chooni halafu hawataki kutoka?[Samahani! katika sentensi ''Waingiao chooni'' nilitakakuandika na kumaanisha ''Waingiao Ofisini''!:-(DUH NASITISHA WAZO HAPA halafu ngojea niende CHOONI tu kidogo Mheshimiwa !
WAKATI NIMEACHA kumbuka hili ni WAZO TU Muungwana!

Ngojea FOXY BROWN akiweka spin yake kwenye wimbo wa Jimmy Hendrix abadili hali ya hewa KIJIWENI HAPA kwa kitu -ART OF WAR[Tahadhari: Lugha chafu!:-(]Au tu Foxy Brown andelee tu kufafanua kipengele-Hot Spot[Tahadhari:Lugha inaweza kumkwaza mlokole!:-(]

Read more...

DINI nzuri kweli UKICHACHA!:-(

>> Sunday, September 27, 2009

Swali:

 • Kwani ulifikiri matumizi ya dini ni kupeleka tu watu mbinguni?Dini tamu kwa kuwa mambo ya kidini,...
..... ni ya KIROHO na hayanunuliki hata katika soko mjinga.

Na kama unauziwa dini,...
.... jiulize na tafakari kama katika jedwali KUUZIWA mambo ya DINI na ukanunua hakuna ujinga.

Na matatizo ukubwa yakizidi kiboko ni dini,...
... kwa kuwa haikawii kukushawishi yote ni mipango ya Mungu ingawa alikupa akili na wajua kunayafanyikayo duniani kijinga.

Ukichacha na kama unafuata dini,...
.... inasemekana kwa imani yako waweza kujifariji angalau umeshiba na WEYE NI tajiri kiroho.

Swali:
 • Hujastukia kuwa matatizo yakizidi imani inakua?
 • Kwani hujui kwenda kanisani au msikitini ni bei poa kuliko kwenda baa au disko au kununua malaya?

 • Kwani pamoja na yote mazuri yaletwayo na dini hujawahi kustukia dini inasaidia kweli kuhalalisha kurahisisha bajeti hasa ukichacha?

NI wazo tu MHESHIMIWA!

Ngojea Will Smith abadili hali ya hewa kwa kibao -SwitchAu tu Vybz Kartel ft Spice wazungumzie-Ramping Shop


Asanteni TENA wadau wote mkiwemo MadICe, Nester, Ray na wangine wote ambao baadhi mpo kwenye picha hizi nilizozidaka juzi ya Jana.....


Photobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucket
Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

PhotobucketPhotobucketPhotobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucket


Photobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket
PhotobucketPhotobucket


PhotobucketPhotobucket

Read more...

KUTOKA JUU kama unataka kuifikia FIRIGISI NONIHINO, labda wahitaji kuingiza ANGALAU kidole /KIFAA chini kidogo zaidi kama unadili na kitu KIPENZI!

Mara nyingi MAJAMBOZ hayadumu kwa kuwa umuhimu wake wathaminiwa kwa juujuu,...
.... na kwa kukwepa ugumu NA KUZOEA URAHISI hatutaki kuyaelewa hata kwa chini kidogo.

Na kwa juujuu ,...
.......ikiwa inanoga unaweza kutostukia ukitaka kujua mpaka asili ya utamu labda ni muhimu uchimbe angalau kwa chini kidogo.

Na kama umeshajua mpaka shina la utamu KWA URAHISI utastukia ukipewa kwa juujuu,....
.... na hakuna kitu kitamu kama kujua unachodili nacho NI NINI au tu kama ni kweli unagawiwa au KUGAWA kwa juujuu , KATIKATI au HATA kwa kukionja umestukia mpaka mizizi yake kwa kuwa ni katika NANIHIII hii inapatikana chini yake kidogo.


Swali:
 • Unauhakika naongelea nini?
 • Unauhakika utamu ni nini?

USITISHIKE Mkuu ni WAZO TU HILI !

Hebu Venessa Paradis adai-Joe le Taxi
Au tu Sade arudie Sweetest Taboo

Read more...

Ndani ya UTAMADUNI wa kama NYUMBANI hapakaliki basi ngojea TUKAWACHEKEE MAJIRANI!

Kuna watu wakuchekeao huku wameshikana mikono nje ya majumba yao,....
.....wakati wametoka kupigana roba, au tu KUPARUANA MAKUCHA huko kwao.

Kuchekelea majirani imekuwa tabia yao,...
....wakati nyumbani wakiongea Kiswahili wanasikilizana kwa lugha wasiyoielewa isiyo Kiyao.

Tatizo ni , kama hao ni mke na mume na wewe sio ndugu yao,...
....ukistukia kiendeleacho na kujiingiza kwenye yao, unaweza kujikuta WEYE sio tena rafiki yao.:-(

Kama tu ndugu kwa ndugu WAKIGOMBANA na ukiingilia yao,...
.... waweza kujikuta unachekesha ndugu wakipatana hata kwa sababu za kijinga LAKINI zilizo suluhisha yao.

Swali:
 • Unauhakika kuna ajuaye kwa uhakika wakati mwanana wa kuingilia ya wengine?
 • Unauhakika hutumii kuchekea watu ili tu kuzuia wasistukie una bomba la kibano?
 • Umemchekea jirani leo kisawasawa au umemkenulia tu meno?
 • Hujawahi kustukia angalau uwezo wa binadamu kujichekesha katika kubaraguza kuwa mambo shwari mgeni akija GHAFLA wakati watu wako katikati ya ugomvi?

Nasitisha wazo!


Turudi tena Reunion kupata haka kawimbo kutoka kwa Granmoun Lele kaitwako - Soleye


Au tu Kassav warudishe kitu -Zouk La Ce Sel Medicament Nou Ni (Live)

Read more...

Jamani JAMANI jamani LEO MIE MWENZIO najisikia vibaya JAMANI![sentensi hii imebaniwa pua na Shuga Dada!:-(]

>> Friday, September 25, 2009

[Tahadhari:Wazo limepindia kushoto zaidi kidogo ya kulia!:-(]

Kujisikia vibaya bomba la nishai,...
...halafu kwa ushenzi wake hata ulipate kubwa zima utastukia HICHO KITU halijui vizuri kusimulia.:-(

Na kwa kujisikia vibaya waweza kujisikia mpaka kutapika ilivyokuwa nishai,...
... halafu KITU cha ajabu labda hata jinsi TU mtu ajisikiavyo kichefuchefu hakuna awezaye vizuri kukisimulia.:-(

Swali:

 • Unabisha?
 • Unadhani kuna watu wawili wajisikiao kichefuchefu sawasawa?
 • Ushawahi kumsikia mtu awezaye kuelezea ajisikiavyo vibaya akaeleweka bila kufafanua?
 • Kwani WEYE unajua jinsi ya kusimulia unavyojisikia vizuri au ndio weye ukisikia tamu watwambia unajisikia vizuri ?
 • Hivi kama wewe ni mpenda chai ya sukari unajua KWELI kusimulia utamu wa chai isiyokuwa na sukari?LIONE VILE!

NI WAZO TU MHISHIMIWA usiye BWANYENYE na NIMEACHA wazo Mkuu!

Nakutakia SHIBE ya KILA la KHERI na CHOO CHAKE Ijumaa na WIKIENDI HII!


Mie naanza lakini hebu turudi Afrika kidogo pale CAPE VERDE tena tukutane na Bi MKUBWA CESARIA EVORA alete tena kitu-ANGOLAAU turudi kwa Mhaiti WyClef Jean ft Mary J Blige watukumbushe zilipendwa katika kidude-911

Read more...

Mie MKULIMA lakini sijui nijiite WHITE FARMER kama wakulima wa ZIMBABWE ndio nionekane mjanja BONGO a.k.a BAB K?

[Tahadhari: Hili ni wazo holela!.-(]

Ukulima ni kitu bomba,....
.....ingawa BONGO kuna wachanganyao UKULIMA na USHAMBA!:-(

Swali:
 • Hivi unauhakika ushamba ni kitu KIBAYA?

Haki ya nani tena, Masela na Masista DU dukinaa, hata ukiwa fundi bomba,...
.... ukichemka au kuingia kichwa-kichwa kabla hawajakutoa nishai WE WAKUJA wanaweza kukukejeli katika staili ya tusi '''WEWE MKULIMA NINI!'' utafikiri wanajua ulivyokuwa mtundu hata gizani ukiwa SHAMBA:-(

Na usishangae kama wewe ni mbongo ukiwakuta WABONGO wadhaniao KIMTOKO wako bomba,...
....wakimshangaa Robert Mugabe na wenzake huko ZIMBABWE wanavyong'ang'ania mashamba wawe WAKULIMA baada ya kumstukia MKULIMA a.k.a WHITE FARMER kuwa ni mjanja kwa kuwa na SHAMBA.

Sasa Sista Du makalio mtikiso SINGIDA-DODOMA uninyimaye nafasi ya kukuomba,...
......kwa kuwa umestukia mie MKULIMA, sijui nikijiita WHITE FARMER Bongo utaniniruhusu angalau nikung'ate sikio katika kujaribu KUMWAGA KAULI NIKUELEZE ningependa katika mambo mpwito basi MWENZIO NIMEJIFIA na ningependa IKIBIDI kimbinde twende SAMBAMBA kwa staili matata za PENDO KIBONGE nilizojifunzia SHAMBA?


Samahani NASITISHA WAZO!:-(
Swali:
 • Hustukii kuwa ni kweli kuna Masista DU na Masela MZANI TANI ambao hawakuchekei wakistukia wewe MKULIMA?
 • Hivi unaamini kilimo cha mkono na hata kile cha trekta vyote vinastaili kuwa na jina moja kuwa eti vyote ni KILIMO?
 • Unakumbuka kutishika kama unajua Tanzania huita kilimo ni UTI WA MGONGO wakati ukifuata takwimu na tafiti za C.I .A zilizomo katika C.I.A World FACTBOOK ardhi inayolimika katika Tanzania ni asilimia NNE tu a.k.a 4%?
 • Unauhakika UTI WA MGONGO ni muhimu kuliko KINYEO?


NIMEACHA wazo Mheshimiwa!

Na hebu tufuatilie tena UKIMWI kwa msaada wa CNN idaiwe -HIV vaccine brings new hope


Au tukumbushane tena kuhusu saratani ya nyonyo kwa tangazo hili[Tahadhari zaidi:Tangao hili halikuhusu kama mtoto au unamchezo wa kukwazika au kufadhaika kirahisi!:-(]

Read more...

MAPENZI ya watu na IBILISI!

>> Thursday, September 24, 2009

[Tahadhari : Wazo limepinda ingawa sio sana!:-(]


Kwa kusema unaweza kuwasikia wakisema IBILISI nyoko weee,...
....kwa vitendo utashuhudia wakinene IBILISI yako matamu wee!:-(

Ukiwauliza watadai HATA tunamuogopa MUNGU weee,....
....lakini ukiwastua kwa stori hata za MAJINI na wala sio za SHETANI utastukia na IBILISI wanamuogopa na wanaweza toka baruti weee!:-(
Kwa kifupi nataka kusema:

Binadamu kirahisi ukiwapa uwanja watamsuta IBILISI nikome weee,....
....lakini ukiwafuatilia matendo yao unaweza kukuta kirahisi bila aibu wanakatikia kiuno ya SHETWANI hata bila kutamka IBILISI mtamu wee!:-(

NAKATIZIA WAZO HAPA na NAKUSHAURI jaribu kukwepa lakini ya IBILISI kama unamjali MUNGU ingawa labda hapa najiongelea MIMI MWENYEWE na wala sikuongelei wewe MHESHIMIWA!

Swali:
 • AU?

Naacha na moja kwa moja hebu turudi CUBA kukutana na LOS VAN VAN watupe ILE KITU TAMU hasa KWETU TUPENDAO MIONDOKO iruhusuyo mwanamke na mwanamume kutiana mshawasha katika miondoko ndani ya DANSI kwa kitu kama - Aqui el que baila gana


Au tu tubakie tu na Wakuba LOS VAN VAN wafanye matusi live katika kitu kijulikanacho pia kama -TIMBA POP

Read more...

FAIDA za kuongezea chumvi STORI!

Kama mazingaombwe vile mpaka stori YAKO na POOZEO ya ngono,...
.... ghafla ikisimuliwa hugeuka kuwa KAMA VILE ulifanya mapenzi ya ndoa na wandoa mpenzi!:-(

Na akutishaye kwa ya gono,...
... kwa kuzidisha chumvi akufanya uogope mpaka minyoo na sio tu kaswende na UKIMWI wakati aongeavyo kwako mwenye akili UKIFIKIRIA ni anatukania ubongo wako wenye miakili KWA KUTOFIKIRIA KABLA YA KUONJA angalau usisababishe mimba, shenzi.

Swali:
 • Hivi CHUMVI ikizidi kwenye stori ya kweli si TAMTHILIYA itageuka na kufanya igizo zima liwe ninachezwa kwa stori ya uwongo?

Kumbuka lakini wengi wasimuliao mpaka wa ngumi ugomvi na sio tu malumbano,...
.... wanaweza wakawa hawajashuhudia sio tu malumbano BALI na pia hawajaona hata mtu kapigwa konzi!:-(

SWALI:
 • AU?

NIMEACHA wazo!

Hebu Jay Z na Pharell wanadishe katika-Excuse me MISS


Au tu Jay Z, Rihanna na Kanye wadanganye katika-Run THIS TOWN

Read more...

Labda kuna ukweli hata KIRUKA NJIA mwenye sura mbaya JAMII humzidishia kazi kwa MALIPO kama ni ya nyanya basi ni za bei RAHISI!:-(

[Tahadhari: Stori hii utafiti wake haukufanyika gizani na haujakamilika!:-(]

Lakini:

Jamii ikiamini unasura mbaya,...
... haikusamehi ujinga kirahisi KAMA WATOTO WAZURI hasa kama unasura kama kikwapa na mafanikio inaaminika hayajakuzingira.:-(


Na kwa kuwa KWENYE JAMII kuna waaminio kuna wenye sura mbaya,...
..... waaminio hivyo jihadhari nao kama una sura mbaya kwa kuwa hata wakiibiwa kwenye UMATI WA DALADALA wamuhisio kwanza NI MWIZI ni wahisiye ana sura mbaya ALIYEKUWEPO kwenye mazingira.:-(

Chakutisha ni kwamba huku mbaya,...
.... huko kwa wengine kwa uzuri kaumuka utafikiri kalishwa hamira.:-(Na kwa wadhaniao wewe una sura mbaya,....
...wakistukia na hali yako kimafanikio NI mbaya , wengi wao wanahisi unazidi ubaya kwa kustukia hali yako na akugaiaye pendo katika hali hiyo basi udhaifu wake kwako hauko katika sura.


Chakusikitisha ni kwamba inasemekana makazini hasa kama ni mwanamke ndio mwenye sura mbaya,...
.... anaweza cheleweshwa kupandishwa cheo na ukilinganisha na bosi amfikiriaye ni KISURA na kirahisi KISURA MBAYA atalipwa mpaka MDOGO wa mshahara.:-(

Na yasemeka makazini vidume akina dada wawapendao sura SI KAA SIYE wenye sura mbaya,...
.... wao VIDUME WALIMBWENDE wakimshika hata tako mtu ni ruksa na watachekewa WAKATI siye wenzangu na mimi tutashitakiwa kwa SEKSHO HARASIMENTI na, na kukunyiwa na sura.:-(

WAZO LIMENISHINDA!:-(

Swali:
 • Kwani kuna ukweli wengi waaminikao kuwa wanamiakili sana huwa wana sura mbaya?
 • Si umestukia ukipenda mtu basi unamuona mzuuuriiiii?
 • Umestukia kama unamchukia mtu na bado KISIRI unastukia wake uzuri AKIKUCHEKEA kuna uwezekano akikutongoza hata ukimnyima majaribuni alishakuingiza na labda vigezo vya UCHOYO ni kuogopa dhambi au mashoga zako watasemaje wakistukia wajuaye unamchukia chachandu umemgaia?
 • Si unakumbuka akuonaye mbaya kuna wamuaonao mbaya na kama upendavyo ukipendavyo kuna watumiao nguvu kwa sababu hizo hizo zako kukichukia?
HAKI YA NANI TENA WAZO HILI LIMENISHINDA !
Lakini kumbuka ni WAZO TU Mheshimiwa !
Hebu twende Mexico kukutana na Instituto Mexicano del Sonido


AU tu tubakinao tu Mexico walete kitu -ALOCATEL

Read more...

Kama kuna AAMINIYE kwa kuwa kimeandikwa KITABUNI!

>> Wednesday, September 23, 2009

Kilichoandikwa,....
....labda kimepitwa na wakati au kinahitaji tena kuhaririwa!:-(

Haki ya nani tena kama ni zamani kiliandikwa,...
... labda ukweli wake ulikuwa sahihi zamani na umuhimu wake LEO labda ni kama unataka TU kujua ya kitu historia.:-(

Na kumbuka tu kwa kawaida historia huwa inaandikwa,....
..... na walioshinda wakati inawekwa hiyo historia.


Na historia ya wanyonge hata ya AFRIKA iliyoandikwa,...
.... karibu yote haikuandikwa kwa mtazamo wa wanyonge hata hao Waafrika WALIOPEWA KIBANO ambao labda bado wanaugulia.:-(

Kumbuka ni vigumu kwa chochote kufikiriwa kuandikwa,...
....kama yamuhusuyo NA LABDA AYAJUAYE KWA UNDANI ananjaa na matatizo kibao mengine ya kufikiria.


Na labda kweli kuna umuhimu wayakale yaliyoandikwa,....
....lakini jihadhari na utafsirivyo YALIOANDIKWA ENZI ZA KALE ZA hata za JANA na kuyaoanisha na MCHEUO WA LEO ukugusao kama wewe kweli unamchezo wa kufikiria.:-(

Swali:
 • Hivi wewe huwa unatafsiri mwenyewe au unatafsiriwa?
 • Hivi uaminicho unauhakika si kwakuwa umekisoma kama sio umesomewa kilichoandikwa na waliowanukuu ambao walifikiria?
 • Hivi huwa unasimulia kwa juhudi historia yako ya kweli ya wakati unabwengwa AU TU KUPIGWA KONZI kama usimuliavyo ikiwa wewe ndio umebwenga mtu halafu ukamrukia kichwa kabla ya kumpiga ngwala na kumfyonza NYOOOOOO huku unamtemea mate?
Samahani ngojea nibadilishe nyoko na kulainisha aina ya maswali au TU kubadili aina ya cha kuuliza KATIKA swali :
 • Umevaaa chupi?
 • Si unakumbuka mara nyingi hata usipomjibu mtu swali KWA STAILI NA MKAO WA KUKAA KIMYA huwa LAKINI tayari unakuwa unajua jibu?


DUH!
NAACHA na ni wazo tu MKURUGENZI na wala USITISHIKE!

Hebu tubaki Ivory Coast tushuhudie Waafrika tujulikanacho nacho a.k.a kukata kiuno katika miondoko ya sindimba ya huko a.k.a MAPOUKA


Au tupoteze muelekeo na kwenda MIAMI kwa lengo lilelile la kufananisha ukataji kiuno kwa msaada wa PITBULL wakati anadai-I KNOW U WANT ME[calle ocho]

Read more...

Wakati na wasiwasi kuwa asilimia kubwa ya wachawi sio bado MAFISADI!:-(

Swali:

 • Hivi kisirisiri hudhani katika mazingira ya sasa hivi bongo mafisadi wanafaidi halafu hata WACHAWI AMBAO NAO WANAFISADIWA bado nao FISADI hawamlogi?
 • Unauhakika UFISADI ni nini?
 • Kwani hisia zako zinadhani wachawi wengi ni mafisadi?
 • Unauhakika MAZINGIRA yakikuruhusu HASA siku hizi mafisadi wafaidizo WEYE hutaki kuwa FISADI?INAAAMINIKA:
Binadamu wana tabia zao,....
..... wasichonacho wataka kiwe chao.

Na watu wenye yao,....
..... ndio wafaidikao kwa kuonjesha vyao kwa wasio na vyao.

Wakati wakijifanya kwa kuonjesha wanasaidia hao...
.... wasio na chao ingawa hawana kwa kuwa wananyimwa na MAFISADI hao wenye vyao.

Na si bure waliozidiwa na vyao wakijifanya burebure wanamegea wengine vyao,...
..... kwa kuwa LABDA wajilimbikizi wasivyovihitaji wao NA kumbuka HASA watu WAKIJIZIDISHIA hata UBWABWA, moja ya hofu yao ni usije kuozea kwao.

Jihadhari na vya bure vyao,...
.... kwa kuwa ndivyo vikununuavyo kuliko ulivyovinunu kwao.

Na kama unanunua kwao,....
..... basi kumbuka unawahitaji na bado uko ndani ya makucha yao.

Lakini hata kama hawategemei wewe ununue kwao,....
..... kumbuka bila wewe wadhaniaye UNAVIHITAJI na KUWAONEAGELE wao, havina maana walivyonavyo na KUJILIMBIKIZIA mafisadi shenzi-nyoko hao.

Lakini cha ajabu, mpaka wachawi waliokuwepo ulipokuwepo na MAFISADI hao,....
..... waweza kukuta watamaniye ZAIDI kumloga ni weye uhangaikaye kujikwamua na sio FISADI yule AWAFISADIYE ili ubakie tu kama wao.


Swali:
 • Kwani hujastukia Watanzania wengi na naweza kusema Waafrika wengi[sio wote] wapendavyo kushushana wao kwa wao na kupenda kusifia wengine ambao wanafikiri WANA zaidi ya ya KWAO?

NI WAZO TU KIJEBA na kumbuka wala hii sio Korani wala BIBLIA!:-(

Tubadili kidogo kwa kupata kitu kutoka kwa Werrason katika muradi-Techno Malewa


Au tu twende Ivory Coast Nastou alete-Voici Lolo

Read more...

UKILEGEZA akalegea!

Kulegeza kitu ni lugha na watu huielewa kwa kuwa huumua kama hamira,....

.... na ukilegea kwa kulegezwa ni udhaifu na jihadhari na kinachokulegeza hasa usichokitambua kama kazi .


Na kulegeza mdomo kwawezaongea we taahira,....
.... wakati kulegeza macho kwaweza mtambulisha mtu kunakitu anapatia na ndio sababu ushaanza kurembulia macho uitarajiayo kazi.

Kulegeza kamba KATIKA MAKUZI ya TOTO ni aina YA kuonyesha dira,....
.... hasa kama kukaza kamba huonyesha umfunzaye mpaka aina la vazi.


Swali:

 • AU?

Na kwa binadamu walivyo wabishi, kulegeza KWAO kwaweza kaza,
... na ukikaza kwaweza kuwaLEGEZA.NI WAZO tu na usipolielewa WEYE endeleza SENDEMA TU kinamna Mheshimiwa!


Hebu tubadili kidogo basi kwa kumsikiliza Gregory Isaacs akiomba agawawiwe tena katika-One more time

Au tu THIRD WORLD warudie -Lagos Jump

Nipo na Asanteni Wadau wote msionichoka baadhi mkiwemo katika picha zangu hizi za juzi ya jana...


Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket

PhotobucketPhotobucket

Photobucket
Photobucket


PhotobucketPhotobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucket


Photobucket

PhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucket

Read more...

TATIZO la KUDHANI kwa kuwa hukioni KITU basi HAKIPO na HAKIKUHUSU!

>> Thursday, September 17, 2009

Ukifumbia macho jambo,....
.... kwa staili hiyo BADO huliondoi JAMBO!:-(


Na ni UNAFIKI kujifanya unashtushwa HATA na kifo,...
.... kwa kuwa safari hii ni NDUGU au JAMAA umjuaye KAFA au kakumbwa na KIFO.


Na ni kukuza ujinga,...
.... kwa kutotaka kuelewa ya WAJINGA kwa kuwa unaamini YAKO NI YAKIEREVU na wewe sio MJINGA.


Na ukisubiri MPAKA ukabiliwe na tatizo ndio uelewe wenye matatizo,...
.... ni wewe mwenyewe ujiwekeaye kiporo cha mshituko na kuchanganyikiwa likikukumba hilo TATIZO.

Na kwa kuwa yasiyokuhusu unayafumbia macho,...
.... kumbuka tu kwa kawaida YASIYOKUHUSU kila siku yako macho na yanakukodolea MACHO!

Swali:
 • Hivi wewe ni miongoni mwa wamuonaye aliyevaa nguo wasahauo aliyevaa nguo chini ya nguo yuko uchi?
 • Unakumbuka kuingilia yasiyo kuhusu ni kawaida na tatizo huja tu UKIVUKA MPAKA na kujifanya ya mwingine yasiyokuhusu yana umuhimu kwako kuliko yanayemhusu?


NI HILO TU na NI WAZO TU MHESHIMIWA!

Tutaonana JUMATATU HAPA KIJIWENI kama sijafa na na nguvu na muda wa kublogu !:-(


Mpaka siku hiyo basi MI NAANZA kivyangu na nakutakia kila la KHERI KWA YAKO YAKUKUNAYO ROHO MKUBWA!

Au mpate MARIJANI RAJABU kwa hisani ya TIZEDBOY azungumzie-SALAMAAu tu DULLY SYKES akumbushie-HUNIFAHAMU

Read more...

LEO NI KRISMASI! HEPIBESIDEI MKUBWA!

Kama wewe ni miongoni mwa waaminio leo ni tarehe 17.09.2009.


Swali:

 • Unakumbuka tofauti ya JULIAN Calendar na Gregorian Calendar,
 • Kwani wewe nawe unaamini kuna kelenda sita tu ambazo ni ya Kigregory, Kiyahudi, Kiislamu, Kihindi, Kichina na Kijuliani kama wataalamu wengi wadaivyo?[Gregorian, Hebrew, Islamic, Indian, Chinese, and Julian Calendars]

 • Unauhakika kweli unamiaka mingapi weye mwanakwetu?


Kumbuka tu kumshukuru Papa Gregory wa kanisa la Kikatoliki kama unaamini leo ni Alhamisi terehe Kumi na Saba , Mwezi wa Tisa, Mwaka 2009 kwa kufanya kalenda uitumiayo ichukuliwe kuwa ni kweli.

Jisomee somee mwanakwetu ili ustukie angalau hata kuhusu swala liwezalo kusababisha kuanza kupata suluhu ya swala la umri wako likusababishalo umuone jirani mwenye umri sawa na wewe kazeeka na hamtakufa dakika moja kwa uzee moja ya sababu ni nini.!

Cheki tu hata hapa ujikumbushe historia ya KALENDA kunoga.

NIMEACHA MKUU na hili ni wazo tu NJONJOLI na wala USITISHIKE!

Au jikumbushe kalenda ya WAMAYA katika -Mayan Calendar Explained


Kama topiki ya kalenda inakuboa unaweza kurudia kujikumbusha tofauti za kuoga kati ya Wanawake na Wanaume katika-How to shower like a woman/Man

Read more...

MWENYE NJAA!

Mwenye njaa tu ukiwa
Chakula chako huliwa
Waitwa mtuhumiwa
Na yako kuchukuliwa.:-(


Silaumu mwenye njaa
Bado busara kajaa
Ila tumbo lenye njaa
Ni kichwa cha mwenye njaa!:-(


Leo kwako kesho kwake
Na mnyonge mpe chake
Ukisahau tu yake
Wewe hujali tu yako!:-(Swali:
 • Hivi si ni kweli UKIWA NA NJAA stori za chakula ndio zikufanyazo uwe MAKINI ZAIDI?
NIMEACHA , halafu kumbuka hili ni WAZO TU FUPI la leo Mheshimiwa!!

Hebu tujifunze kuwa Mbwa anaweza kutembea kwa miguu miwili huku anakojoa...-Chester, the incredible peeing dogAU tuwe tu makini na KWENDA DARASANI kujifunza tena moja ya mtazamo wa DINI na Professor Jared Diamond wa University of California, Los Angeles [Phi Beta Kappa Award in Science (1997), Royal Society Prize for Science Books (1992, 1998 & 2006) Pulitzer Prize (1998), National Medal of Science (1999)], katika -The Evolution of Religions

Read more...

WALEVI na UZURI!

JINSI unavyozidi kulewa,....
.... ndivyo mbaya azidivyo UZURI!

:-(
Swali:
 • Kwani hujui hilo?
 • Si unakumbuka pia JINSI unavyozidi KUAMINI ndio DINI YAKO izidivyo kuleta MAANA?

NI HILO TU!

Hebu tubadili kwa kuingia shule kujifunza tena kitu katika VIPENGELE VYA MWILI WA BINADAMU.
[Tahadhari: Kama ni mtoto au Muzee wa kukwazika usiangalie video zinazofuata]


Tupate basi elimu ya jinsi kipengele cha nyuma kinavyokaguliwa na Dakitari
-Rectal exam


Kama una muda unaweza kuangalia JINSI kipengele cha mbele cha mwanaume kinavyo kaguliwa na daktari-Male genitalia examinationUnaweza tu pia kujifunza kipengele cha kike a.k.a kidude -Vagina Exam

Read more...

WAKATI unachagua MCHELE!

>> Wednesday, September 16, 2009

Kwa kupepeta MCHELE,...
.... uondoacho ni pumba na hapo huchagui MCHELE!


Na wakati unachagua ukikuta HINDI kwenye MCHELE,...
... hindi ni uchafu NA HUONDOLEWA kama MAWE tu kwenye MCHELE.


Na kama huna mchele,....
...NI ALINACHA kufikiria sana jinsi utakavyochagua mchele kama huweki mikakati utapataje kwanza MCHELE.

Na wakati hupendi mahindi na unasifia sana MCHELE,...
...... kumbuka wenye kipindupindu muonekano wa uharisho wao ni rangi ya MCHELEMCHELE.:-(

NA wakati unaringishia wenye mahindi mchele,...
... kumbuka JELA YA WANAUME TUPU wengine huwatibu matibabu wenzao MATIBABU ambayo kwa kawaida hutibiwa na wanawake na hapa siongelei MCHELE!:-(

Swali:
 • SI unakumbuka huhitaji kunielewa naongelea au KUMAANISHA nini?

NIMEACHA na nakutakia siku yako iwe MCHELEMCHELE!

Ngojea Louis Armstrong aendeleze madai kuhusu dunia hii nyoko - What a wonderful world!


Au tu RAY CHARLES adai-HIT THE ROAD JACK

Read more...

Nafasi ya ALIYEKUPA KIDUDE KWA HURUMA akishakupa kidude KWA HURUMA!

Kama umeshapewa kidude,...

..... wewe ni bingwa kwa wasionacho KIDUDE wakihitajio NA ni kweli unacho KIDUDE hata kama aliyekupa ALIKUGAIA kidude kwa kukuonea HURUMA!

PAMOJA NA YOTE; aliyekupa kidude,...
... kumbuka ALIKUGAIA SI KWA KUWA TU ANAHURUMA, bali kwa kuwa KWANZA alikuwanacho kidude au alikuwa na uwezo wa kukupa kidude na labda ALIKUWA NA UWEZO WA KUKUGAIA hata BILA kukuonea HURUMA.:-(

Na kama unabisha , kumbuka tu HILI ; hata ufanyeje ,KAMA HUNA kidude na huwezi kumsawazishia mtu atakaye kidude angalau apewe na mtu mwingine kidude,...
...HAZIMTIBU KITU MTU ZAKO HURUMA kama matibabu ya mtu ya MKUNO yanahitaji tu kidude na SI HURUMA , hata kama ni kweli unamuonea HURUMA.

Kumbuka pia hata umjuaye KWA UZOEFU huwa ukitia huruma anakugawia kidude,...
....kumbuka kuna awanyimao BILA SABABU MAALUMU hata watieje HURUMA.:-(

Na kama unamchezo wa KUONA HURUMA KIRAHISI na una kidude,...
..... kumbuka DUNIANI kuna watongozaji wasiostahili ZAKO HURUMA ambao STAILI ZAO TU ZAKUOMBEA KIDUDE ni kutia HURUMA!:-(

Halafu kumbuka kuwa kama hupendi kuonewa huruma na WEWE NI MPENDA kula ulichokitolea jasho MWENYEWE kidude,...
....ukihisi umeonjeshwa kidude kwa KUONEWA HURUMA daima kidude hicho hakitanoga kwa LADHA FULU YA UONJO kwa kuwa wakati UNAKIGIDA KIDUDE kuna kitu kitakuwa kinaondoa au kupunguza FULU MRIDHIKO kwa kukukumbusha unagida tu UGIDACHO KIDUDE kwa kuwa TU umeonewa HURUMA.:-(


Na kama wewe ndio ugawaye kidude,...
.... kumbuka kama ushakigawa kidude na kimeliwa, huruma zako zimeshafanya kazi yake na hata ufanyeje makali ya mgao huo yalishapita KILELE CHAKE na kidude CHAKO NDIO kimeshaliwa hivyo TENA , hata kama SASA HIVI uliyemgaia kidude UMESTUKIA HAKUSTAHILI KUGEWA KWA HURUMA na humuonei tena HURUMA.:-(Swali:
 • Ujastukia kuwa ni rahisi kuingia unyonge kwa aliyewahi kukusaidia kwa kukuonea huruma?
 • Unafikiri Rais wa Tanzania katika ziara zake ughaibuni za kutia huruma ili Tanzania igawiwe kidude mwaka huu, haingii unyonge mbele ya aliyegawia mwaka jana Tanzania kwa huruma kidude, kwa kuwa tu anakumbuka na mwaka jana alihurumiwa tu alichopewa kidude?
 • Kwani unataka kudai hujawahi kustukia kuna ulichonacho kidude ambacho unacho kwa kuwa aliyekugaia alikuwa anakuonea tu huruma?
 • Unajua mazingira yakijiweka sawa kukuvumbulia unahitaji kidude ,inawezekana ni wewe utakayeshinda kwa kutia huruma ili upewe KIDUDE?


Samahani NALIKATIZIA wazo hili nyoko HAPA Mheshimiwa!:-(

KUMBUKA lakini HILI NI MOJA TU YA mtazamo katika WAZO tu MHESHIMIWA Kishtobe au weye MHESHIMIWA Bitozi !
Na KAMA HULIELEWI HILI WAZO wala USITISHIKE Mheshimiwa!Ngojea Milli Vanilli watupeleke zamani kiduchu katika-GIRL, I am gonna miss U


Au ngojea LL Cool J aibakize hukohuko zamani katika-Phenomenon

Read more...

Unafikiri ni kweli UNAFANANA NA PICHA ZAKO unazozipenda?

>> Tuesday, September 15, 2009

Watu hukwepa hali halisi,...
.... na halihalisi inaweza kuwa ni sura nyembamba halafu BOMBA LA PUA!


Na kwa kuwa unatetesi ya nini ni hali halisi,...
.... katika kukwepa kudhihirishia umati kuwa NI KWELI ulichokuwanacho si mwanya BALI ni bonge la PENGO ,wawezakujikuta uchaguapo picha utakazo UMMA ukutambuenazo MAPOZI YAKO ni yakukwepa KUCHEKELEA KANYAU kwa kujifanya unapenda mapozi ya kununia hata kivuli kama vile kina JOTO LA JUA.Na ni kweli hali halisi,....
.....pamoja na mengine yote kama ya KUTOPENDEZA KWA UHALISI wa MUONEKANO wa USO KWA USO, inaweza pia ikawa INANUKA KIKWAPA badala ya kunukia kama UA.:-(

Swali:
 • AU?
 • Kwani unataka kusema hujastukia watu wengi hawafanani na picha zao wanazokuonyesha ukikutananao uso kwa uso?

NI HILO TU weye MHESHIMIWA utuonyeshaye PICHA NZURI !

Hebu tuiangalie AFRIKA idaiwavyo na baadhi ya watu inavyofanana katika picha...-The Africa They Never Show You.

Au tu STING na CRAIG DAVID wabadili kwa kitu-RISE&FALL

Read more...

UNAWEZA KUSAHAU ulipokwenda msalani ULIKOJOA PIA kama kilichokupeleka chooni kililenga KUNYA!

Kumbuka tu,...
....KABLA ya kukifikia unachofikiri ni MUHIMU,....
........ulivyovipita hapo katikati NJIANI wakati unamendea na kukiendea UNACHOFIKIRI NI cha muhimu, NAVYO ni MUHIMU,....

... na LABDA vina umuhimu wake hata katika KULIFANYA hilo ulengalo UDHANI ni la MUHIMU.

:-(

Swali:
 • Si unakumbuka BINADAMU ni wasahaulifu na vingi wavikumbukavyo labda ndio sio vya MUHIMU?
 • Si unakumbuka huwezi kutafsiri au kujua tu NI nini MUHIMU kama hakuna udhaniavyo si muhimu?
 • Hivi unafikiri kuna binadamu ambaye ni muhimu SANA mpaka akifa dunia itasita kuzunguka kwa kuwa katutoka aliyekuwa muhimu sana na pengo lake kwa dunia halizibiki?{kumbuka siongelei swala la limtu binafsi na lifamilia lake, rafiki au limchumba}
NI HILO TU na NI WAZO TU weye MHESHIMIWA uliyesahau kuwa KAMA uliwahi kubadilishwa NEPI basi weye ulishawahi kuwa KIKOJOZI!:-(


Ngojea BLAXX abadili kwa Soca katika kitu kiitwacho-TUSTY


AU tu ROSE MUHANDO apindishe muelekeo wa wazo lako lililoanza kukaa kimatumbi baada ya kumsikiliza BLAXX hapo juu kwa kitu-NAKAZA MWENDO

Read more...

Kuna uwezekano WEWE NI MHUNI!

>> Monday, September 14, 2009

Ndio!

Kunauwezekano kama unafikiri wewe sio MHUNI labda kweli wewe sio MHUNI!

Lakini kama huamini wewe ni mhuni wakati ni kweli weye ni mhuni haibadili ukweli kuwa WEWE NI MHUNI!:-(

Swali:
 • Kwani hujastukia hata WAHUNI sio sehemu zote wafanyacho hujulikana ni UHUNI?
 • Kwani hujastukia hakuna mhuni afanyaye uhuni masaa ishirini na nne ndani ya siku?
 • Kwani unauhakika na kwalifikesheni zisababishazo mhuni afuzu kuwa ni MHUNI zikusababishazo UWE NA UHAKIKA wewe sio MHUNI?

NI wazo tu MHESHIMIWA na labda naamini wewe WALA SIO MHUNI!

Ngojea ni muachie TITI kutoka Senegal aongelee-LOVE YOU
Au tu twende Mali, Salif Keita amuongelee-African Woman

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP