Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mheshimiwa Mzee , TOKA CHOONI BASI na wengine waingie!:-(

>> Monday, September 28, 2009

[Tahadhari: Neno tamu CHOO halina maana ya CHOO katika taralila hii!:-(]


Kwako MWANASIASA MKONGWE wa Tanzania!


Wadai we' mzoefu
Twajua we' maarufu
Wasahau udhaifu
Ni choo kung'ang'ania


Ukiingia utoke
Kung'ang'ana usitake
Damu mpya ndio pake
Unapopang'ang'ania

Usilale TU chooni
Kunya wengine makini
Twasali madhabahuni
Toka tu basi chooni!


Ukipitwa na wakati
Umepitwa na wakati
Achia TU madhubuti
Nao pia wathubutu!


Swali:
  • Hivi kwanini unafikiri kuna wanasiasa VIKONGWE ambao hawataki kuachia wengine nao wajaribu hasa ukizingatia hata kama kunakipindi mchango wao ulikuwa unaonekana basi kipindi hicho kishapitwa na wakati?

  • Unauhakika mbunge wako sio walewale waingiao chooni halafu hawataki kutoka?[Samahani! katika sentensi ''Waingiao chooni'' nilitakakuandika na kumaanisha ''Waingiao Ofisini''!:-(



DUH NASITISHA WAZO HAPA halafu ngojea niende CHOONI tu kidogo Mheshimiwa !
WAKATI NIMEACHA kumbuka hili ni WAZO TU Muungwana!

Ngojea FOXY BROWN akiweka spin yake kwenye wimbo wa Jimmy Hendrix abadili hali ya hewa KIJIWENI HAPA kwa kitu -ART OF WAR[Tahadhari: Lugha chafu!:-(]



Au tu Foxy Brown andelee tu kufafanua kipengele-Hot Spot[Tahadhari:Lugha inaweza kumkwaza mlokole!:-(]

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:59 am  

Labda kwa vile wamezoea kuwa na cheo na pia wanaogopa kwa bila cheo. Kushika jembe na kulima au basi ni ujinga yaani kuwa na fikra duni.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:48 pm  

kuna mmoja nataka nimfurumue humo chooni. subilia muziki wake

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:48 pm  

kuna mmoja nataka nimfurumue humo chooni. subilia muziki wake

Simon Kitururu 3:38 pm  

@Dada Yasinta: Mara kibao huwa nawazia hili nikistukia viaongozi waliofikia kujiaminisha ni wao tu wanaweza!:-(
@Mkuu Kamala: Kila la kheri kwa hilo Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP