Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama NIA YAKO ni kumfunza KINUKA MKOJO aanze kunukia PAFYUMU!

>> Friday, September 04, 2009

[Tahadhari: Stori hii haina uhusiano na MKOJO!:-(]


Kwa kawaida KINUKA MKOJO akishazoea kunukia PAFYUMU,...
...hujifanya kasahau kuwa alikuwa ananuka MKOJO.:-(

Na kwa kawaida KINUKA MKOJO idaiwaye ni MSTAAFU anukiaye manukato siku hizi akikutana na KINUKA MKOJO bikra hujifanya ANAFYUMU,...
.... na anaweza mpaka afanye watu wote wamstukie ANUKAYE MKOJO/WAPAFYUMU BIKIRA mpaka utafikiri yeye mwenyewe anakojoa PEPSI TU siku hizi wakati ni rahisi yake KUYAJUA hata bila kumuona akienda haja, HASA kwa kuwa siku hizi yeye ni mvivu wa kufua mwenyewe na WAMFULIAO CHUPI ZAKE hawana siri ya kuwa KWA KAWAIDA chupi yake HUWA ina bomba za DOA ZINUKAZO za AINA MBILI na ziko sehemu mbili ,na moja linukalo zaidi huwa si DOA la MKOJO:-(



Na usishangae, ni kawaida mchango wako kusahaulika na KINUKA MKOJO baada ya kujulia PAFYUMU,...
.... na ushauri ni kwamba HATA KAMA HUJAWAHI KUWA KINUKA MKOJO jihadhari na KINUKA MKOJO MSTAAFU anayejifanya kasahau alikuwa ananuka MKOJO!.

Kumbuka lakini kwa kawaida KINUKA mkojo wakati ananukia ya mkojo PAFYUMU,...
... pua HUWA inazoea hayo manukato ya mkojo na kama UKITAKA KUMSAMEHE kwa kunuka kumbuka ni kawaida kwa aliyeizoea harufu anaweza asisitukie ananuka HATA ikiwa anukacho ni MKOJO na akigundua watu walikuwa wanajua ananuka MKOJO hujitahidi hata akibanwa haja ndogo HUJITAHIDI angalau kutembea kama kabanwa na USHUZI ilitu kuepuka tusijue mwendo wake unauhusiano na MKOJO!:-(

DUH nalikatiza wazo!:

Lakini MASWALI mchanganyiko kiduchu:
  • Unauhakika naongelea nini?
  • Unajua KWA WAKUANGALIAO ni vigumu kuwaficha kuwa umebanwa na mkojo kwa kujaribu kujifanya unazuia ushuzi?

  • Unakumbuka anukaye kikwapa hukizoea kikwapa na wasumbukao ni wengine na sio mwenye kikwapa?

  • Ushawahi kukutana na tajiri MPYA atakayekujaribu kufanya watu wasistukie juzijuzi alikuwa MASIKINI?

  • Unakumbuka waishio karibu na JALALA LINUKALO huzoea harufu ya jalala na ni wageni watesekao na harufu ya jalala?

  • Unakumbuka msemo wa TENDA WEMA wa kumfunza mtu KUPIGA MSWAKI uende zako usingoje shukurani AKIACHA KUNUKA MDOMO na meno yanang'aa?

  • Unafikiri ni wajanja wangapi wanakumbuka aliyewafunza UJANJA?

NAACHA wazo MHESHIMIWA na nakutakia Ijumaa na WIKIENDI KIBONGE!



Hebu tushangalie tena kidogo kifaa watumiacho siku hizi wasichana KUKOJOA wamesimama kijulikanacho kama-GO GIRL


Au tu twende CUBA Celia Cruz alete tena -Quimbara



Au twende tu Nigeria P-Square waombe-DO ME

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha Wambura 9:08 am  

SK, huu ni ujumbe murua sana kwetu. Unawezatumika katika siasa (soma SIHASA!), makatisani kwa watakavitu wenzio na katika jamii.

Asandu sana mwanakwetu

Simon Kitururu 9:23 am  

@Mkuu Chacha de Wambura: :-)
Asante kwa kunitembelea hapa kijiweni mwanakwetu!

Yasinta Ngonyani 4:06 pm  

Mta. Simon ujumbe wa leo kali kali kali mno. Pia ni ujumbe mzuri. Asante kwa ujumbe kuna kitu nimejifunza.

Simon Kitururu 10:09 pm  

@Sister Ngonyani: Asante kama mahubiri yametekenya eneo!

mumyhery 6:30 am  

Simon na wewe kwa mistari tu!!!

Simon Kitururu 1:40 pm  

@Mumyhery: :-)

Yasinta Ngonyani 3:43 pm  

Simon:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP