Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BURUDANI za KUDANGANYWA!

>> Thursday, September 10, 2009

Unawezabisha!

Kuna starehe zake wakati unadanganyika kabla hujastukia UNADANGANYWA!

Na unawezabisha , lakini kwa kawaida unakuwa umekaa mwenyewe TAYARI mkao wa kudangaywa wakati UNADANGANYWA!

Kwa kawaida kudanganywa ni bomba la STAREHE kwa kuwa kuna KUNA maswahibu yako kwa muda fulani na kukutuliza moyo hasa kama hufikirii kinachoendelea ni KUDANGANYWA!

Wanasiasa wanajua hilo tokea hilo ndio maana hotuba zao asilimia KARIBU zote ni UONGO, na WATONGOZAJI hukubuhu kwa UJUZI wa HILO na bila aibu wanaweza kumsifia mwenye sura kama trekta ana sura kama TOROLI yote ni katika kukuna hisia za MDANGANYWA.

Na MISIBANI ndio kabisaaa, unaweza UKADANGANYIKA kwa kufikiri wote waliao wanamlilia marehemu aliyewakusanyisha msibani, wakati waliao wengi msibani wanawalilia marehemu ndugu zao mpaka marehemu hawala zao kwa kuwa labda hata marehemu wa leo hawamjui vizuri na ukiwauliza katika hilo, WEWE unajitafutia KUDANGANYWA.

Kumbuka tu kuwa hata UTONGOZWE kikweli hata kuhusu dini ya kweli, hutaamini kitu kama umekaa mkao wa kudhani katika kupewa ukweli huo UNADANGANYWA:-(


Swali:
  • AU?
  • Lakini unafikiri ni wote huchukia baada ya kustukia WALIDANGANYWA?
  • Unajua kuna watu wengi wameoa kwa kudanganya na wameolewa kwa kuwa wamedanganywa?

NI hilo tu KINGUNGE na ni wazo tu MBILIKIMO na wala usitishike!


Hebu JIBJAB wabadili kwa kitu cha SOUL TRAIN..



Au tu Brian Adams aulize tena-Have U ever really loved a WOMAN


AU CHRIS ROCK aharibu tena kwa kuongelea -View on Love and Relationship[tahadhari:topiki na lugha yake haikufai kama ni mtoto]

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 2:09 pm  

Have u ever really loved a woman?
Mkuu hapa jibu ntalokupa ntakudanganya tu!

Ila hilo la Brian ni bonge la song!

Yasinta Ngonyani 3:01 pm  

mimi nimogopa kusikiliza wimbo kwa vile bado mtoto:-)

Faith S Hilary 1:28 am  

Chris Rock always cracks me up...so do you Simon...so naweza kusema MSHABIKI wako au?? I know its a different post ila habari ndio hiyo...hehe

Simon Kitururu 3:27 am  

@Papaa Fadhy: Brian ana bomba za sentensi! :-)
@Yasinta: :-)
@Candy1: DUH!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP