Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI unachagua MCHELE!

>> Wednesday, September 16, 2009

Kwa kupepeta MCHELE,...
.... uondoacho ni pumba na hapo huchagui MCHELE!


Na wakati unachagua ukikuta HINDI kwenye MCHELE,...
... hindi ni uchafu NA HUONDOLEWA kama MAWE tu kwenye MCHELE.


Na kama huna mchele,....
...NI ALINACHA kufikiria sana jinsi utakavyochagua mchele kama huweki mikakati utapataje kwanza MCHELE.

Na wakati hupendi mahindi na unasifia sana MCHELE,...
...... kumbuka wenye kipindupindu muonekano wa uharisho wao ni rangi ya MCHELEMCHELE.:-(

NA wakati unaringishia wenye mahindi mchele,...
... kumbuka JELA YA WANAUME TUPU wengine huwatibu matibabu wenzao MATIBABU ambayo kwa kawaida hutibiwa na wanawake na hapa siongelei MCHELE!:-(

Swali:
  • SI unakumbuka huhitaji kunielewa naongelea au KUMAANISHA nini?

NIMEACHA na nakutakia siku yako iwe MCHELEMCHELE!

Ngojea Louis Armstrong aendeleze madai kuhusu dunia hii nyoko - What a wonderful world!


Au tu RAY CHARLES adai-HIT THE ROAD JACK

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:53 pm  

Nimeishiwa la kusema :-( ila najua tupo pamoja!!!

Fadhy Mtanga 3:50 pm  

Mi nshajua unaongelea nini. Kinyundo hicho!

chib 5:20 pm  

Kama huelewi kiswahili barabara na mafumbo yake, unaweza kuchekwa!!

viva afrika 9:20 pm  

naona mawazo yangu bado hayajatenga pumba na mchele, acha niwaachie wanazuoni, na sasa naelekea kula mchele

Simon Kitururu 12:10 pm  

Asanteni wote!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP