Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MWENYE NJAA!

>> Thursday, September 17, 2009

Mwenye njaa tu ukiwa
Chakula chako huliwa
Waitwa mtuhumiwa
Na yako kuchukuliwa.:-(


Silaumu mwenye njaa
Bado busara kajaa
Ila tumbo lenye njaa
Ni kichwa cha mwenye njaa!:-(


Leo kwako kesho kwake
Na mnyonge mpe chake
Ukisahau tu yake
Wewe hujali tu yako!:-(



Swali:
  • Hivi si ni kweli UKIWA NA NJAA stori za chakula ndio zikufanyazo uwe MAKINI ZAIDI?
NIMEACHA , halafu kumbuka hili ni WAZO TU FUPI la leo Mheshimiwa!!

Hebu tujifunze kuwa Mbwa anaweza kutembea kwa miguu miwili huku anakojoa...-Chester, the incredible peeing dog



AU tuwe tu makini na KWENDA DARASANI kujifunza tena moja ya mtazamo wa DINI na Professor Jared Diamond wa University of California, Los Angeles [Phi Beta Kappa Award in Science (1997), Royal Society Prize for Science Books (1992, 1998 & 2006) Pulitzer Prize (1998), National Medal of Science (1999)], katika -The Evolution of Religions

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 5:09 pm  

Mkuu si unajua lakini nikiona mashairi huwa nanogewa kiasi cha kuacha hata kuchagua mchele? Hapo umenogelesha kwa staili ya asiye mchoyo.
Tupo pamodzi.

Faith S Hilary 10:45 pm  

Oh my god the dog just made me wonder mpaka sijaelewa what is going on...lol...oh my god...lemme go to the toilet...brb

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP