Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

YA WENGINE yakisaidia kukukumbusha YA KWAKO!

>> Wednesday, September 02, 2009

Unaweza ukampigia chabo CHEUPE DAWA,....
.... akafanya ujistukie kuwa weye ni CHEUSI DAWA kama mimi.



Na unaweza kuona tajiri,...
....ukakumbuka jinsi ulivyo masikini.

Unaweza pia kustukia WAKRISTO,...
....wakafanya ujifunze zaidi kuhusu UISLAMU.

Ila jihadhari tu kama kwako ukienda HAJA kunakukumbusha KULA,...
.... hasa kama CHAKULA na VIFYONZO/kilainisha kiu , NI vya kubahatisha au mipango na mikakati ya kuvipata leo tokea jana kulikuwa HAKUNA.


Nikiacha utani!:-(

Kama ukitumbulia macho wengine unajiona wewe,....
... au vyako hukusaidia kuwafikiria na kuwaongezea wengine, ...
....BASI kunauwezekano WEWE ni BOMBA la mtu na unastahili hata kwa mara nyingine kuchumbiwa au tu kupewa tendo walifuatilialo wachumba kama tu angalau ushasawazisha ya chumba !


NIMEACHA wazo na KUMBUKA HILI ni wazo tu KIBOSILE!






Swali:

  • AU?
  • Kwani ni lazima mpaka uwemtaani NA kwa bahati mbaya ufanikiwe kukipigia chabo KIFICHA NYETI/kitunza eneo cha mtu MWINGINE ndio ukumbuke kuwa wakati unavaa kabla ya MTOKO ulisahau kuvaa kificha nyeti!CHUPI?



Ngojea ukumbushwe MUHAMMAD ALI asili yake sio MBEYA au KILOSA bali eti ni Ireland



Samahani siku yangu iko fastafasta kidogo leo kama spidi na sauti ya Daddy Freddy katika-Haul &Pull



AU nafikiri ni kama Daddy Freddy katika-Bring the Girls

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:25 pm  

Duh! Mkuu wiki yote nilikuwa najaribu kuweka maoni MAWAZONI ikawa inanigomea.
Kama kawa, pamoja kama mchafukuoga na chawa!

Simon Kitururu 8:45 pm  

@Papaa Fadhy: Sijui kwa nini iko hivyo kwa kuwa na Muzee Black a.k.a Blackmannen amenistua siku si nyingi zilizopita kuwa inamzingua kuweka maoni. Lakini sijabadili kitu na nashangaa ni kwa nini wengine inaruhusu na wengine inawadengulia wakati muegesho ni KWA YOYOTE MAONI RUKSA!:-(

Tuko pamoja lakini Mkuu!

Chacha Wambura 9:29 am  

Kwani kuna tofauti kati ya cheupe-dawa na cheusi-dawa ama kimojawapo kati ya hivyo kinakaribiana na chekundu-dawa?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP