Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI umestukia KWA NJE kibwengo ni FASHENISTA!:-(

>> Saturday, September 12, 2009

KWA bahati mbaya hakuna UHAKIKA na YA NDANI!:-(

Ya ndani ni MWANANDANI,...
.... na ukichokoza waweza kutoka damu au kuwekwa NDANI.

Na ukichokonoa zaidi katika nia ya kuchungulia, waweza ukakuta kuna giza ingawa yasiyokodoleka labda yana miba NDANI.

Lakini labda tubaki na yalio NJE ambayo kwa tumtafutaye undani BADO anapendeza kwa nje tusipochunguza wake UNDANI.:-)

NDIO!
Kwa kawaida FASHENISTA anapendeza kwa nje na kama nia ni kumsifia alivyopendeza, bakia nje INGAWA NJE LABDA NDIYO ambayo ikupayo dalili za labda KIBWENGO AMBAYE UNAFIKIRI NI MZURI KWA KUWA KAPENDEZA KWA NJE, ukweli NI kaoza NDANI au anatibu udhaifu wa ndani kwa kupendeza nje ya NDANI.:-(


Na ni kweli kama fashenista anajulia UFASHENISTA hata kama taahira , huwa anapendeza kwa nje kama hunogewi kumdadisi yake ya NDANI!:-(

Swali:
  • Lakini si ni kweli UKIPENDA kwa kuwa nzuri NJE NA karibu ya nje kwa kudonoa na kukodolea kwa juujuu, huwa baada ya muda kiduchu utastukia haitoshi kwa NJE au juujuu ya karibu na sebule ya nje na utataka ujue kama kipanulio misuli yake inabana kwa ndani ya chumba cha ndani?
  • SI unakumbuka hata ukimstukia taahira kwa JINSI TU alivyo kwa nje, bado utaahira wake MAKAO MAKUU YAKE ni kwake hasa KICHWANI MWAKE ndani?

NIMEACHA wazo MHESHIMIWA na kumbuka ni wazo tu NJONJOLI usitishike !:-(


Hebu tubaki Afrika Bunny Mack aongelee tena -MY SWEETIE


Au turudi JAMAIKA Tony MATTERHORN arudie tena kitu -DUTTY WINE



ASANTENI WADAU WOTE mnao nitembelea hapa au tu msionitenga uso KWA uso !
Baadhi mpo katika BAADHI ya picha zangu za juzi ya jana hizi...

Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket


Photobucket





Photobucket




Photobucket





Photobucket








Photobucket




Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 12:08 am  

lol...haya mawazo they are nice! and very nicely put together na inaleta maana...ila sitosema what it means to me ili watu wengine waingie "mawazoni"...n by the way has anyone told you kwamba you have "baby face"?....lol...

Simon Kitururu 1:39 am  

@Candy1: Asante Candy1 kwa kutozinguliwa na yangu mawazo. Wapo watu KADHAA wanafikiri mie kichaa kwa niwazayo!:-)

Kuhusu Baby Face thing, sijawahi kuambiwa .:-(
Wewe ndio umenitoa bikira hiyo!:-)

Mie huwa naambiwa tu ''Kata nywele wewe kama unataka upate mchumba!'':-)

Mzee wa Taratibu 3:16 pm  

Naona Simon umkuwa na mawaso sana unafikiri nini haswa?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP