Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

IGA TU kama nia yako ni kuwa mtu YUNIKI ufanyaye YAKO kivyako!

>> Monday, September 14, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda kushoto zaidi ya kulia usipotafakari nijaribucho kuongelea katika hoja hii kwa kutumia sentensi hizi nyoko kimeegemea zaidi kulia!:-(]


Kwa kawaida vitu HAVIIGIKI na kama wewe ni baiskeli huwezigeuka TUKUTUKU kwa kuiga PIKIPIKI!:-(

Na kama wewe ni KHADIJA unataka kuiga ya SARA,...
......hata upatie kuiga utabakia tu KHADIJA ingawa UNAWEZA ukaanza kujulikana kama siku hizi WEWE ni Khadija awezaye kama Sara, na ni vizuri ukijua hilo ili ikusaidie kujua UISHIE WAPI KUIGA kabla ya kuacha kuiga kwa kuwa UNATAMBUA hata KARAFUU ITAKEJE KUIGA HILIKI itafanya ya HILIKI kikarafuu na haiwezigeuka HILIKI.


Unaweza ukatanua ujazo wa UYAJUAYO akilini kwa kuiga ya BUSARA,...
.... lakini kumbuka tu uigayo unayajazia kwenye MSINGI WAKO NA WA YAKO ULIOKUWEPO TAYARI na JUU YA YALE YAKO UYAJUAYO TAYARI kwa hiyo mchanganyiko wa ULIYOKUWA NAYO na ULIYOIGA bado si lazima yatageuza ASHKI zako zigeuke kuwa nyege kwa kuwa siku hizi unaiga nyege KWA kunyegeleshwa na kwa hilo unafikiri utapata nyege na sio kujizidishia tu ASHKI.:-(


Swali:
  • SI umestukia juhudi za mtoto kutaka kuiga wakubwa kutembea ndio humfanya atambae kwanza na sio kutembea na AKIJUA kutembea anaweza kujikuta anajua kutingisha tako zaidi huku akitembea kuliko wakubwa aliowaiga kutembea?

  • Ushagundua kwa kuiga kuimba kama Bob Marley unaweza ukajikuta uwimbaji wako unafananishwa na wa Peter Tosh na sio wa Bob Marley uliyekuwa unamuiga NA LABDA kamwe hautafananishwa na UIMBAJI wa MARIJANI RAJABU au Bi KIDUDE katika taarabu?


Nimeacha WAZO Mheshimiwa MWANAMBILIMBI!:-(
Kumbuka hili ni wazo tu KIJEBA Mheshimiwa au tu wewe KIGOLI Mheshimiwa na wala USITISHIKE!

Hebu basi BANTU abadilishe kwa kurudia tena ule wimbo wa Third WORD-Lagos JUMP




AU twende mtaani KONGO kukutana na watoto wa mtaani wakikuonyesha RAW TALENT MTAANI
katika -JUPITER's DANCE CLIP

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP