Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika KUVALISHA SUTI SAFI maneno wakati usemacho unahisi ni KICHAFU!

>> Friday, September 11, 2009

Ghafla mavi huanza kuitwa KINYESI,...

... na ukiyaita uharisho wewe KWA WAHESHIMIWA unajitafutia KESI.
Kijambo nacho hugeuka KUPUMUA,....
...na kama aliyetoa ushuzi NI MHESHIMIWA utaonekama huna heshima ukionyesha umestukia kwa kubana PUA.

''Shenzi wee !'' nayo hugeuka ''JAMANI WEWE VIPI !'',....
... na ukiwa na kiburi mpaka wa kurudia tusi ulilojifunza kutoka kwa mtoto wa jirani lenye nguvu zaidi ya NYOKO, waweza kufinywa kwanza kabla hujala mkong'oto na sahau ile ahadi ya kupewa PIPI.
Lakini mabingwa wakuvalisha SUTI SAFI MANENO ni wanasiasa,...
... kwa kuwa karibu hotuba na ahadi zao zote kwa wananchi ni matusi yafichayo neno na sentesi,...

.....''Nyie mafala kwa kunipigia kura kwa ahadi zangu za uongo!''....

......''Yaone vile PUA kama KIKWAPA,majinga , halafu masikiini wakati yatanifanyamie tajiriiii kilaini kama vile hawastukii niahidizo ni POROJO na kuwa mie najali yangu na familia yangu KIANASIASA!:-(


DUH!

Swali:
  • Kwani wewe huvalishi suti maneno hata wakati unaliacha limchumba ulilolichoka lakini hutaki kuliumiza roho?
  • Lakini unakumbuka kuwa unaweza kulivalisha chupi neno mpaka likashindwa kufikisha makali ya ujumbe uliotaka kuufikisha kwa neno?

NAACHA WAZO Mheshimiwa!

Ngojea Ndala Kasheba abadili kwa kutupa kitu -Yellow Card



Au tumkumbuke tu zaidi Maestro Ndala Kasheba kama aongeavyo mwenyewe ...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP