Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna uwezekano WEWE NI MHUNI!

>> Monday, September 14, 2009

Ndio!

Kunauwezekano kama unafikiri wewe sio MHUNI labda kweli wewe sio MHUNI!

Lakini kama huamini wewe ni mhuni wakati ni kweli weye ni mhuni haibadili ukweli kuwa WEWE NI MHUNI!:-(

Swali:
  • Kwani hujastukia hata WAHUNI sio sehemu zote wafanyacho hujulikana ni UHUNI?
  • Kwani hujastukia hakuna mhuni afanyaye uhuni masaa ishirini na nne ndani ya siku?
  • Kwani unauhakika na kwalifikesheni zisababishazo mhuni afuzu kuwa ni MHUNI zikusababishazo UWE NA UHAKIKA wewe sio MHUNI?

NI wazo tu MHESHIMIWA na labda naamini wewe WALA SIO MHUNI!

Ngojea ni muachie TITI kutoka Senegal aongelee-LOVE YOU




Au tu twende Mali, Salif Keita amuongelee-African Woman

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:17 pm  

Simon:-(

John Mwaipopo 6:57 pm  

zamani rafiki yangu mmoja aliniita mhuni. alipendelea kuniita hivyo. mpaka leo sijajua kwa nini aliniita mhuni. sijui ni kwa sababu ya nywele nyingi (afro)nilizokuwa nazo kipindi kile? sijui suruali zangu za kubana? sijui uswahilini nilikokuwa naishi? sijui ilikuwa na uchanya (u-+ve(upositive)au uhasi (u--ve(unegative)). ila umenikumbusha nitamuuliza kwani bado yupo.

Ninamaanisha nini maana ya uhuni?

Simon Kitururu 3:23 am  

@Yasinta: :-(

@Mkuu JOHN: Na kwa kiswahili chetu sikuhizi UHUNI unaweza kumaanisha kitu chochote kile!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP