Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TATIZO la KUDHANI kwa kuwa hukioni KITU basi HAKIPO na HAKIKUHUSU!

>> Thursday, September 17, 2009

Ukifumbia macho jambo,....
.... kwa staili hiyo BADO huliondoi JAMBO!:-(


Na ni UNAFIKI kujifanya unashtushwa HATA na kifo,...
.... kwa kuwa safari hii ni NDUGU au JAMAA umjuaye KAFA au kakumbwa na KIFO.


Na ni kukuza ujinga,...
.... kwa kutotaka kuelewa ya WAJINGA kwa kuwa unaamini YAKO NI YAKIEREVU na wewe sio MJINGA.


Na ukisubiri MPAKA ukabiliwe na tatizo ndio uelewe wenye matatizo,...
.... ni wewe mwenyewe ujiwekeaye kiporo cha mshituko na kuchanganyikiwa likikukumba hilo TATIZO.

Na kwa kuwa yasiyokuhusu unayafumbia macho,...
.... kumbuka tu kwa kawaida YASIYOKUHUSU kila siku yako macho na yanakukodolea MACHO!

Swali:
  • Hivi wewe ni miongoni mwa wamuonaye aliyevaa nguo wasahauo aliyevaa nguo chini ya nguo yuko uchi?
  • Unakumbuka kuingilia yasiyo kuhusu ni kawaida na tatizo huja tu UKIVUKA MPAKA na kujifanya ya mwingine yasiyokuhusu yana umuhimu kwako kuliko yanayemhusu?


NI HILO TU na NI WAZO TU MHESHIMIWA!

Tutaonana JUMATATU HAPA KIJIWENI kama sijafa na na nguvu na muda wa kublogu !:-(


Mpaka siku hiyo basi MI NAANZA kivyangu na nakutakia kila la KHERI KWA YAKO YAKUKUNAYO ROHO MKUBWA!

Au mpate MARIJANI RAJABU kwa hisani ya TIZEDBOY azungumzie-SALAMA



Au tu DULLY SYKES akumbushie-HUNIFAHAMU

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 12:32 pm  

Kweli Ujunga BUSARA. Maana nakumbuka jamaa aliyesema alikuwa anamuendesha mtu kwenye pikipiki kisha akamuuliza kama abiria anaogopa kama anavyoogopa mwendeshaji, abiria akasema HAPA. Kisha akamshauri kuwa afanye kama afanyavyo yeye ili na mwendeshaji asiogope. ETI AFUMBE MACHO!!! Mmmmmhhhhh. Akiendesha pikipiki huku kafumba macho si "hataoopa milele kwa kuwa hatafungua tena macho?"

Ama ya mlevi wangu alibanwa na mkojo mchana na kwa kuwa alikuwa barabarani akawafanya wasimuone kwa kufumba macho na kuchomoa "mdudu" na kukojoa. Mmhhhhhhh

Labda swali hapa ni kuwa tunaona aibu na kufedheheka tukionwa ama tukiona tumeonwa??? Kwani ukichunguliwa bila kujijua utakasirika ama kufedheheka? Ila ukiambiwa umechunguliwa (hata kama utakuwa unadanganywa) utajisikia mnyonge. Sometimes it works right??
Naacha, nishaletewa panga lililoenda kunolewa. Bado nipo hapa shamba. Wacha niendeleze kilimo

Fadhy Mtanga 5:18 pm  

Mtakatifu Simon upo juu. Na Jumatatu Mungu atajalia tukutane ili libeneke litambae mbele.
Mube kaka, lima sana, vuna sana, pika sana ili kwenye kula tuwe wote.
Pamoja kama kawa, usichoke.

Yasinta Ngonyani 8:41 pm  

nimenukuu "Tutaonana JUMATATU HAPA KIJIWENI kama sijafa na na nguvu na muda wa kublogu !:-("Mwisho wa kunukuu. kaziiii kwelikweliiiii!!!!

Faith S Hilary 10:42 pm  

Have a nice weekend MSHABIKI mwenzangu! Na mawazo nimeyapata...naendelea kufikiria..lol

Unknown 10:08 am  

Ambiere, Kitururu,
naendelea kuelimika na falsafa yako mzee......

Koero Mkundi 3:04 pm  

kama kawaida, nimepita kwa kaka kukemewa mapepo......lol

Anonymous 7:12 am  

Mkuu Simon Habari za siku.
Usemayo yaendana na ukweli na pia usemayo yatokea.

Rasta hapa.

Anonymous 8:23 am  

Karibu katika nyahbingi worriors.
http://nyahbingiworriors.blogspot.com/

nyahbingi worrior. 5:33 pm  

kaka simon.
nyahbingi worrior anakusalimu.naomba unitembele nami.

Mwanasosholojia 7:13 pm  

Kaka Kitururu nikusomapo kila mara mawazo yangu hutururu...heko, unatiririsha kwa mirindimo ya kitururu pasipokuwa na msururu...teh!

Simon Kitururu 4:31 pm  

ASANTE KUBWA KULIKO WADAU WOTE kwa kutonitenga hapa Wakuu!

Na asante kwa yote mlionitonya hapa!
TUKO PAMOJA!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP