Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati UMPENDAYE kimapenzi anakuita RAFIKI TU na anapenda kukusimulia ya LIMTU JINGINE alipalo PENZI!

>> Thursday, September 03, 2009

Atakusimulia MPAKA ya wake MPENZI!
Na kwa kumpenda wavumilia ili utunze angalau wake URAFIKI,.....

....na kinafiki inabidi UCHEKELEE,...
...na kwa watazamao unaonekana UNACHEKELEA!:-(

Wakati unaagananaye unamkumbatia KIMAPENZI!
Na yeye kwa kukuaga juu ya mkumbatio eti anakupiga na busu adailo ni la tu KIRAFIKI,....
.....anakukonyeza PIA ili UCHEKELEE,...
... na kwa mtazamo wake UNACHEKELEA!:-(


Na unajikuta bila kupanga umekuwa mnafiki kwa kuficha PENZI!
Na ukimuona akiwa na wake mpenzi angekuangalia angejua wakati huo we we ni MNAFIKI na si RAFIKI,...
... ..na sasa inafikia vikuumizavyo moyo inabidi UVICHEKELEE,...
.... na vinakuliza mpaka roho wakati dunia nzima inadhani UNAVICHEKELEA!

KWA KUMUELEZA MPENZI UMEJIFIA yadaiwa utaharibu URAFIKI na sasa wafa na PENZI!
Na kama si mnafiki labda bado huo ufanyao sio URAFIKI,...

...na unajua ni ukichaa KURUHUSU vikulizavyo kukufanya UVICHEKELEE,...
.....Na BADO ni UNAFIKI kufanya wakulizao wadhani UNAWACHEKELEA!:-(

Kihitimisho ni kwamba labda umpendaye anakosa yote yako ya urafiki na ya PENZI
Wewe wabakia wajijua ni MNAFIKI na si RAFIKI,.....
....na NI UAMUZI WAKO na kama waona inalipa umia tu kama maumivu yanakufanya UCHEKELEE,....
..... ingawa labda UTAKAYE LAKE PENZI ukweli huo anaujua na kwa KUJIFANYA HAJUI ni staili YAKE tu yakukunyima huku akiwa bafuni kuisafisha ANACHEKELEA!:-(

Duh nimeacha na kumbuka hili NI WAZO TU NJOLINJO na wala sikuongelei wewe MHESHIMIWA!:-(

Swali:
  • Unauhakika urafiki ni nini?
  • Si inasemekana Urafiki ni aina la penzi tu?
  • Kwani hujawahi kusikia waliopendana kimapenzi wadumupo HATA katika ndoa kiwafanyacho wadumu ni mazoea na labda hata hawafanyi yaliowahi kuwapeleka mpaka migombani enzi zile hayo mapenzi?

Sawa mkuu ngojea tubadili hali ya hewa kwa kwenda tena South Africa kwa Vyonne Chaka Chaka aongelee-Stimela



Au tubaki tu hapa hapa South Africa Athur Mafokate arudie tena-Oyi Oyi

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 2:04 pm  

Hapo ujumbe uko wazi, ukipenda usipopendwa...... Labda kama wee ni J.I.N.G.A. ndio utapoteza muda wako :-(

Yasinta Ngonyani 4:05 pm  

Inaunakana ni ujumbe mkali sana:-(

Chacha Wambura 4:24 pm  

Chib, J.I.N.G.A. ni kifupi cha neno gani? nimesahau kidogo nokumbushe!!!

Naota kama nimetapeliwa vile na yule nilodhani ni wangu tuuu, kumbe kuna mwingine anamega tonge!!!

tupo pamoja

Simon Kitururu 9:25 am  

@Mkuu Chib:Si utani!
@Dada Yasinta:Kuna uwezekano hakuna ujumbe wowote!:-(
@Mkuu Chacha: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP