Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu VIFANYIKAVYO BAFUNI!

>> Friday, September 04, 2009

[Tahadhari:Wazo limepinda!:-(]

Kumbuka,....
..... watu huwa hawaendi msalani KUTIBU haja ndogo na kubwa TU,....
....ingawa vifanyikavyo huko bado tunaweza kuviita KUJISAIDIA.:-(



Kumbuka,...
....Usishangae watokao bafuni ukiwachunguza ukastukia hawajaosha ukionacho KITU,....
...watafiti watakwambia kuna WASIKIKAO wakicheka peke yao bafuni na mpaka watoao MILIO ya ajabu iliyozoeleka chooni ,BILA kuisahau na milio iliyozoeleka kusikiwa kukiwa na zaidi ya mtu mmoja WAKATI WA FARAGHA chumbani, na ndio yuko peke yake bafuni lakini usishangae, ANAJISAIDIA.


Kumbuka,...
...inasemekana siri nyingi AFAZONAZO MAREHEMU aliyekuwa ni mke au mme wa MTU,...
... zilikuwa ni siri mpaka kwa ndugu ,jamaa, mpenzi hawala na kimada. Na hata kama kuna chumba KIJUACHO SIRI ZA WATU ZAIDI ndani ya NYUMBA ,afadhali choo hujua karibu sawa na bafu. Na hapa HATA tukiruka siri ya mheshimiwa ya kulamba makamasi kwa siri , INASEMEKANA SIRI nyingi binafsi hufanyika, sitaki kurudia kulitaja BAFU bali angalau kumbuka SI wakati ule mtu kakuaga au katangazia UMATI anakwenda KUJISAIDIA.



DUH!

Swali:
  • Unabisha?

NIMEACHA wazo NJONJOLINJO Mheshimiwa na USITISHIKE NI WAZO TU!!:-(

Hebu twende Italy waziri mkuu Silvio Belusconi ambaye ndio tajiri kuliko wote ITALIA aonyeshe bado Kahawa kwa kamasi RUKSA!....


Au tu twende Tanzania BI KIDUDE &Culture Musical Club waongee kitu..



Au tu UB 40 nao waendelee kutuliza na kitu-Adella

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP