Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Simulizi za mpenda BONGO FLEVA ughaibuni!

>> Friday, September 11, 2009

[Tahadhari:simulizi hii inaweza ikawa ina maana chafu kama unamawazo machafu au haikuhusu kama hujawahi kuwa mbali na nyumbani!:-(]

Upweke U duniani
Kama kwenu si jirani
Kama hatudanganyani
Fleva iko nyumbani!


Wakati uko nyumbani
Labda hukutamani
Ilijaa kibabani
Na sasa haba jamani

Leo U ughaibuni
Jipu tamu watamani
Ubinywe na wanyumbani
Anogaye kinyumbani.

Ghafla ni ya nyumbani
Uko nayo kiwanjani
Jinome ka hayawani
Si uko mbali jamani?


Ghafla uko kunyumba
Waupata tu unyumba'
Umenogewa waimba
Wimbo huu wa nyumbani.


Pata pekechapekecha
Au hata na chakacha
Na tena usiku kucha
Katika pata fleva

Pata tu BONGO FLEVA
Adamu ipate Eva
Kama tunda limeiva
Kula mwanawane kula!

Muziki wetu nyumbani
AU mtu wa nyumbani
Ukiwa navyo chumbani
Ni tamu ughaibuni.

Lakini tu kama uko ughaibuni:

Muziki bongo fleva
Magimbi bongo fleva
Mchumba bongo fleva
Bado tu hauko kwenu!:

Swali:
  • Ushastukia ukiwa ughaibuni kama wewe unapenda bongo fleva unaweza kuitamani hata bongo fleva mbaaaya?
  • Si unajua Wali ukizidi matamanio ya ugali yanakua?
DUH!
Samahani kwa kukupotezea muda KIJEBA kama umesoma huu UjingaBUSARA mpaka sentensi hii hasa kama hakikukuni nilichoongelea!



Hebu Saida Karoli atusaidie kwa kutupa hii bongo fleva iitwayo-Nkaba Ningya


AU tupumzishe na kubadili kwa kuangali matatizo ya kuzidiwa freetime kama aonyeshavyo CUBBY katika -Single Ladies

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:31 pm  

Simon asante kwa yote na hasa Sida karoli:-( kazi kwelikweli

Faith S Hilary 1:26 am  

Somehow hizo Bongo Fleva huwa sina mdadi nazo nikiwa huku...ila nikienda Bongo basi nyimbo za huku nasahau...its funny..

Hahahaha and this chubby boy!! Akaenda Tyra Banks Show...ningejua na mimi ningefanya...hahahaha

Simon Kitururu 3:21 am  

@Sister Ngonyani:Asante na wewe kama ni tusi!:-)
@Candy1: Uligundua lakini nikiongelea bongo fleva siongelei muziki?

Chubby boy always cracks me up!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP