Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUHUSU nywele nywele za MWILI!

>> Monday, September 07, 2009

Inasemekana VINYWELEO hata mpaka vya mwenye mchezo wakujinyonyoa,....
...pamoja na vingine shughuli yake ni mpaka kuwa MGAMBO WA PUA , kumbuka tu shughuli hasa ya KINYWELEO ni kutoa JASHO.


Na hata uvipige kalikiti vinyweleo katika staili ya kukwepa kuvinyoa,...
....au tu uachie LAVU GADENI iote rasta , wajipotezea muda kama juhudi zako zinakusahaulisha kuwa shughuli kuu ya vinyweleo si kupendezesha sehemu za siri , bali ni kutoa JASHO!

Na vinyweleo kama ni siasa ya nchi havina usawa, na kama mbishi vipime ukivinyoa,...
....na cha ajabu , WAWEZA GUNDUA vile virefu vikusababishiavyo UNUKE KIKWAPA , vile virefu vya chini kidogo ya kitovu viletavyo bughuza wakati hutumii eneo kukojoa, vile virefu vya wachache wenye kuota nywele mpaka kwenye chuchu na vile vifupi vya mgongoni au juu kidogo ya tako, havitofautiani KITU kama kipimo ni kuangalia ujazo wa vilivyochangia unuke JASHO.


Swali:
  • Unakumbuka kukumbuka urefu wa nywelenywele au ufupi wa nyweleo bado hauongezei nywele shughuli?


Ni hilo tu na NI WAZO TU MHESHIMIWA usitishike!
JUMATATU NJEMA KIJEBA au wewe SHUGA DADA!

Ngojea THE DRAMATICS waimbe wimbo wa Billy Paul umzungumziaye aonjaye mke wa mtu-ME and MRS JONES



Au tu CLUB FOR FIVE warudie kwa staili ya acapella wimbo wa Eurythmics-Sweet Dreams

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP