Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ndani ya UTAMADUNI wa kama NYUMBANI hapakaliki basi ngojea TUKAWACHEKEE MAJIRANI!

>> Sunday, September 27, 2009

Kuna watu wakuchekeao huku wameshikana mikono nje ya majumba yao,....
.....wakati wametoka kupigana roba, au tu KUPARUANA MAKUCHA huko kwao.

Kuchekelea majirani imekuwa tabia yao,...
....wakati nyumbani wakiongea Kiswahili wanasikilizana kwa lugha wasiyoielewa isiyo Kiyao.

Tatizo ni , kama hao ni mke na mume na wewe sio ndugu yao,...
....ukistukia kiendeleacho na kujiingiza kwenye yao, unaweza kujikuta WEYE sio tena rafiki yao.:-(

Kama tu ndugu kwa ndugu WAKIGOMBANA na ukiingilia yao,...
.... waweza kujikuta unachekesha ndugu wakipatana hata kwa sababu za kijinga LAKINI zilizo suluhisha yao.

Swali:
  • Unauhakika kuna ajuaye kwa uhakika wakati mwanana wa kuingilia ya wengine?
  • Unauhakika hutumii kuchekea watu ili tu kuzuia wasistukie una bomba la kibano?
  • Umemchekea jirani leo kisawasawa au umemkenulia tu meno?
  • Hujawahi kustukia angalau uwezo wa binadamu kujichekesha katika kubaraguza kuwa mambo shwari mgeni akija GHAFLA wakati watu wako katikati ya ugomvi?

Nasitisha wazo!


Turudi tena Reunion kupata haka kawimbo kutoka kwa Granmoun Lele kaitwako - Soleye


Au tu Kassav warudishe kitu -Zouk La Ce Sel Medicament Nou Ni (Live)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP