Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HISTORIA za mambo mengi zijulikanazo ni UONGO!:-(

>> Wednesday, September 02, 2009

[Tahadhari:Unaruhusiwa kunibishia!]


Kama wewe ni mchunguzaji wa tabia za watu utastukia karibu kila asimuliaye kitu,....
..... kuna uwezekano anaongezea CHUMVI STORI au anapunguza mpaka ujazo wa utamu wakitumbua . Kwa mfano stori yenyewe inaweza kuwa ilihitaji tu sentensi: ''KITUMBUA CHANGU UPANDE MMOJA kimeungua'' ,na anaweza akakusimuliwa MPAKA kuwa na mafuta yaliyotumika KUKIUNGUZIA kitumbua ni ya fisi. Na utakoma mwenyewe ukitaka akusimulie histori ya jinsi KITUMBUA kilivyogunduliwa kabla ya MAANDAZI!:-(

Na ukibadili mkao na kuwachunguza tena MTU KIBAO zikusimuliazo KITU,....
.... utazidi kugundua kuwa huwa mara KEDEKEDE wanakusimulia wapendavyo kuikumbuka stori na sio kama stori ILIVYOTOKEA kitu kisababishacho dunia kujaa HISTORIA MKWECHE!:-(


Haki ya njiwa tena!

Ukichunguza utastukia mpaka STORI ya KUMLA KUKU WA KIENYEJI hasa kama IMETOKEA asimuliaye ni MPENDA NYAMA YA BATA ,....
......STORI ambayo KIMILA inabidi IANZIE ...... alivyokimbizwa kuku VICHOCHORONI na hata alipokimbilia KIBANDANI ilivyobidi ndani ya kibanda ahangaike naye KABLA ya kumnyonyoa MANYOYA kuliko ruhusu JICHO lione vizuri UPAJA ULIVYO NONA kabla KIUMIO na kionjeo havija muhakikishia UPAJA ulivyo MTAMU,.....
.... kumbuka tu kama asimuliaye ni MPENDA NYAMA YA BATA , kama wewe NI MPENDA KUKU ,isikilize na fikiria mara mbili au zaidi kwa kuwa akusimuliaye stori hiyo kwa kuiita ya kuku anaweza akawa anakusimulia STORI YA KUMLA BATA ambaye kwake ni mtamu na ndio apendaye stori zake KUSIMULIA ingawa kwako huwa UNAANZA KUSIKIA KICHEFUCHEFU wala hata kabla hujaanza kufikiria maringo ya bata anavyotembea BILA VIATU na bila aibu anaenda msalani!:-([Samahani kwa kurefusha taralila:-(]


DUH!

Sipingi lakini umuhimu wa kujua HISTORIA ya vitu kwa kuwa inaweza kukurahisishia HATA kuelewa kwanini kwa WAHESHIMIWA WAKIAFRIKA au tu wadhaniwawo ni WAHESHIMIWA maeneo bado :

  • Wavaao BIKINI wasio na tako ni bomba na wavaa vibwaya pamoja na kuwa na bomba la tako la KISWAZI ni nishai!



  • Waafrika wakatao WEI kama lile la KAMBONA ni waheshimiwa na TUSIOCHANA Nywele na turasta TWETU ni nishai!

  • Keki na Mikate kwao bomba na Kula magimbi na viazi vitamu kwa chai NI nishai .

  • NA na nakadhalika kadhaa tatu na nusu unaweza ukajazia hapa...... na hapa......na...... ,au unaweza tu usijazie kitu kama unajisikia uvivu kidogo kama kawaida yako!:-(


KUMBUKA tu kuwa bado tunabishana kuhusu HATA histori ya MTU mpaka wajanja wanaweza kukulaani ukikana BINADAMU HAKUUMBWA na MUNGU hata kama WEWE huamini kuna MUNGU.

Na wengine wajanja watakusimulia historia ya mtu tokea alivyokuwa MJUSI mpaka alivyo geuka NYANI pale SERENGETI na kwa data ambazo sijazipata zote inasemekana MJUSI ALIPOFIKIA kuwa nyani hapo akagundua tendo la ndoa na kuzaliana mpaka akatoke MTU tena ni mitaa HIIHII ya Afrika Mashariki.

Tukiacha utani:

Na wasiwasi kama kweli MTU hakuumbwa na MUNGU kama HISTORIA fulani na tafiti za akina DARWIN zidaivyo na kutuhakikishia, basi Nyani wa kwanza kugeuka mtu kwa vyovyote VILE mchumba wake alikuwa bado ni NYANI.:-(

Swali:
  • Kama unaamini ya evolution basi si ni kweli yako Nyani aligeuka mtu?
  • Na kama unaamini uliumbwa na Mungu na wazazi wa kwanza wa binadamu ni Adam na Eva si maana yake unakubali lazima DADA alizaa na KAKA kipindi fulani wakati Nyumbani kwa Mzee Adam hakukua na jirani ?

  • Kwani usipojua historia ya JOGOO kuwa inaanzia kwa KUKU au YAI maana yake inachangia kukupunguzia utamu wa NYAMA YA KUKU/jogoo au inakukufanya uwe VEGETERIANI kisa hujui asili ya kifaranga?



Ni wazo tu PAPAA wa KUNESANESA na SISTA Mtanashati!
Labda kuna ukweli kwenye historia USINUNE BASI!:-(


Tupumzike Mtoto amwambie MAMA kitu katika-I don't like U Mommy


AU ngojea Artful DOdger ft Craig David warudie-Re Rewind


Au tu tubakie na Craig David katika kitu - Fill ME in

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 4:48 pm  

Ni sawa na mkorea au mchina aanze kukusimulia namna ya kumuandaa konokono kwa mlo safi, au aanze kusimulia utamu wa samaki faluda :-(

Faith S Hilary 7:33 pm  

Baba yangu anasema he doesnt believe na hiyo evolution thing coz kwanini hao nyani hawageuki kuwa binadamu...but that second point nikaona mmh...lol...maswali magumu haya! hahaha...

And I only like you when you give me cookies! I don't like you all the time. Hahahahhaha

And Craig David kashindwa kuja na BIG COMEBACK, ame-hit kidogo huku UK then kapotea zzzzzzzzz....he needs to come back BIG!

Simon Kitururu 8:49 pm  

@Mkuu CHIB : Si utani!

@Dada Candy1: SI utani haya maswali yanamzinguo fulani.

Huyo mtoto ananiacha hoi anavyomwambia mamayake very innocently: ''I love U but I don't like U all the time ''.:-)

Kweli Craig kapotea lakini music industry ni ngumu!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP