Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama kuna AAMINIYE kwa kuwa kimeandikwa KITABUNI!

>> Wednesday, September 23, 2009

Kilichoandikwa,....
....labda kimepitwa na wakati au kinahitaji tena kuhaririwa!:-(

Haki ya nani tena kama ni zamani kiliandikwa,...
... labda ukweli wake ulikuwa sahihi zamani na umuhimu wake LEO labda ni kama unataka TU kujua ya kitu historia.:-(

Na kumbuka tu kwa kawaida historia huwa inaandikwa,....
..... na walioshinda wakati inawekwa hiyo historia.


Na historia ya wanyonge hata ya AFRIKA iliyoandikwa,...
.... karibu yote haikuandikwa kwa mtazamo wa wanyonge hata hao Waafrika WALIOPEWA KIBANO ambao labda bado wanaugulia.:-(

Kumbuka ni vigumu kwa chochote kufikiriwa kuandikwa,...
....kama yamuhusuyo NA LABDA AYAJUAYE KWA UNDANI ananjaa na matatizo kibao mengine ya kufikiria.


Na labda kweli kuna umuhimu wayakale yaliyoandikwa,....
....lakini jihadhari na utafsirivyo YALIOANDIKWA ENZI ZA KALE ZA hata za JANA na kuyaoanisha na MCHEUO WA LEO ukugusao kama wewe kweli unamchezo wa kufikiria.:-(

Swali:
  • Hivi wewe huwa unatafsiri mwenyewe au unatafsiriwa?
  • Hivi uaminicho unauhakika si kwakuwa umekisoma kama sio umesomewa kilichoandikwa na waliowanukuu ambao walifikiria?
  • Hivi huwa unasimulia kwa juhudi historia yako ya kweli ya wakati unabwengwa AU TU KUPIGWA KONZI kama usimuliavyo ikiwa wewe ndio umebwenga mtu halafu ukamrukia kichwa kabla ya kumpiga ngwala na kumfyonza NYOOOOOO huku unamtemea mate?
Samahani ngojea nibadilishe nyoko na kulainisha aina ya maswali au TU kubadili aina ya cha kuuliza KATIKA swali :
  • Umevaaa chupi?
  • Si unakumbuka mara nyingi hata usipomjibu mtu swali KWA STAILI NA MKAO WA KUKAA KIMYA huwa LAKINI tayari unakuwa unajua jibu?


DUH!
NAACHA na ni wazo tu MKURUGENZI na wala USITISHIKE!

Hebu tubaki Ivory Coast tushuhudie Waafrika tujulikanacho nacho a.k.a kukata kiuno katika miondoko ya sindimba ya huko a.k.a MAPOUKA


Au tupoteze muelekeo na kwenda MIAMI kwa lengo lilelile la kufananisha ukataji kiuno kwa msaada wa PITBULL wakati anadai-I KNOW U WANT ME[calle ocho]

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP