Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda kuna ukweli hata KIRUKA NJIA mwenye sura mbaya JAMII humzidishia kazi kwa MALIPO kama ni ya nyanya basi ni za bei RAHISI!:-(

>> Thursday, September 24, 2009

[Tahadhari: Stori hii utafiti wake haukufanyika gizani na haujakamilika!:-(]

Lakini:

Jamii ikiamini unasura mbaya,...
... haikusamehi ujinga kirahisi KAMA WATOTO WAZURI hasa kama unasura kama kikwapa na mafanikio inaaminika hayajakuzingira.:-(


Na kwa kuwa KWENYE JAMII kuna waaminio kuna wenye sura mbaya,...
..... waaminio hivyo jihadhari nao kama una sura mbaya kwa kuwa hata wakiibiwa kwenye UMATI WA DALADALA wamuhisio kwanza NI MWIZI ni wahisiye ana sura mbaya ALIYEKUWEPO kwenye mazingira.:-(

Chakutisha ni kwamba huku mbaya,...
.... huko kwa wengine kwa uzuri kaumuka utafikiri kalishwa hamira.:-(



Na kwa wadhaniao wewe una sura mbaya,....
...wakistukia na hali yako kimafanikio NI mbaya , wengi wao wanahisi unazidi ubaya kwa kustukia hali yako na akugaiaye pendo katika hali hiyo basi udhaifu wake kwako hauko katika sura.


Chakusikitisha ni kwamba inasemekana makazini hasa kama ni mwanamke ndio mwenye sura mbaya,...
.... anaweza cheleweshwa kupandishwa cheo na ukilinganisha na bosi amfikiriaye ni KISURA na kirahisi KISURA MBAYA atalipwa mpaka MDOGO wa mshahara.:-(

Na yasemeka makazini vidume akina dada wawapendao sura SI KAA SIYE wenye sura mbaya,...
.... wao VIDUME WALIMBWENDE wakimshika hata tako mtu ni ruksa na watachekewa WAKATI siye wenzangu na mimi tutashitakiwa kwa SEKSHO HARASIMENTI na, na kukunyiwa na sura.:-(

WAZO LIMENISHINDA!:-(

Swali:
  • Kwani kuna ukweli wengi waaminikao kuwa wanamiakili sana huwa wana sura mbaya?
  • Si umestukia ukipenda mtu basi unamuona mzuuuriiiii?
  • Umestukia kama unamchukia mtu na bado KISIRI unastukia wake uzuri AKIKUCHEKEA kuna uwezekano akikutongoza hata ukimnyima majaribuni alishakuingiza na labda vigezo vya UCHOYO ni kuogopa dhambi au mashoga zako watasemaje wakistukia wajuaye unamchukia chachandu umemgaia?
  • Si unakumbuka akuonaye mbaya kuna wamuaonao mbaya na kama upendavyo ukipendavyo kuna watumiao nguvu kwa sababu hizo hizo zako kukichukia?
HAKI YA NANI TENA WAZO HILI LIMENISHINDA !
Lakini kumbuka ni WAZO TU Mheshimiwa !




Hebu twende Mexico kukutana na Instituto Mexicano del Sonido


AU tu tubakinao tu Mexico walete kitu -ALOCATEL

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP