Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kumbuka tu hata ufanyeje HUWEZI KUPENDWA NA KILA MTU!:-(

>> Tuesday, September 08, 2009

Kumbuka kuna wengi tu hawakuhusudu,...
.... ingawa ukiwapa mtihani wa kwa nini hawakupendi watapata ZIRO!

Na ukijaribu sana tukuhusudu,....
.....kuna watakaochukulia hiyo ndio sababu ya kukupa mapenzi yenye ujazo ZIRO.


Na kama wewe ni binadamu na sio jini na unamchezo wa baadhi ya watu kuwahusudu,....
..... basi inamaana hata wewe kunausio wahusudu na wawezashindwa kujibu maswali hata ya kwanini kuna uwapendao zaidi na ya kwa nini kuna uwachukiao pia , NA KWA HILO waweza pata maksi karibu na ZIRO!:-(


Lakini tukikuchimba labda kweli wewe haifai tukuhusudu,....
....kwa kuwa labda kweli wewe ni MBAYA hata kama una sura nzuri ,kwa kuwa LABDA ya siri uyafanyayo kwa chuki ni maksi mia KWA mia na kwa kuwa hatujastukia hilo , kwa hilo tupe tu maksi ZIRO.

Swali:
  • Unauhakika hujawahi kuchukia mtu kwa unayohisi tu ambayo kwa kawaida si ya kweli?
  • Unakumbuka binadamu wanapigana mpaka vita kwa hata chuki zisizo za msingi?
  • Kwani hujakutana na wakuchukiao tu hata kwa jina kwa kuwa tayari hilo jina labda LINAASHIRIA WEWE ni mpagani na mhusika kwa zake zisizo na sababu kaamua anapenda wakristo?
  • Unajua unaweza kukosa demu sehemu kisa unajina la kikristo?


NIMEACHA na nakutakia JUMATISA na nusu NJEMA!


Ngojea twende tena Haiti ,T vice aongelee-Pou Jam Vle


Au tu ngojea JEAN-PHILIPPE MARTHELY alete kitu- Bèl kréati

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:05 am  

Ulijuwaje yote hayo? U must be genius!

Simon Kitururu 10:37 am  

@Papaa Fadhy: Haya si tunaishi nayo tu kila siku mtaani Mkuu?

chib 10:38 am  

Pia ukumbuke hata yule anayechukiwa na wengi, bado anao wanaompenda!

Simon Kitururu 10:47 am  

@Mkuu CHIB: Kweli kabisa maana hata HITLER alikuwa na GIRLFRIEND!

Mzee wa Changamoto 1:12 pm  

Baelezeee Papa Mkodo

Yasinta Ngonyani 5:10 pm  

Kumpenda au kuchukia si sawa tu:-)

Faith S Hilary 7:55 pm  

This is ukweli no doubt at all

Simon Kitururu 11:18 am  

@Mubelwa+Yasinta+Candy1: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP