Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nafasi ya ALIYEKUPA KIDUDE KWA HURUMA akishakupa kidude KWA HURUMA!

>> Wednesday, September 16, 2009

Kama umeshapewa kidude,...

..... wewe ni bingwa kwa wasionacho KIDUDE wakihitajio NA ni kweli unacho KIDUDE hata kama aliyekupa ALIKUGAIA kidude kwa kukuonea HURUMA!

PAMOJA NA YOTE; aliyekupa kidude,...
... kumbuka ALIKUGAIA SI KWA KUWA TU ANAHURUMA, bali kwa kuwa KWANZA alikuwanacho kidude au alikuwa na uwezo wa kukupa kidude na labda ALIKUWA NA UWEZO WA KUKUGAIA hata BILA kukuonea HURUMA.:-(

Na kama unabisha , kumbuka tu HILI ; hata ufanyeje ,KAMA HUNA kidude na huwezi kumsawazishia mtu atakaye kidude angalau apewe na mtu mwingine kidude,...
...HAZIMTIBU KITU MTU ZAKO HURUMA kama matibabu ya mtu ya MKUNO yanahitaji tu kidude na SI HURUMA , hata kama ni kweli unamuonea HURUMA.

Kumbuka pia hata umjuaye KWA UZOEFU huwa ukitia huruma anakugawia kidude,...
....kumbuka kuna awanyimao BILA SABABU MAALUMU hata watieje HURUMA.:-(

Na kama unamchezo wa KUONA HURUMA KIRAHISI na una kidude,...
..... kumbuka DUNIANI kuna watongozaji wasiostahili ZAKO HURUMA ambao STAILI ZAO TU ZAKUOMBEA KIDUDE ni kutia HURUMA!:-(

Halafu kumbuka kuwa kama hupendi kuonewa huruma na WEWE NI MPENDA kula ulichokitolea jasho MWENYEWE kidude,...
....ukihisi umeonjeshwa kidude kwa KUONEWA HURUMA daima kidude hicho hakitanoga kwa LADHA FULU YA UONJO kwa kuwa wakati UNAKIGIDA KIDUDE kuna kitu kitakuwa kinaondoa au kupunguza FULU MRIDHIKO kwa kukukumbusha unagida tu UGIDACHO KIDUDE kwa kuwa TU umeonewa HURUMA.:-(


Na kama wewe ndio ugawaye kidude,...
.... kumbuka kama ushakigawa kidude na kimeliwa, huruma zako zimeshafanya kazi yake na hata ufanyeje makali ya mgao huo yalishapita KILELE CHAKE na kidude CHAKO NDIO kimeshaliwa hivyo TENA , hata kama SASA HIVI uliyemgaia kidude UMESTUKIA HAKUSTAHILI KUGEWA KWA HURUMA na humuonei tena HURUMA.:-(



Swali:
  • Ujastukia kuwa ni rahisi kuingia unyonge kwa aliyewahi kukusaidia kwa kukuonea huruma?
  • Unafikiri Rais wa Tanzania katika ziara zake ughaibuni za kutia huruma ili Tanzania igawiwe kidude mwaka huu, haingii unyonge mbele ya aliyegawia mwaka jana Tanzania kwa huruma kidude, kwa kuwa tu anakumbuka na mwaka jana alihurumiwa tu alichopewa kidude?
  • Kwani unataka kudai hujawahi kustukia kuna ulichonacho kidude ambacho unacho kwa kuwa aliyekugaia alikuwa anakuonea tu huruma?
  • Unajua mazingira yakijiweka sawa kukuvumbulia unahitaji kidude ,inawezekana ni wewe utakayeshinda kwa kutia huruma ili upewe KIDUDE?


Samahani NALIKATIZIA wazo hili nyoko HAPA Mheshimiwa!:-(

KUMBUKA lakini HILI NI MOJA TU YA mtazamo katika WAZO tu MHESHIMIWA Kishtobe au weye MHESHIMIWA Bitozi !
Na KAMA HULIELEWI HILI WAZO wala USITISHIKE Mheshimiwa!



Ngojea Milli Vanilli watupeleke zamani kiduchu katika-GIRL, I am gonna miss U


Au ngojea LL Cool J aibakize hukohuko zamani katika-Phenomenon

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 3:56 pm  

Kidude kama unakipata kwa kuonewa huruma hata ladha ya muonjo wake inakuwa ya kihuruma huruma.

Yasinta Ngonyani 4:33 pm  

Simon:-(
Fadhy nawe:-(

chib 5:22 pm  

:-o!!

Simon Kitururu 12:11 pm  

@Wote: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP