Mtu mwenye Kifafa akijamba.........
>> Friday, March 23, 2007
Kuna baadhi ya hoja hupenda kuzirudia . Hasa kutokana na baadhi ya washikaji kuniuliza maswala na pili kutokana na yanitokeayo katika maisha haya magumu ya kila siku.Moja ni hili nalo andika hapa......lakini kabla sijaanza kuandika......
Watu hupenda kupata majibu au maelezo ya karibu kila kitu kiwagusacho. Lakini kama jibu halipo hupenda kubunia maelezo ambayo huchukuliwa kama ni ukweli.
Jibu ambalo watu wanashindwa kulibishia vizuri hugeuka kuwa ndio ukweli.
Inabidi tukubali tu kuwa si kila kitu kiko kama tufikiriavyo. Mara nyingine hisia za kawaida(common sense) hudanganya hasa kama malengo ni ya mbali. Na sababu kubwa ya kudanganyika na matumizi ya hisia hizi (common sense) ni ukweli kuwa ujenzi wa hii kitu unahitaji uzoefu ambao hakuna mtu anaweza kuupata katika kila kitu katika maisha haya mafupi ya binadamu.Kila mtu kunasemu tu hataweza kuijua na hisia zake zawezakuwa potofu.Hivyo kila mtu kwa kutumia hisia za kawaida huweza kujikuta kajilenga pabaya.Lakini kutokana na kwamba binadamu tofauti wananguvu za hoja tofauti , basi kuna baadhi yetu tunaweza kuwa tunaweka mapotofu yetu ya hisia za kawaida yachukuliwe na wengi kama ndio ukweli halisi.Na dunia imejaa mambo haya. Na nahisi wengi wetu tunadhurika na hisia hizi ambazo zimegeuka kuwa ndio ukweli.
Utasikia kuwa eti binadamu walikuwa wanajenga mnara kwenda mbinguni ndio Mungu akaamua kuwachanganya kwa kuwafanya wasielewane ndipo lugha nyingi zikatokea. Swala hili kwa taaluma za leo utagundua kuwa ilikuwa haiwezekani kujenga mnara wa babeli kwenda mbinguni. Lakini bado maelezo ya vyanzo vya lugha utasikia baadhi ya watu waki zungumzia hili kama moja ya sababu ya kuwa na lugha nyingi duniani.
Hivi mbinguni ni wapi?
Utasikia.....
- Kinjekitile alidai anaweza kubadili risasi kuwa maji.
- Utasikia kuna watu wanadai kuwa zeruzeru hapigiki picha.
- Kunawakati nishasikia watu wakisema wanawake wa kizungu hawadanganyi.
- Nishasikia kuwa eti Tanzania masikini.......na kwamba Watanzania tunaamini hatuwezi kujikwamua.
- Nakadhalika kadhaa
Nakumbuka wakati niko shule ya msingi , darasani tulikuwa na mshikaji anayeanguka kifafa. Basi ilikuwa akianguka watu tunakimbia kama vile sijui nini kimetokea. Sababu kubwa ya kukimbia huku ilikuwa kwamba tumeambiwa kuwa jamaa wakati kaanguka akijamba basi wote tutapata kifafa. Matokeo yake ilikuwa tunaumia kwakukimbia na jamaa anajing'ata ulimi kutokana na watu kukwepa kumsaidia asijing'ate wakati ameanguka.Ilichukua muda mrefu kujua kuwa hakukua na ukweli katika jambo hili.
Lakini inabidi nikubali kuwa katika mambo mengi ambayo hukutananayo na kujaribu kuyaelewa yanayoniacha hoi moja wapo ni hili la wabunifu wa maelezo ya mambo. Mambo mengi tu duniani tusiyoyaelewa kuna jamaa ambaye alifanikiwa kuelezea watu ni nini kinaendelea hata kama sababu hizo amezibuni tu.Na si watu binafsi tu .Mpaka nchi , makanisa , misikiti, masinagogi nk yameshiriki sana kutuletea tafsiri na maelezo ambayo kila siku yanazidi kugundulika kuwa mizizi ya ukweli wake inautata.Unakumbuka kuwa kanisa lilishawahi kung'ang'ania kuwa dunia iko kama meza?Na aliyebisha aliuawa. Unakumbuka Afrika Kusini kwa msaada wa kanisa walishapitisha kuwa waafrika si watu kamili?
Duh!
Ngojea turudi katika mambo ambayo hata hatuyafikirii. Mimi naamini hizi hisia za kawaida(common sense) zinatufunga mimi na wewe sasa hivi navyoongea. Kuna mambo hatuyastukii kutokana na kutumia common sense. Hizi hisia za kawaida zinatupa majibu kuwa haiwezekani. Zinatupa sababu kwanini haiwezekani- kwasababu fulani na fulani walifanya hivyo halafu haikuwezekana. Lakini kila mtu atakubaliana na mimi kuwa , kila mtu anabahati yake na kila mtu anastaili yake. Halafu wote sisi ni binadamu , hivyo hakuna mwenye ukweli asilimia mia.Kumbuka kila siku ni siku nyingine. Hiki kitu mimi nakiamini sana. Na naamini kuwa kila mtu ananafasi ya kufanikiwa.Si lazima kama jirani kaanzisha kioski anauza ndala basi wote tuanzishe kioski na kuuza ndala, lakini tukiwa wabunifu na kujiamini katika yale tuhisiyo kuwa tunauwezo nayo nadhani tunanafasi ya kufanikiwa.Sisemi kuwa ni rahisi! Hawa jamaa wa Google walipoanzisha kampuni wafanya biashara wengi wakubwa walisema kuwa haiwezekani kutengeneza pesa kwa staili yao. Sasa hivi kila mmoja kakaa kimya. Nilikuwa namsoma huyu jamaa Tyler Perry.Yeye sasahivi amefanikiwa sana kwa kuamua kuwalenga wanawake weusi Marekani.Alipoanza akiwa kama mbeba maboksi na mfagiaji na mkusanya kodi.Watu walimpuuzia. Sasa hivi wakati tayazi ana milioni mia moja mfukoni, wapo wamsemao kuwa maswala yake ni ya kijinga lakini anasoko lake. Siongelei maswala ya pesa tu. Naamini kufanikiwa kivyovyote. Hata kama unataka kujiua naamini unaweza kujiua kwa mafanikio . Labda bila maumivu sana au kusumbua watu .Fikiria tu kidogo.
Duh!Ngojea basi tujichakalishe maana itageuka kuwa stori tu. Tuulizane baadaye maswala vipi basi!
Lakini.......
Wanasayansi, mimi hupenda michezo yao, kwani huwa wanamchezo wa kuhakikisha maswala yaendavyo. Lakini pia hata wao majibu hawajapata yote. Sisemi kuwa ukijua mwenzako alishika moto akaungua ni lazima na wewe ushike moto. Lakini kumbuka si ukweli mwenye kifafa akijamba atakuambukiza kifafa.
Ngoja nimuache Vanessa Paradis
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment