Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Binadamu na matumizi yake ya Mungu!

>> Thursday, June 04, 2009

Tukiachana na swala la MUNGU wanani ni sahihi,....
......kwa mwenye udhaifu wa kibinadamu kuna SIKU au KITU utakwama na litokeapo hilo nikikusimulia hata ya kuhusu Mungu wa Kimandengereko anavyosaidia unaweza kuchukua muda kunisikiliza wakati kwa kawaida ulikuwa unamjali na kumuabudu Mungu wa Kihindu.

Na usipoangalia,....
..... labda kuna mambo unakosea mwenyewe halafu UNAMSINGIZIA MWENYEZI!


UKITAKAKUJUA ni kwanini Mungu ni muhimu,...
....fikiria jinsi ilivyorahisi hasa BINADAMU akikwama apatavyofaraja hata kwa kudai HATA KIBANO ni mipango ya MWENYEZI MUNGU!


Binadamu wengi wakati wanajisikia kufakufa ghafla na imani inakua.

Jinsi kibano cha udhaifu wa KIBINADAMU ulivyomkali,...
.....kuna ambao mpaka wanaokoka au kustukia imani za kuabudu Mbuyu hata kwa KIBANO cha KUCHACHA.

Ukweli ni kwamba,....
.....KWA ASILIMIA kubwa ya BINADAMU, ni FARAJA wapatazo kwa kuamini kitu chenye uwezo na NGUVU kuliko wote kinakutunza na KUKULINDA.

Swali:

  • Unakumbuka enzi zako za utoto za kufikiria Baba Yako anaweza yote na haanguki?
  • Unakumbuka filingi ya kuzidiwa nguvu hata wakati jamaulilofikiri unalizidi nguvu halafu ghafla ukastukia linakubwenga kisawasawa kisha ukamstukia mtu mtetezi anakuja ?


Kwa imani inasemekana yote yanawezekana,...
.....lakini kama weye mchunguzi utastukia asilimia kubwa ya waombewao dua hata kama ni za ugonjwa huwa hawaponi.:-(


Kikubwa ni FARAJA uipatayo!

Unaweza kubisha ,...
.....lakini asilimia kubwa ya waombao Mungu , MUNGU wao huwa hawajibu na ni imani tu inayoendelea kuwafanya wasikufuru kwa faraja kuwa kuna sababu ajuazo MUNGU wao kwanini umeomba weee halafu mpaka leo HUJAPATA na wapatao ni wezi na baadhi uliwapigia kura.

Na aaminiye hata ajuapo anakufa kinachoweza kumfanya afe kwa amani ni kwamba anafaraja tu.

Na wamuombeao mtu hata yule mgonjwa asipopona muhimu kwao ni FARAJA kuwa anaenda Mbinguni au kwa waaminio dini fulanifulani labda hufarijika kuwa anarudi Kigoma na mzimu wake utaendelea kuwalinda.

Swali:
  • AU?

JIANDAE kinamna kivyako na Mungu wako kwa kuwa Mungu usiyemuamini unaweza usiwe na uhakika naye mpaka dakika za mwisho na utakacho kosa ni kupoza roho ya na kuanza huku huna FARAJA!

Swali:

  • AU?


Naacha na kumbuka hili ni moja ya wazo tu USITISHIKE!

Lakini kama umekwazika niombee au tubu kivywako kama katika imani yako ukitubu maswala ya PARADISO yatakuwa MSWANO!


DUH!

Ngojea tupumzike kwa kuangalia talanta za Mwenyezi....


Au tu ngojea tutulie na King Boogaloo Tut -Smooth poppin'..

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP