Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAFISADI wa CHANGU changu na CHAKO changu!

>> Thursday, June 25, 2009

Ukiwaangalia WANASIASA-mafisadi,...
... utastukia wanadhani CHAKO CHAO,....

..... KAMA HUJASTUKIA tayari KWENU wanadai ni KWAO.

Afadhali na MALAYA-mafisadi wa NGONO,.....
.....ambao CHAKO hukitakakiwe CHAO,....
....na ukiishiwa nakukistukia CHAKO ndio waweza kustukia hawakukuacha mtupu na kwa UKARIMU walikuachia angalau GONJWA LAO.


MAFISADI wa UNDUGU,....
.... ukifanikiwa wewe ndugu YAO,....
.... ila ngojea UCHACHE ndio ustukie wao si ndugu kwa KUSIKIA wadaivyo hawakujui na matatizo YAKO si YAO.



Na wale MAFISADI wa URAFIKI,...
....CHAO ni CHAO na CHAKO ni CHAO,.....
.... na unaweza usistukie mpaka usiwe na CHAKO.:-(


Swali:
  • Lakini kwanini ujilimbikizie CHAKO kwa kuwa ni CHAKO KIDUDE ili iwe nini kama HUKITUMII kidude?

  • Unakumbuka ukifa hata uwe na chupi ngapi labda ni moja tu utazikwa nayo halafu makorokocho yako yote mengine utayaacha?




NAACHA wazo!

Ngojea AEROSMITH wadai..-I don't wanna miss a thing

Au tu ALAINE abadili bila kubadili hali ya hewa...-Make me WEAK

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP