Wakati TUPO tusubiriao MELI kwenye uwanja wa NDEGE!
>> Tuesday, February 28, 2012
Ndio,..
... kuna tuyasubiriayo KUSIKO,...
.....halafu tunashangaa TUYASUBIRIAYO yasipojitokeza huku tukijishaua kuwa tumeyahangaikia.
Swali:
- Na si kama umsubiriaye anakuja na basi la ARUSHA hata umsubiri vipi kwenye basi la MTWARA yawezekana ni kujipotezea tu MUDA?
- Na kama utumiacho ni unga wa MAHINDI labda basi si usitegemee upikacho kitageuka UBWABWA?
Ndio,...
.... LABDA maishani,....
.... wengi ya NDEGE hatuyasubirii uwanja wa ndege,...
.... na ingawa tunayahangaikia ila bado mahangaiko yetu tunakosea pakuyalenga na bila kustukia tunasubiria ya NDEGE bandarini na ya MELI kule uwanja wa NDEGE na hapo ni kama kabisaa sio kwenye kituo cha daladala MOROGORO ambako hata BANDARI hakuna!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Hugo Nyame arudie - Pardon Madame
Au tu Majoie Ayi azime kwa - Aicha
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh! sijui hao akina dada hawana mifupo?
Hizo kweli ni sawa na ndoto za Alinacha, anawaza kumuoa binti mfalme, baada ya kutajirika kutokana na kuuza vito kidogo vya gilas, au kutokana na kuuza genge....ni sawa na wale wanadai bahari wakati wapo bara ndani ndani kabisa....
Post a Comment