Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

FASHENI ZA MAKABURI!

>> Thursday, March 13, 2008

Kuongelea kifo ni mwiko kwa watu lukuki.
Kuongelea makaburi kwa wengine ni swala la nuksi.
Kupita makaburini , kwa wengine ni kwa mwendo wa kama umebanwa uharisho.

Sasaaaa....


DUH!

Nahisi umestukia nafikiria sana mambo ya kifo!
Samahani!

Lakini tuendeleee........

Swala la kuchagua uzikwe wapi limenikuna kidogo tena baada ya kukutana na namba zisemazo:

  • Asilimia 50 ya Waingereza wanataka wachomwe na majivu kutupwa maeneo baada ya kufa.
  • Asili mia 40 ya Wamarekani (USA) wanataka wachomwe na majivu kutupwa vilevile.

Lakini....

Kilichonizingua zaidi ni huu mradi wa PIRAMIDI MPYA , ambao na wewe unaweza kushiriki kujiandaa kuzikwa kwenye PIRAMIDI lililoko katika hatua za kuanza kujengwa.

Kama unataka kuzikwa kwenye piramidi hili, BBC inaripoti kuwa bei ya jiwe ni EURO 700 kwa bei ya sasa.











DUH!

Sasaaa......

Swali:
  • Hivi makaburi umuhimu wake haswa ni nini?

Naamini kuna wengi ambao hutembelea makaburi ili kuendelea kuungana na wapendwa waliotutoka .

Wengi hutembelea makaburi ilikujiliwaza, kutoa heshima na hata kuendeleza uhusiano na wapendwa waliotutoka.

Kwa kweli kuna sababu nyingi sana zilizomfanya binadamu fulani aamue kuwe na kaburi likumbukwalo .


Lakini......

Kuna mtu kaniambia kuwa, kutokana na technolijia, watu wana video, picha na njia nyingi tu juu ya kumbukumbu walizonazo mukichwa ambazo zinaondoa umuhimu wa mtu kuwa na kaburi.

Swali:
  • Je kumbukumbu mukichwa ya waliotutangulia +video+picha=hatuitaji kuzika tena?
  • Unaogopa kufa eeh?
  • Unakumbuka enzi fulani za kale , ilikuwa mtu akifa wanamkimbia na kuhamia pengine?




SAMAHANI!
HABARI ZA KIFO SI ZA UTANI!



DUH!

MUNGU awapumzishe na kuwapa raha wale wote waliotutangulia mahali pema peponi!


Ngoja nikutoe katika habari hii ya makaburi kwa kukusikilizisha huyu mwana mama kutoka MALI aitwaye Oumou Sangare



SIKU NJEMA!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDWIN NDAKI (EDO) 10:59 pm  

Binafsi hiyo ya kuchomana bado haijakaa vema kwangu.

Hao sasa naona wanataka kuziba rizki zetu wengine,maana vilio bongo vinasaidia kubana matumizi ya msosi...aaa aaaaa

Ngoja nikunje ndita sasa nitoe mawazo yangu.

Waafrika lazima tukubali kuendelea kushikiria vilivyo vyetu ikiwemo mila na desturi.

Kuzikana ni moja wapo ya desturi zetu.Sasa haya mambo ya kufanyana jivu,nafikiri pia wenzetu hawana ardhi yakutosha inaweza kuwa moja ya sababu.

Sisi tuna misitu na nyika bado zipo ..plain chips..yaani miti bila wajenzi.

kwa leo inaosha..wacha niwahi luoka kwanza..


chwaaaap

Simon Kitururu 3:15 am  

Nakubali kabisa kuzikana ni moja za desturi zetu. Umenichekesha ulivyosema;`vilio bongo vinasaidia kubana matumizi ya msosi...aaa aaaaa
´:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP