NANI KAKUAMBIA KILA MTU ANAKWENDA BAA KWA FURAHA?
>> Thursday, March 27, 2008
Asili ya uelewaji wako kitu, unaweza kujengwa na uzoefu ua ukosefu wa uzoefu wako katika jambo .
Tatizo liwakumbalo binadamu wawili tofauti katika uelewaji wa jambo moja, ni jinsi binadamu hawa wawili wanavyoweza kuwa wamejengeka tofauti kutokana na makuzi tofauti , mazingira tofauti au kutokana na ukweli kuwa hawa binadamu wawili ni tofauti.
Swali:
- Ushawahi kuelewa ni kwanini binadamu wengine wengi(hasa wazungu), wanaongea na mbwa au paka wao kama wanaongea na mtu?
- Unakumbuka wenye majonzi na wenye furaha unaweza kuwakuta msikitini au kanisani wakipata na kuwakilisha mahitaji yao ya kidini tofauti kwa pamoja mbele ya Mwenyezi Mungu?
Maeneo, utawasikia watu kibao ambao wamejipa UTAALAMU WA KWANINI.
Taaluma hii ya kujipa ndio huamua mambo kibao kuhusu kwanini watu wengine wanaonekana au wanafanya hiki na kile.
- Ni rahisi kufikiri kila uonacho kuhusu mtu fulani ni lazima ukielewe.
- Ni rahisi kufikiri kuwa umekielewa uonacho.
Ngojea ni kupe kastori:
---------Hadithi! Hadithi!-----------
Hapo zamani za kale , wakati bado niko mdogo, mitaa ya Songea, nilikuwa nakatazwa kucheza mpira na unifomu za shule kutokana na udongo mwekundu wa Songea na sababu nyingine kadhaa. Nilikuwa nakatazwa kupitiliza saa kumi na mbili jioni michezoni hasa kutokana na wazazi kutaka kuhakikisha najisomea na kumalizia zile Home Work.
Niliyekuwa namuogopa sana kushikwa naye nikivunja sheria alikuwa ni Baba yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa inatokea mara kwa mara anayenidaka nacheza mpira au nimepitiliza muda ambao natakiwa kuwa nyumbani alikuwa Baba.
Mdingi alichokuwa anafanya kilikuwa kinawashangaza marafiki zangu! Alikuwa anaweza kuja kujiunga katika kushangilia au analeta stori na marafiki zangu na hata pipi anaweza akatununulia.
Kitu ambacho marafiki zangu walikuwa hawajui ni jinsi mimi jasho linavyonitoka, kwa maana pamoja na Mdingi kucheka nasi, ninlikuwa najua ni kibano gani nitapata pale tu nitakapofika nyumbani. Kwa sababu ilikuwa napata kibano cha kuotea mbali.
Lakini....
...Kesho yake nikikutana na marafiki zangu , hawakawii kusifia jinsi gani nilivyokuwa na Baba poa, kutokana na wao kutojua jinsi gani nilipata kibano pale nilipofika nyumbani baada ya kuachana nao.
-------Mwisho wa Hadithi-------
Dhumuni ya hadithi hii ni kutaka kumkumbusha jamaa huyu na yule kuwa , unaweza ukawaunaona kisehemu tu cha sura nzima ya kitu kama utakuwa unajenga hoja kutokana na kumuona mwanadada yule kavaa kimini na yuko uchochoroni. Anaweza akawa kakimbia kibano ndani kwao na hayuko uchochoroni kuuza nanihiii.
Swali:
- Unafikiri mtu akiwa na ze bia au ze gongo mbele yake , maana yake anafurahia maisha?
- Ushawahi kujisikia vizuri baada ya kulia?
- Ushawahi kulia kwa furaha?
Kuna watu wanafuraha nyumbani.
Lakini kuna watu wako mbali na furaha za nyumbani.
Kuna watu nyumbani ni sehemu ya kujilaza tayari kwa maumivu ya kesho.
SIKU NJEMA!
Pumzika na..Basement Jaxx wakikuambia DO YOUR THING
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment