Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUHUSU MATUMIZI YA KIKOJOLEO!

>> Monday, March 10, 2008

Matumizi ya kitu fulani , yako mengi ingawa vitu fulani vinapewa jina kutokana na kitu fulani , kitu ambacho kinaweza kuondoa umuhimu wa matumizi fulani ya sehemu fulani.

SWALI:

  • Unakumbuka matumizi mengine ya takataka yanaweza kupewa jina mbolea, na kwa mmea mbolea ni pilau?
Haja ndogo ni kubwa kama umebanwa na haja ndogo.
Kitu kiletao umuhimu wa shughuli iitwayo haja ndogo, ni haja kubwa ya uhitaji wako wakwenda haja ndogo katika wasaa nyeti usababisha haja ndogo kuwa ni kitu kikubwa maishani mwako katika dakika zile ambazo umebanwa.

Kama unakiu , unahitaji maji na sio pilau ingawa mbele yako kuna ubwabwa.

DUH!

Ukishiba, pilau/Ugali wa muhogo/nanihiii......,nanihii haina kautamu fulani ambako ingekuwa una njaa udenda ungekutoka.

Staili ya kula ni kula.
Na kuna mtu kadhaa wanaweza kuniambia kuwa matumizi makubwa ya mdomo ni kula.

Swali:
  • Ushawahi kutumia mdomo kutema mate?
Hebu pumzika kidogo na Jamie Foxx , akijaribu kuwafanya watu wachekelee kanyau.


Utamu wa ubwabwa msibani na ule ubwabwa uliojipikia , kisaikolojia unaweza kuwa na tofauti.
Lakini matumizi ya ubwabwa na kiporo cha makande ndani ya mwili hakuna tofauti kubwa sana.
AU?

DUH!
Hebu msikilize kidogo Bill Withers atukumbushe wanaume jinsi yakukubali nanihiii fulani zihusianazo na maamuzi ya wanawake.


DUH!
Tatizo la kula, halisaidii kutumia kikojoleo.
Tatizo la ubongo , halisaidiii kuwa na busara au kuwa na kitu binadamu fulani wamekiita akili.

Swali:
  • Hivi unaakili?
  • Hivi asiyekuwa na akili ni nani?
  • Matumizi ya akili yako yameshawahi kukusaidi kukosa furaha?
DUH!

Naacha basi!
Jumatatu njema!
Tumia lakini kitufulani kinamna.Unajua tena matumizi ya kitu fulani muhimu kinamna kama kitu fulani unacho. Usipotumia si maana yake kitakosa makali kile kitu ikiwa ni ubongo au sindimba.

AU?

Nakuacha na Onyx


BAADAYE BASI!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP