Ukichunguza ni wapi BINADAMU hutolea hasira zao waweza hisi tabia za BINADAMU wakiwa na hasira ni za KIMALAYA!:-(
>> Tuesday, September 21, 2010
Kulengesha hasira kwa kikutiacho hasira tu ni bonge la SANAA,...
....na si watu wengi wanapatia kulengesha hasira kwa aliyewatia HASIRA,...
.....na hasira zao huzigawa ovyoovyo kama tu MALAYA WAGAWAVYO,...
... ndio maana kuna WAKOROFISHWAO na LIMKE na kuanza kupiga WATOTO wasiohusika na yao ya WAZAZI.:-(Swali:
- Unabisha?
Wengi wenye hasira,....
...... chochote kilichombele yao wanaweza kukitolea hasira,....
.... ndio maana hata mtandaoni unaweza kukuta LIMTU limechukizwa na LIMPENZI lake huko na kuja mtandaoni kutoa hasira kwa kutukana WATU WENGINE ovyo.:-(Swali:
- Unabisha?
- Unafikiri wewe unajua kukwepa kulengesha HASIRA ZAKO kwa yahasira yako yasiyo WAHUSU?
Ndio kuna waudhiwao na KUKU,...
.... na kwa kuwa tu wamuonaye mbele yao NI BATA basi wanafikiri kwa hasira za KUKU ni sahihi kumpiga BATA bonge la teke.:-(Swali:
- Unabisha?
Na ni ndio,....
...pamoja na yote ni vizuri kumbuka KUNAWAKUCHEKEAO kutokana na kwamba walikotoka WAMESHACHEKESHWA na mambo mengine ,...
... na nikweli wala llabda siku hiyo wewe HUCHEKESHI.:-(
Swali:
- Si unajua kuna WAUME wa watu ambao huchekewa na kufurahishwa zaidi kwa kuwa tu mama watoto wakati KIDUME yuko kazini alichekeshwa na kufurahishwa vizuri tu na HOUSEBOY aka kwa lugha ya kitaalamu -´´Mtumishi wa nyumbani wa KIUME``?
- Si unakumbuka si kweli furaha zako haziwafurahishi hata adui zako hasa ukizingati kuwa wewe ukitabasamu unakuwa mzuri kweli kwa kila mtu na sio tu kwa mpenzi wako wa siri PADRE kwa kuwa hata SHEKHE anapata ile kitu roho -samahani -MWILI YA MTU inatamani ?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ruksa kulibishia!:-(
Hebu Heavy D arudie tena ndude- Mr BIG STUFF
HEAVY arudie na -Nuttin' but LOVE
Au tu Heavy D and The BOYS warudie pia na ndude-Now tha we have found LOVE
Ndio niliwadaka Jacaranda wakifanya vitu vyao
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment