Katika kutetea haki ya watu KUJISAIDIA HADHARANI!:-(
>> Tuesday, September 21, 2010
[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]
Kuna MAMBO huhitaji uwe na kidhaniwacho ni TABIA MBAYA hadharani,...
..... laasivyo unaweza KUJINYEA BURE HADHARANI wakati ni kweli ulipo hakuna vyoo hadharani na labda katika kibano hicho BUSARA ni kunya HADHARANI!:-(Swali:
- Unadhani kati ya KUJIKOJOLEA au kwenda msalani pembeni ya gari la MBUNGE hadharani kama umebanwa ni nini busara?
- Unauhakika ni rahisi hivyo kujisaidia HADHARANI wakati unalaumu wajisaidiao HADHARANI wakati vyoo vya uma haviko hapo HADHARANI?
Na wakati niko katika HOJA nawezakusema pia UDHAIFU wa wenye tabia nzuri HADHARANI,....
... ni moja ya kichangiacho TABIA MBAYA HADHARANI!
Swali:
- Kwani unafikiri kwa kuwa unaTABIA NZURI zikufanyazo umekaa kimya HADHARANI wakati adhaniwaye KIBAKA anabwengwa bila uhakika kama kweli KAIBA, wananafunzi wananyanyaswa kwenye DALADALAZ mbele yako, watoto wanatukanana ,........ hakuna uwezekano TABIA YAKO NZURI YA KUKAA KIMYA hadharani inachangia TABIA MBAYA uzichukiazo HADHARANI?
Ndio,...
.... kuna hata MABLOGA wajulikanao kwa tabia nzuri MTANDAONI,...
....INGAWA wanatabia NZURI wakijulikana majina tu ,...
...na ukiwastukia kumbe ni haohao wenye tabia mbaya chumbani/WAKIWA ANONYMOUS unaweza hata kuanza KUHISI kuwa mmoja wa waliowahi kukutukana mtandaoni ni yule MCHUNGAJI / SHEKHE wako ambaye anatabia nzuri sana na unadhani hana matusi ya nguoni kwa jinsi umjuavyo HADHARANI kisa umestukia KITU kwa KUSTUKIA kumbe Simon KITURURU umdhaniaye hana adabu HADHARANI ni yule mwenye tabia nzuri kweli chobisi asikoonekana.:-(
Ni wazo tu hili MKUU na nakutakia KAMANYOLA bila JASHO Mkuu!
Au ngojea nikuage kwa ung'eng' e -BADAYEZ!Kwa kubadili hali ya hewa hapa KIJIWENI tumrudie Lil VICIOUS wakati bado kinda ingawa msiniulize BUSARA za kumuachia mtoto aongee aongeayo LIL VICIOUS ni nini tukianza na -FREAKS
Au tu Lil VICIOUS arudie- NIKA
Lil VIcious amalizie na-The GLOCK
Au tu tubadili kwa kumuachia mtoto wa Will Smith kwa jina Willow alainishe kwa-Whip my HAIR
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
siku moja inawatu wengi .... cha ajabu ni walewale wenye jinsia ya kike na kiume...
siku moja ni ileile yenye mawio na machweo... sasa kuna uhakika kuwa mwenye jicho chongo hawezi kuona machweo?.... Duh nawaza tu hapa nimejaa kibwanyenye
Post a Comment