Kutoka mdomoni mwa Spika wa Bunge la Tanzania
>> Tuesday, December 05, 2006
Wiki kadhaa zilizopita nilipata kusikia hoja moja kwa moja kutoka mdomoni mwa Spika wa Bunge, Mzee Samwel Sitta. Kuna mengi aliongelea. Ingawa pia kuna mengi hakuweza kuyaongelea kutokana na muda mdogo uliokuwepo na maswala na maswali kuwa mengi.
Aliongelea umeme. Akasema kuwa sasa hivi ndani ya Tanzania kuna mpango wakutumia nyanja tatu za uzalishaji wa umeme. Kuna Wachina ambao wataanza kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe katika sehemu mbili tofauti Tanzania.Pia kuna mpango wa kuongeza sehemu moja ya uzalishaji wa umeme kwa maji.Umeme wa gesi unafanyiwa mpango kuingizwa katika mfumo pia. Kwa kifupi kuhusu mashine mpya za dharura ziletazo majadiliano mengi mtandaoni amesema zinahitajika na pia kuwa bila mashine hizi za muda sehemu kama za Mwanza zingekuwa zinakosa umeme masaa ishirini na nne.
Kuhusu matatizo ya Zanzibar alisema tatizo kubwa liko katika uhasama uliojengeka kabla na baada ya mapinduzi. Asilimia kubwa ya wenye asili ya kiarabu au kipeshia ndio waliokimbia visiwa baada ya mapinduzi. Na wengi wao ,takribani laki tatu wako Uarabuni. Hawa na ndugu zao ndio wenye pesa na elimu. Maana hawa ndio walioweza kuwasomesha ndugu zao visiwani na hata nje. Lakini hawa ndio ambao wanachuki juu ya yaliyotendeka baada ya mapinduzi. Baadhi yao walilazimika kuolewa na wasiowapenda hata kuzalishwa na wasiowapenda. Sasa hivi wengi wao ndio wako katika upinzani visiwani.Kwa mtazamo wa Spika hawa jamaa hatakama wanaona ukweli wa mambo hawawezi kuukubali kwani bado yale machungu yayaliowatokea bado yapo ndani ya jamii yao. Hivyo ni vigumu kudili nao kwani mara nyingi ni machungu ya kihistoria ya wapandishayo mori na sio hali halisi ya mambo.
Kuhusu Umoja wa Afrika Mashariki , yeye anaona hakuna haja ya Watanzania kuuogopa muungano. Alisema kunanjia nyingi za kisheria ambazo zitawalinda Watanzania katika mambo mengi. Anasema kuwa kwa mfano ndani ya muungano kutakuwa na sheria kama za kuzuia asiyekuwa Mtanzannia kumiliki ardhi Tanzania nk.Alisisitizia kuwa tunahitaji kuungana ililikukuza soko la Afrika Mashariki kwani tukijitenga ni vigumu kuvutia wawekezaji wenye kuvutiwa na soko na pia itasaidia kujengea wanaafrika mashariki soko kubwa zaidi la bidhaa zao.
Aligusia pia maswala ya Watanzania waishio ughaibuni na maswala ya usalama wao. Anasemakuwa serekali inajua matatizo ya Watanzania Ughaibuni na inayafanyia kazi. Anasema baadhi ya misiba iliyotokea Ughaibuni ilipewa hadhi iliyokaribia ya msiba wa kitaifa Tanzania. Alisisitiza watu kujisajili kwenye mabalozi yao ilikuwezesha baadhi ya mambo yawe rahisi kwa balozi kushughulikia.Alisema serikali inafuatilia vifo na matatizo ya Watanzania ughaibuni.
Kuhusu wawekezaji wa Kiafrika kusini alidai kuwa si kweli kuwa wao ni wabaya. Alidai matatizo mengi ya kibiashara na dhuluma za kibiashara hufanywa na wahindi.Alisema kuwa kwanza mfumo uingizwawo na waafrika kusini unasaidia kurekebisha biashara. Kwa mara ya kwanza unaweza kupata uhakika wa bei za vitu na pia wameleta utumiaji wa viwango vya ubora wa bidhaa ndani ya biashara Tanzania. Anasema si kweli kuwa Waafrika kusini hawanunui bidhaa za Tanzania. Anasema wao hutoa viwango vya ubora wa bidhaa watakazo kuzinunua. Katika mazao hutoa mpaka aina za mbegu za vyakula watakavyo kuviuza. Na watanzania wote wafikiao viwango vitakiwavyo ,bidhaa zao huingizwa dukani.Alisema kuna tatizo sana kwa wahindi kufanya biashara chini ya meza na kupeleka pesa nchi za nje.
Haya ni baadhi tu ya aliyo yasema muheshimiwa.Maswali mengi hakujibu kutokana na muda.Nikikumbuka mengine aliyoongelea nitayaandika hapa.
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Asante Simon kwa kutupa aliyosema Spika wa bunge. Anasema wahindi ndio wabaya zaidi kuliko makaburu sio?
Asante sana kwa taarifa hii ya maelezo ya Spika Sitta
Post a Comment