Baada ya mafanikio ya Asia je, ni Afrika iatakayofuata?
>> Tuesday, December 05, 2006
Hakuna ujanja, baada ya Asia itakuwa ni zamu ya Afrika.Huu ndio mtazamo wangu.Kwa jinsi uchumi wa Asia unavyokua ni rahisi kujua kuwa na gharama za uzalishaji wa bidhaa zifanyazo makampuni mengi yaende Asia kuongezeka. Na kama kawaida ya mfumo wa biashara ulioshamiri duniani lifuatalo ni wawekezaji kukimbilia katika sehemu ambazo wanaweza kuzalisha bidhaa zao kwa bei ya chini. Sehemu ambayo haijatumiwa kisawasawa katika uzalishaji mali ni Afrika. Asia ilipata umaarufu kama sehemu ya kuzalisha mali kwa sababu kubwa mbili,unafuu wa gharama za uzalishaji na pili, uwepo wa wafanyakazi wenye taaluma za kazi.Ingawa pia huwezi kupuuzia nguvu ya idadi ya watu waishio Asia ivutiayo wawekezaji kwa sababu ya soko kubwa.
Tatizo kubwa la Afrika ni ukosekanaji wa wafanyakazi wenye taaluma za kazi.Ukosefu wa mfumo uelewekao uwezeshao mambo kufanyika. Hapa na maanisha udhaifu wa institutions na mifumo iwezeshayo mambo kufanyika. Tatizo la nishati za umeme ziwezeshazo uendeshaji wa viwanda.Ukosefu wa nguvu za ununuzi kutokana na umasikini wa watu.Haya ni baadhi tu ya mambo yatatizayo. Lakini, bado kila kukicha utakutakuwa inakaribia siku ambayo dunia haitakuwa naujanja wa kukwepa Afrika kwani ,Afrika inazidi kuwa ndio sehemu itakayo kuwa inatoa faida zaidi katika mitaji ya wawekezaji.
Inashangaza jinsi viongozi wetu Afrika wanavyoweka umuhimu wa mambo gani yatendeke ili kuboresha nchi zao. Unakuta kiongozi anazunguka dunia kutafuta wawekezaji katika viwanda wakati anajua wawekezaji hao hawawezi kufanya lolote bila ya nishati ya umeme. Mifano ipo mingi tu ambayo hata haileweki kuwa hawa viongozi wetu wanafikiria nini.
Si ajabu sasa hivi kuona Wachina wakihamia Tanzania ingawa kwao Uchina ndio wawekezaji wengi wa kimataifa bado wanakimbilia. Hii ni moja tu ya kidokezo kuwa tabaka la wenye navyo Uchina linazidi kuongezeka hivyo wengine inabidi wakimbilie sehemu ambazo wanaweza kujishamirisha bila kuwa na mtaji mkubwa.Pamoja na sera za serikali kusababisha hili kuwezekana sasa, lakini ukweli kwamba hili ni jambo ambalo imefikia kipindi chake kutokea hasa ukiangalia mwelekeo wa uchumi dunia nzima.Ukiangalia hata mwelekeo wa nguvu za nchi ziendeshazo mifumo iliyojengeka duniani zinavyobadilika utapata dondoo nyingine.
Sitaki kuusifu huu mfumo wa kibepari ambao umetunyonya kwa mamia ya miaka, lakini najua mfumo huu unakasumba moja, nayo ni kwamba hufikia wakati mewnye nguvu anakuwa hana uwezo tena wa kutawala mwelekeo wa mfumo. Kwa mfano kuna savei nyingi zioneshazo kuwa asilimia mpaka 60% za Waulaya na Wamarekani wanatishika na ukuaji wa uchumi wa nchi kama Uchina, lakini hakuna ujanja wawezao kuufanya kujitoa katika mahusiano na na nchi hizi sasa hivi. Kwani Wachina wameweza kuwazidi kete katika mchezo wao wenyewe.
Mifumo iundwayo na binadamu mimi naamini huweza kuchezewa kete na binadamu. Ukiangalia maswala ya demokrasia, imedhihirika mara kibao kuwa ilikuwa sio nia ya waihubiriyo baada ya walengwa kuitumia kwa kuchaga kidemokrasia maswala ambayo wahubiri hawakuya dhamiria.Mfano kidemokrasia , Wapalestina wakachagua Hamas jambo ambalo ilikuwa si nia ya Marekani kuhubiri demokrasia itakayo chagua maadui zao. Hili limetokea Venezuela pia baada ya Chavez kushinda tena. Naamini sio demokrasi tu zinaweza kutoa jawabu kinyume bali hata maswala mengine. HAPA NA MAANISHA INGAWA WANAOTULENGA AFRIKA WANATULENGA ILIKUTUNYONYA TWAWEZA KUWAGEUZIA KIBAO WAKAJAKUJIKUTA KUWA SISI NDIO TUMEWAZIDI TUKITUMIA AKILI.Itafurahisha siku tukifikia sehemu China waliyofikia ambapo hakuna ujanja nchi nyingine zawezakuwaletea bali kudili nao tu, hata ikiwa kwa shingo upande.
Afrika na pamoja na umasikini wa serekali zetu hatuwezi kujitoa kirahisi katika mfumo.Bado asilimia kubwa za pesa ziendeshayo shughuli Afrika ni tupewazo na wamagharibi. Mpaka uendeshaji wa Afrika Union unashindikana kutokana na ukosefu wa pesa na kila ukifanikiwa ni kwasababu kunamfadhili katoa pesa.Sasa tuna taratibu gani au strateji gani zitakazo tupa nguvu ya kuja kuzishika nyenzo za kiuchumi za nchi zetu?Je , mipango hii tuwekayo inatazama mbele? Au ndio kama maswala ya umeme?Kwa maana maswala yaumeme hayakupewa mstari wa mbele kama maswala ya rada na ndege ya Raisi. Je, Viongozi wetu wanaona mbele?
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment