Vyakula vipo duniani, mbona twafa njaa?-----Na .1
>> Tuesday, December 05, 2006
Konokono huyu kanona!
Konokono huliwa sehemu nyingi lakini ni maarufu zaidi Ufaransa , Uspain ,Italy na Ureno. Afrika kusini kwa sasa ndio inaongoza katika nchi za Afrika katika biashara ya kimataifa ya konokono. Ushawasikia wakinamama hawa wa Western Cape township walivyojiajiri katika maswala ya kukusanya konokono?Kwa habari zaidi kuhusu kama unadhurika (allergy) kivyovyote kuhusu msosi huu soma hapa
Chura aliye nona kabla ya kuingizwa jikoni.
Kwa habari zaidi kuhusu msosi wa chura na kama unazurika naye (allergy) soma hapa
Chura hawa washaiva , karibuni mezani.
Panzi ni msosi babu kubwa
Nyoka ni msosi mahali pengi.King Cobra pichani ni miongoni mwa nyoka ambao katika mitaa ya nchi kama Thailand, damu yake pia ni kinywaji kiaminiwacho kuongeza nguvu za tendo la mapenzi na pia dawa kwa magonjwa
Bado najiuliza, nini kinasababisha tufe njaa Tanzania ?Kwa maana sidhani hata inahitaji kuangaika sana kutafuta mnyama, mdudu, ndege nk ambaye analika.
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nadhani ili konokono kushamiri panahitajika mvua. Wadudu hawa wanapenda nyevunyevu. Watu hufa njaa kwa sababu ya ukame - inapokosekana mvua.
Penginetuangalie ni jinsi gani ya kuwahifadhi hawa konokono kwenye makopo, ili mvua ikipiga chenga tufungue maghala ya konokono wa kopo.
Hakuna sababu ya kufa njaa.
Halafu ndio hapo mtu utakaposhangaa kuwa kwa miaka maelfu watu wameishi majangwani wakitegemea maji ya kwenye oasis. Mpaka siku hizi nasikia watu hawa majangwani hawakosi kunywa kahawa .Halafu utakuta watu wanakosa msosi wakati wamezungukwa na maziwa yote makubwa Afrika.Kazi ipo
MMMmm yummy! Naona nishakula kilakitu hapo kasoro Nyoka. Unajua pia konokono wa baharini ni watamu sana!!!!!! Ingekuwa vizuri duniani tule karibu kilakitu kama wenzetu watu wa Asia.
Post a Comment