Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tukondani ya KWANZAA na tukisubiri Mwaka mpya wa Kalenda ya Kirumi...

>> Thursday, December 28, 2006


Kabla sijasema sana ningependa kuachia The Last Poets wamwage shairi....


Watu weusi bado tumegawanyika sana.Moja ya mgawanyiko ni ule wa Weusi wa Afrika na weusi wenye asili ya Afrika ambao kuwako kwao mbali na Afrika ni matunda ya utumwa, na wengine ambao walihama wenyewe. Waafrika ndani ya Afrika bado tumegawanyika sana pia, kimakabila , kidini,kiutajiri au umaskini na mambo mengine kemukemu ikiwa mpaka rangi.Unakumbuka katika kundi la watu weusi bado tunabaguana kwa rangi , nani mweupe na nani mweusi? Watu weusi waishio mabara mengine nao wamegawanyika kwa hali ya mali,elimu na hata jinsi ya toni za mwonekano wa rangi ya weusi wao . Marekani na sehemu nyingi bado ile hali iliofanya watumwa weupeweupe kupewa kazi za ndani na wale weusi kabisa kazi za nje bado upo.Hivyo bado wale weupe weupe mara nyingi huonekana wazuri kuliko weusi kabisa. Hiki kitu ndio kile kile kinachofanya akina dada kujichubua Afrika katika kutafuta kuwa weupe weupe kwa imani ya kuwa ndio uzuri. Hivi uzuri ndio nini?Haya mambo ambayo binadamu anajitengenezea akilini na kutengeneza mazingira ya kuhalalisha mtazamo yanazingua sana.

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana! Kila wakati na kila siku yuko shuleni. Anajifunza ladha na anajifunza kuishi katika mazingira yake. Ndio maana kila siku utasikia, alah! Hiyo fasheni imepitwa na wakati! Halafu ghafla atakuambia nilipoonja bia kwa mara ya kwanza sikupenda ladha yake.Wakati yeye ndiye ajulikanaye kwa unywaji wa bia. Binadamu huyo huyo katika kutafuta kujiridhisha huwa anapenda kujifananisha na wenzake na kujipima kupitia wenzake. Hii pamoja na kujipatia furaha pia huleta mikwaruzo ndani ya jamii.Mikwazuzo hii hutugawa lakini pia kutujenga.Tatizo letu watu weusi bado tumeshindwa kuunganisha nguvu zetu na mikwaruzo yetu inatubomoa zaidi yakutuletea changa moto zakutujenga.


Tukirudi kwenye KWANZAA, mimi naona ni moja ya jambo ambalo pamoja na mengine linajaribu kuunganisha watu weusi. Na nafikiri jambo lolote liunganishalo watu weusi wenye asili ya Afrika ni jambo muhimu kwa sababu umoja tuna uhitaji sana sisi kama watu weusi.Vizazi vijavyo vya watu weusi vitashindwa kutuelewa ni namna gani Afrika pamoja na mali zetu bado tumefanikiwa kuwa masikini na wanyonge hivi.Kizazi chetu hiki tu bado tuna maswali ilikuwaje wakoloni wachache waliweza kututawala .Unakumbuka tulikuwa tunawabeba kuwasafirisha maporini? Unakumbuka mara nyingi ilikuwa waafrika wanne wanambeba mzungu mmoja na anatoa amri hata huko msituni, huku watu wakitii?Sasa fikiria baada ya miaka kadhaa sisi ndio tutakuwa somo.Vizazi vijavyo watajiuliza, hivi hawajamaa vipi? Kila siku kugombana tu huku wakijua maugomvi yao yananufaisha wengine.

Sasa hivi kuna Wamarekani weusi watambuao umuhimu wa Afrika katika maisha yao lakini wapo wengi wachukiao Afrika na waafrika.Wao kwa wao hawana umoja , wamegawanyika hadi kwenye maadili.Waangalie wengine hawa hapa wakijielezea....


Nasi Afrika hatujakuwa mfano mzuri wakujivunia. Na katika hili na kubaliana na wale wanaoenzi nguzo saba za kwanzaa ambao wanatafuta maadili kutoka Afrika ilikujisikia kamili.Kwani hata kwa hili kuna kaumoja kanajengeka. Kumbukeni kama watu weusi ni miaka mingi imepita bila kula raha na kufurahia uweusi wetu.Ngoja Mighty Diamond wakukumbushe hapa chini...



Sasa mimi na wewe tunafanyanini katika kuleta mikwaruzo yetu na tofauti zetu kama watu weusi iwe inatujenga zaidi ya kutubomoa?

Samahani nilisahau kuwa bado tuko katika shamra shamra za KWANZAA, kusubiri mwaka mpya na kadhalika nyingi!Haya basi tuendelee kufurahi. Nakuacha na Lagbaja hapa chini.


Heri ya KWANZAA!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 3:11 pm  

hiyo sinema inayoonyesha kugawanyika kati ya ma-uncle tom na waafrika sana, imenichengua kidogo.

Katika mambo wanayosema waafrika sana ni kuwa akina Jesse Jackson na Condoleeza, powell na wengine wamekata tamaa na ni sawa tu watu weupe wanaowakandamiza - wame-sell out.

Katika historia kila mara lengo limekuwa kujipa nguvu na ikiwezekana kuanzisha taifa lao au kurudi Afrika - hayo hayajawezekana - na ilipowezekana Liberia matabaka kati ya waliorudi na wengine yakazaa Samuel Doe, na hata sasa wenye asili ya waliorudi wamerudi nguvuni.

Kuhusu sherehe za kutuunganisha - ni vigumu kuwakutanisha watu wenye faslafa tofauti kuamini katika umuhimu na "ukweli" unaoambatana na sherehe, hivyo inawezekana tukaendelea tu kusherehekea falsafa tofauti.

kitu kinachounganisha kusherehekea krismasi ni consumerism na media hype, wameanza zamani.(huko china mwaka huu mauzo ya zawadi za krismasi yameongezeka bila watu kujua krismasi ni nini)

Nina mashaka kwamba sio waafrika wote wanaoamini katika kwanza na nguzo saba hata kama nia ya kwanza ni nzuri - hivyo itachukua muda sana kupiga debe mpaka wengi waunge mkono, na wakiunga mkono pengine itaambatana na consumerism sawa na ya krismasi bila watu kujua sana maana.

Saa nyingine nadhani tunakwama pale ambapo tunajaribu kupinga ukandamizwaji kwa kutumia silaha zile zile zilizotumiwa kutushambulia. kuna madhehebu ya kiafrika yaliyotumia Uislamu 'black Muslims" na nadharia za kibaguzi zilizotumiwa na wakandamizaji ili kuwaunganisha waafrika na kuwapinga wabaguzi, au wengine wanatumia biblia kwa minajili hiyo hiyo iliyotumiwa na wakoloni na wabaguzi.

Pengine ni wakati muwafaka wa kusherehekea kwanza - wiki ya krismasi na mwaka mpya - wiki ambayo kwa mujibu wa wapinga krismasi ni wiki ya kusherehekea upagani huko ulaya palipoanza krismasi.

Kwani vipi tungeanza na ukurasa mpya usiofanana na ule wa wazungu, labda tukaikuza sabasaba au nane nane halafu tuwaalike waafrika wote washerehekee.

Simon Kitururu 1:51 pm  

Ingekua poa sana tungefungua ukurasa mpya kabisa Afrika. lakini nadhani itakua vigumu sana kukwepa consumerism na media hype hata tukianzisha siku zetu.Kwanzaa miaka arobaini sasa na watu wengi hata ndani ya Marekani hawaijui.Lakini kitiacho moyo ni kwamba ilianzishwa na mtu mmoja.Hii inanipa moyo kwamba kama mtu anawazo zuri na akalifanyia kazi basi linawezekana. Sasa hivi mpaka serikali ya Marekani imetoa stempu ya Kwanzaa , mimi naona ni moja ya hatua .

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP