Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Biblia imetafsiriwa Kiafrika!

>> Friday, July 07, 2006

Nimecheki BBC wananiambia Biblia imetafsiriwa kiafrika na imevunjwa bikira hapo kenya .Kongoli hapa basi usome habari hiyo.Ila Kama umeshaisoma Biblia hiyo tupashe basi. Bwaya Upo?
Sasa hivi ina semekana katika Afrika ni Pentekoste na makanisa ya kiavenjeliko ndio yanayoongoza kukua Afrika.Kongoli hapa kushuhudia. mimi nachojiuliza nikwamba kwanini makanisa na wainjili kutoka Ulaya wanakazania kwenda Afrika wakati huku kwao ulaya siwaoni wakihubiri kwa hawa Waulaya ambao wengi wao hata Mungu hawaamini tena. Mwandani niambie huko Australia Ukristo Unaanguvu?

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 2:29 pm  

Binafsi sijaitia machoni hiyo Bibilia iliyoandikwa kwa kiafrika. Nadhani hata ingeandikwa vipi ujumbe mkuu utabaki kama ulivyo. Kama watakuwa wamebadili kiini cha ujumbe – hiyo haitakuwa Bibilia tena.

Sawa tu na vile shehe mkuu akisoma Kurani kwa Kiarabu halafu akafafanua kwa Kiswahili. Kurani itabaki kama ilivyo.

Kuhusu hili swala la dini ughaibuni huku, naona kimsingi hatutofautiani sana isipokuwa tu raia wa nchi za magharibi wanafanya mambo yao yote wazi wazi zikiwemo imani za kipagani. Hata kwenye televisheni niliona kikundi kimoja cha muziki kinachoamini imani za kishetani katika maana halisi, kuna wanawake watano na mwanamume mmoja – basi hawa wanafanya ngono kwa ujumla huku wakiabudu miungu ya watu wa Ireland wakichanganya na miungu ya Kiskochi, pamoja na mawe fulani makubwa yaliyoko Uingereza. Wanafanya yote wazi wazi.

Halafu kutokana na takwimu za watu wanaohudhuria kwenye makanisa inaonekana bora nchi hii iitwe ya kipagani vile wahudhuriaji ni wachache sana.

Hata ukiwauliza walio wengi kwenye mitaa wakati wa sherehe za krismasi kama kweli wanaamini kuwa Yesu alizaliwa wakati huo na kuwa ndiye mkombozi wao – watakwambia – hawana uhakika bali wanaamini “there is a higher being, certain kind of force, like, like… something is out there, you know god is within me, that good in me, you know…”

Kila mwaka hapa mjini Adelaide kuna tamasha linaloitwa “Body and Mind Psychic Expo”. Kwenye tamasha hilo panauzwa vitabu vya elimu za dini mbalimbali, panauzwa uchawi, kuna maduka ya kupiga ramli, kusoma mikono, kusoma nyota na maduka ya vitabu vya elimu dunia.

Kwa wastani tamasha hilo hupata wata watu kama 65 alfu kwa siku – unaweza kudhani uko uwanja wa maonyesho au kombe la dunia. Watu wote hawa wanaopiga ramli na kununua hirizi au vito vya kuwakinga shari kwa kifupi nadhani wanatafuta uhakika na ushupavu ndani ya maisha yao.

Huwa nawafananisha sana na zile hadithi za mtu kwenda Bagamoyo kabla ya uchaguzi au kupata ngekewa kwenye fani.

Wanajaribu kuukimbia udhaifu walio nao. Hawana uhakika na vipaji walivyo navyo au nguvu ya juhudi zao wenyewe. Uhakika wa nafsi zao umetetereka, haswa vile wameshupalia itikadi za individualism na sexuality.

Basi talaka kila kukicha, aina zote za ngono ruksa, uwongo ruksa – na furaha ya kweli maishani inazidi kuwapiga chenga.

Wanajaribu kutafuta majawabu ya mustakabali wao – labda kama wataendelea kuishi kiroho baada ya kufa, au kama wanafanya yaliyo sawa hapa duniani. Ili mradi tu wanachakurachakura kama kuku tangu mawiyo mpaka machweo japo wapate jawabu.

Naafiki, hawa makanisa ya kiinjili ndiyo yanayoongeza sana waumini pengine kutokana na kwamba yanawapa uhuru zaidi waumini kusoma maandiko ya Bibilia na kujadili wao wenyewe bila kupitia kwa watalaamu. Kuna kanisa moja linaitwa Hillsong lina waumini kiasi alfu kumi na zaidi kila wiki.

Nishakujazia kurasa. Baadaye.

Christian Bwaya 5:49 pm  

Hivi biblia ikiwa ya kiafrika ndio iweje? Nini kibadilike? Itusaidie nini kipya?

Haya jamaa wanahangaika na sioni wanachohangaikia. Kama ingetokea wakaja na biblia yenye tamaduni na imani tofauti na hii tunayoijua ya ukristo, hapo ningesema afadhali! Ya nini kuhangaika na kitu kilekile? Hawana jipya.

Mimi nilishangaa kuona habari hii BBC. Nikawaonea huruma. Ushauri wangu. Watafute nyingine yenye imani za kiafrika zinazoitwa za kipagani wazitengenezee torati. Hapo ningewaelewa.

Christian Bwaya 2:52 pm  

Halafu kitururu hili suala la hawa wazungu kujifanya wanajua sana kuhubiri dini huku Afrika wakati huko kwao hawahangaiki, linatia shaka. Hivi kama wokovu wanaouhubiri hauwafai wenzao (ambao kimsingi wamepotoka zaidi wa waafrika wanaowakimbilia), kwa nini waje kwetu? Hivi huyu Bwana anakuwaje na upendeleo na waafrika tu na aone umuhimu wa kuwatuma wao kuja huku tu na sio huko? Nadhani kuna the hidden agenda.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP