Nina Ndoto
>> Saturday, September 23, 2006
Nina ndoto siku moja WaTanzania tutakuja kupendana.Kwamaana sasa hivi hata katika mablogu maoni mengi ni ya matusi na kujaribu kukatishana tamaa.
Nina ndoto siku moja tutagundua kuwa umiliki wa mali si muhimu sana katika maisha.
Nina ndoto kwamba Tanzania haitakuwa ina wasiwasi itakumbwa na njaa.
nina ndoto kuwa ndugu na jamaa katika dunia yetu watagundua kuwa kweli sisi ni ndugu na jamaa.
Nina ndoto kuwa Tanzania itafikia kuwa elimu ni jambo ambalo Mtanzania akiamua kulipata, hulipata bila ya kipato cha familia au chake kuwa kama ndio kithibitisho cha upataji wake wa elimu.
Nina ndoto kuwa Tanzania na Watanzania watadhihirika kuwa ni kielelezo cha jinsi uungwana na waungwana watakavyo kuwa.
Nina ndoto..................
Alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhh!
Sasa Desmond Tutu ananitisha !Anasema kwa mtazamo wake Waafrika Kusini wamepoteza dira! Halafu nasikitika kwasababu namuunga mkono. Maadili ya mwanzo ya kupigania uhuru,usawa na umoja hayaendani na ya sasa ambayo ndugu kwa ndugu wauana, wabakana,nk.Anashangaa hata inavyo fikia hata Mzee Zuma anaachiwa tu,na labda atakuja kuwa Raisi wa South Afrika.
Msome hapa akilalamika.
Alaaaaaaaaaaah!
Sasa kwanini watu tunaamuatu kutukanana bila sababu? Je tumekosa pakupelekea matatizo yetu?. Wakatoliki walikuwa wakienda kutubu kwa Padre.Waislamu kwa mashehe kupata mawaidha.Sisi wengine tulikuwa tuna enda kwa wazee wetu. Wote tulikuwa na ndugu na jamaa ambao tuliweza kusawazisha mabo yetu. Sasa ni kweli tumekosa pa kwenda kupeleka mambo ya zinguayo mioyo yetu mpaka twatukanana wenyewe kwa wenyewe?Mpaka twafikia kuumizana na maranyingi bila sababu? Mpaka twauana wenyewe kwa wenyewe?Je ni umasikini tu huu? Wamagharibi wana Matherapi, wana masaikolojisti sasa kwanini sisi tuue tamaduni zetu ambazo zilikuwa zimejengeka , zikiunganisha haya mambo yote kama kweli hili ndio pungufu sasa?
Nina ndoto siku moja Waafrika tutaamka nakugungua kuwa bado hatujachelewa na tuna weza kuokoa baadhi ya mambo yetu ambayo ndio msingi wakusimama kwetu kama waafrika.
Hivi ile ndoto ya Martin Luther King iliendaje vile? Hivi inatuhusu sisi Waafrika ?
Ndoto yako ni ipi?
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
ndoto zetu zinafananafanana
Post a Comment