Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Najisikia vibaya kwa kuwa najisikia vizuri!

>> Monday, September 18, 2006

Kuna mambo mengine mengi katika maisha ambayo hukatisha tamaa. Moja wapo linalonisumbua leo ni ukweli kuwa miongoni mwa viongozi wa Ivory Coast alihalalisha kumwagwa uchafu wa sumu kutoka magharibi nchi mwake.Sasa raia kibao wanaumwa kutoka na na uchafu huo wa sumu ulioletwa na meli nchini humo.Hili pamoja na mengi tu yamekuwa yana nizingua.

Kwa bahati nzuri nimefanikiwa kula chipsi dume na kachumbari leo .Kitu ambacho sijawahi kukifanya kwa muda mrefu kutokana naukosefu wa mihogo katika anga niliyopo.Ghafula nikaanza kujisikia vizuri. Na nikamalizia na wimbo wa James Brown I feel good kama uonekanavyo hapa chini.Lakini naanza kujisikia vibaya kwa kujisikia vizuri kutokana na kitu kidogo kama hiki.


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Maisha 10:01 am  

sasa mihogo uliitoa wapi kaka?

Simon Kitururu 5:17 pm  

Rafiki yangu kiana kaweza kuingia nayo nchini.

Maisha 12:14 pm  

raha basi.sisi hapa ofisini kwetu tunakula mihogo kila siku.na viazi vitamu vya kukaanga.na chachandu...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP