Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAMBO YA KIUCHIUCHI, SHEPU ZA MATAKO NA MATAMANIO

>> Tuesday, September 19, 2006


Nice ass





Huwa na shangaa sana jinsi binadamu anavyojenga sababu na anavyo halalisha matamanio.
Katika nchi za magharibi nilizowahi kuishi, utakuta wanawake kwa wanaume walio wengi wana ladha tofauti katika swala la vikalio, na uwezo wake wakufariji matamanio.Hii hasa ni katika kukidhi mvutanio wa jinsia ukifananishwa na wa watu weusi wenye asili ya Afrika. Kinacho nishangaza ni kwamba asilimia kubwa ya watu weusi watakuambia shepu kubwa za vikalio ni muhimu katika matamanio yao. Weupe watasema vikalio vilivyopigika pasi ndio vina mvuto mkubwa.

Cha kujiuliza, ni nini hasa kinatofautisha mvuto wa ngono katika ujazo wa tako?


Sauna ya Kifini ijumuishayo wanaume na wanawake.



Ukiingia katika maswala ya kukaa uchiuchi, naamini katika nchi za magharibi hakuna mabingwa kama waskandinavia. Ukisikia utamaduni wa sauna ,kwenye nchi kama Finland basi ni kasheshe.Huko kukuta dada, kaka,mama,baba,binamu na marafiki wako uchi ndani ya sauna, ni jambo la kawaida.Halafu utamanudi huu wa sauna huendana na pombe . Kwa kifupi ratiba ya sauna iko hivi; unavua nguo, unajimwagia maji au kuoga kidogo, unaingia sauna ambako unapigwa na joto kali na kutowa majasho vibabab vya kutosha, unatoka kwenda kuogelea au kujimwagia maji baridi, halafu unaketi kupata bia moja.Ukimaliza hapo unarudi sauna tena halafu mchezo unajirudia. Cha ajabu ni kwamba mara nyingi watu hawa hawaunganishi watu kukaa uchi na maswala ya ngono!

Ukirudi Afrika utakuta pia kuna tamadunni kibao ambazo kuona matiti ya mwanamke ni kawaida tu.


Nice ass!




Nachojiuliza ni kwa nini kwa wengine hapa duniani kukaa uchi ni jambo la ajabu, wengine wanapandisha ashki na wengine ni jambo la kutia aibu? Na bila kuwasahau wale wajivunialo hili jambo ambao kwako ungefunga machoi kuwaona uchi!

Je, haya mambo si vitu tu ambavyo ubongo unafanya kila mtu avitafsiri kivyake?
Je, ni vitu vya maana vya watu kupigania au kuvichukulia umuhimu?
Je, ushawahi kujiuliza ukipendacho hakina matamanio kwa kila mtu?
Je, kwanini wengine wanaringa?

Najiuliza tu , katika hii treni ya mawazo!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 4:20 pm  

Nadhani umesahau jambo moja, saa nyingine pombe hunywewa nje ya jengo la sauna watu hao wakiwa bila mavazi.

Ilikuwwa nashindwa kuwaelewa wakati nikotoka shule au kazini na kuwakuta watu bila nguo nje wanakunywa pombe na kunisalimu bila haya.

Nikiangalia picha za kwetu nyumbani zamani - au hata siku hizi kwa Mswati, kina mama wanakwenda bila mavazi... anyway nachotaka kusema ni kuwa akili ikiwaza mambo yanayolengesha ngono utaona kila kipitacho ni chombo cha hayo mambo.

Serina 10:34 pm  

Huku uswidi vilevile...lakini pombe nayo hainywiki mle ndani..joto lile we! Cha muhimu ni mtu binafsi kulikubali na kulipenda umbo lake...kuhusu mambo ya kujistiri...mwenyewe bado niko jangwani... wanasayansi kwa mfano wansema kuwa suruali haifai kubana mwili lakini wenye fesheni na wafanyibiashara hawasemi lolote kuhusu jambo hili wanapotuuzia bidhaa kama hizi...swala zuri hili la kuchangamsha bongo.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP