Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Martin Luther King Jr , Alqaida na Peter Tosh mawazoni

>> Tuesday, September 12, 2006





Martin Luther King Jr alisema kama mtu hajagundua kitu ambacho anaweza kukifia basi hana sababu ya kuishi. Cheki aliyosema hapa






Miaka mitano baada ya 9/11 nimejikuta namkumbuka Peter Tosh katika wimbo uitwao Equal Rights , akisema kuwa kila mtu anataka kwenda mbinguni, lakini hakuna atakaye kufa.

Kutokana na maswala ya haki aliyoimba, nilijaribu kufikiria bongo za wanadini wenye siasa kali wanavyoweza kujiosha ubongo mpaka wakaamini kuwa wanatafuta haki katika umwagaji damu za watu wasio na hatia.


Martin Luther King Jr aliwahikusema kama mtu hajagundua kitu ambacho anaweza kukifia, basi hastaili kuishi. Najiuliza tu !Je hawa watu wanaojiua hivi hakuna kauwezekano kuwa kaugunduzi kao ka kakitu ka kujiua, kalikuwa potofu?










Mzee Osama anashauri ujiue lakini naona yeye binafsi hajisikii kufakufa bado









Wafuasi wa Alqaida naona wamepata kitu cha kukifia kwa hiyo wameamua kujifia.Kinacho nisikitisha wameamua kujiua ilikuua na raia ambao hawajaamua kufa.
Kinachonizingua ni jinsi viongozi wa Alqaida wanavyoshindwa kufikia maamuzi ya kujiua kama wawashaurivyo wafuasi wao. Kila siku utasikia tu kuwa wamejichimbia sehemu au wamekimbia .Sasa kwanini hawataki kuwa mfano katika kujiua?Nashindwa kuelewa wana roho ya namna gani kuhalalisha mauaji ya raia wasio na hatia kwa kisingizio cha dini.

Nikiwa bado nafikiria jambo hili maswali hayaishi kunijia. Je Peter Tosh anaweza kuwa si sahihi? Je mimi na wewe leo hii tuko tayari kufia kitu?

Pia wakati maswala haya ya 9/11 yanaendelea hapa duniani, nashindwa kujizuia kukiri kuwa Waarabu wametusaidia sana watu weusi katika kutuondoa katika kitambulisho cha watu hatari.Angalau sio watu pekee tuangaliwao kwa kijicho kibaya fulani tukikatiza katika nchi za watu.

Lakini bado narudi katika swala la usawa ambalo linanukuliwa sana kama ni jambo linalo sababisha matatizo ya kujisikia kufakufa na watu wasio na hatia katika dhamira ya kufikisha ujumbe.Usawa ambao wote, Martin, Peter na Osama wanadai ni muhimu katika kuwepo amani. Nasikitika kuwa huu usawa sioni kabisa ukiota mizizi. Sasa, Je? Iko siku Waafrika tutafikia kufakufa na watu wasio na hatia katika hali ya kutaka kufikisha ujumbe wa amani?Kwanini hatujilipua kipindi hiki? Au tatizo ni dini zetu hazitu ahidi manono mara baada ya kujiua ndio maana bado hatujisikii kufa kufa ?








Peter Tosh alisema kila mtu anataka kwenda mbinguni lakini hakuna atakaye kufa









Ninamsifu Martin Luther King Jr kwa kufia alichokiamini. Natatizo na hawa wanaojiua ilikuua watu wengine wasio na hatia! Bado naendelea kufikiria nakukuna kichwa kuhusu swala hili! Bado namsikiliza Peter Tosh hapa katika huu wimbo wake mwingine akiwa na Mick Jagger akiniambia Walk dont look back.
Bado najiuliza........

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Maisha 5:57 pm  

i would love to read this but im afraid i will have to do it tomorrow.nice bloggie...

Jeff Msangi 8:13 pm  

Simon,
Haya ni mawazo huru,mawazo yakinifu na yenye mlengo wa ndani kabisa.Watu wengi hatupendi kusikia ukweli kwamba kifo ndio njia.

Pia kuna ubishani mwingi sana unaoweza kuzuka ukiwasikiliza watu kama Martin L.King katika mazingira tuliyonayo.Swali zuri sana linaweza kupatikana kutoka kwenye ulichokiandika;mbona mtu kama Osama yeye hataki kuwa wa kwanza kwenda kujivalisha mabomu?

Maisha 11:01 am  

jeff,i agree with you.

simon,what was wrong with your blog?couldnt view end of last week...

Simon Kitururu 11:53 am  

Maisha, I dont know what was the problem with my blog last week.I couldnt access it myself most of the time.

Maisha 1:32 pm  

must have been sabotage...;)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP