Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wamarekani weusi na Afrika!

>> Saturday, September 02, 2006





I aint going back to Africa!












Watu weusi bado tunahitaji watu wamfano. Watu wakujivunia. Bara la Afrika ni bara lenye mengi ya kujivunia.Ni kweli ukifuatilia habari nyingi duniani watu weusi ambao hupewa muda na nafasi ni wale ambao wana sifa mbaya. Bara la Afrika ni mara nyingi huambatanishwa na magonjwa, umasikini na sifa nyingine mbaya.Sasa hivi imefikia kuwa sisi weusi wenyewe kuliponda bara letu wenyewe.Katika mizunguko yangu nimekutana na wamarekani weusi wengi ambao hawakawii kuponda Waafrika na Afrika kwa ujumla. Hawakawii kulaumu kuwa tuliwauza enzi za utumwa.

Mimi naamini kuwa Waafrika wa Afrika tunatakiwa tuwemfano wa kueneza sifa nzuri za Afrika.Kama kuna Muafrika ambaye anatangaza Afrika vizuri kuliko wote basi anaweza kuwa ni Mandela. Lakini naamini kila mmoja anaweza kuchangia katika kuendeleza sifa za bara letu. Hawa wamarekani weusi wapondao Afrika huweza kuathiri sana Waafrika ambao wanawaheshimu na kuwachukulia wao kama mfana. Je ni kweli bara la Afrika linastahili tu kuwa chanzo cha matani na mapungufu tuu?Angalia jinsi ya mitazamo ya baadhi ya Wamarekani weusi hawa katika matani:


Eddy Muphy

Eddy Griffin

Jamie Foxx



Ningependa siku moja listi ya Greatmen kutoka Afrika iwe haihesabiki kutokana na wingi wa watu ambao wamefanya mambo makubwa Afrika.
Mwangalie Burning Spear akikuimbia wimbo Greatmen hapa

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

dara 9:09 am  

i wish i could read this post. i have an idea of what it's about based on the links you provided. thanks for the "great men" video link--i enjoyed that.

Simon Kitururu 10:39 pm  

Nice that U enjoyed the video. I admire U for even visiting blogs written in languages U dont understand!

Jeff Msangi 8:47 pm  

Ukiniuliza mimi nitakuambia kinachowasumbua watu wengi na hata hawa wenzetu wamarekani weusi ni ujinga tu.
Wengi wao hawajaenda shule na hata wakienda wanachoambiwa ndio kama hivi hawa comedians wanachokisema.Sasa wengi hawawezi kutofautisha pumba na mchele na ndio maana wanaamini kabisa haya wanayoyasema.Hawa ni watoto wasio na kwao,lost kids.Wanahitaji msaada wetu wa kuwaelimisha.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP