PUTIN SAFARINI AFRIKA-WADAI NI NEW SCRAMBLE FOR AFRICA
>> Tuesday, September 05, 2006
Putin akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini Nkosazana Dlamini-Zuma
Raisi wa China ameonekana barani Afrika hivi karibuni na sasa imefikia zamu ya Putin wa Rashia.Hizi ziara zimekuwa ziki ongelewa na kuchambuliwa katika Televisheni za ulaya. Lugha itumiwayo inanifanya nishangae na kujiuliza kuwa hivi hawa jamaa wanasahau kirahisi au wanataka kutuzingua tu!Hasa wanavyozungumzia mashwala ya utoaji malighafi Afrika kama vile ni jambo jipya au jambo ambalo lilikuwa limesitishwa .
Hu Jintao akiwa na Mugabe katika mchezo wake wa chesi ya kuendeleza matakwa yake Afrika
Ukiwa unafuatilia maswala ya bara la Afrika ,utagundua tokea enzi za ukoloni mpaka leo hali haijabadilika sana.Hapa nazungumzia maswala ya bara hili kutumiwa kama chanzo cha malighafi. Chakushangaza ukiwa una tazama habari katika Televisheni kama BBC siku hizi wameanza kudai kuwa eti hii ni new scramble for African Raw material.Ninajiuliza tu!Hivi ni lini mataifa ya nje yalisitisha kuchukua malighafi za Africa mpaka sasa hivi isemekane ni mambo yanaanza upya?
Natamani itakapofikia wakati Afrika itaweza kumiliki malighafi zake au kuwa kama Venezuela ambayo imeweza kumiliki malighafi zake chini ya Hugo Chavez. Cha muhimu inabidi kuzifanyia kazi malighafi zetu barani Afrika na kuuza mali zilizo kamilika.
Hugo Chavez yeye hakubaliani na kuuza malighafi za nchi kiholela bila raia kufaidika.
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment