I HAVE BEEN TO TANZANIA. U HAVE BEAUTIFUL ANIMALS THERE!
>> Monday, September 04, 2006
Tanzania is a beautiful country I have seen beautiful animals there. Is that all there is to see?
Halo!Kumbe wewe Mtanzania!Nimetembelea mara nne nchi yenu.Mna wanyama na mbuga nzuri sana nchini kwenu!Hii ni baadhi tu ya maoni ya baadhi ya Wazungu baada ya kugundua natokea Tanzania. Sikatai, Tanzania tuna wanyama pori wazuri. Na mbuga zetu zinavutia. Kinachonisikitisha ni ile baadhi ya watu kuona kuwa zaidi ya mbuga za wanyama basi Tanzania hakuna kitu kingine kifaacho kuitembelea.
Picha kama hizi ndio zilizomo vichwani mwa watu wengi kuhusu Afrika.Sio Wazungu tu bali watu wa mabara mbalimbali mpaka hata Wapakistani hawakawii kuhisi wao wameuchinja kuliko Waafrika.
Halafu hukawii kupitia sehemu nyingine ukakutana na mwingine naye akaanza yake. Mimi nimefika Tanzania mara nyingi sana katika miradi ya kusaidia wananchi.Unajua nchi yenu ina magonjwa sana. Ukimwi na umasikini umekithiri. Nawapenda sana Watanzania ndio maana kila siku najaribu kuja Tanzania kujaribu kusaidia. Mimi sikatai tunahitaji misaada. Magonjwa na umasikini vipo sana. Lakini kuna baadhi ya hawa watu wengi ambao hupenda kutuhubiria jinsi gani wanatusaidia bila kukiri kuwa wanajisaidia pia . Utakuta kwanza ni wao wanafaidika. Wengi wao hata katika jamii zao hawana kitu cha kujivunia. Kwa kuja katika jamii masikini Afrika inawasababisha wajisikie vizuri kwa kujiona kuwa pamoja na yote, bado maisha yao si mabaya.Wengine ni kazi tu .Na hata wengine wameanza kushikwa siku hizi kwa tabia zao mbaya mpaka za unajisi wa watoto wadogo nk.Tabia ambazo wanajua kuwa nirahisi kuziendeleza Afrika bila kushikwa.
Rev. Bonnke akiokoa Waafrika
Nivigumu kuwasahau hawa wengine wanaokuja kutuhubiria dini. Utashangaa mikutano mikubwa ya wahubiri kutoka nje wakiubiri wakiwa na wakalimani wao huku kwetu. Unawezaukashangaa ukiona kuwa hawa watu ni mara chache sana waka hubiri katika nchi zao.Na wanafurahia wingi wa umati unaotoke kuja kuwashuhudi Afrika, kitu ambacho hakitoke kwao. Sasa je ni ukweli wanatupenda sisi zaidi kuliko watu wa nchi zao mpaka waje kutuhutubia sisi na sio watu wa nchi zao?
Baadhi ya watu wa maboti waliobahatika kufika hai Ulaya.
Cha kusikitisha ni kwamba kila siku katika Talevisheni zao siku hizi.Hasa katika mitaa ya ulaya imeongezeka sura moja. Hii ni ya watu kwenye ngalawa na viboti vya ajabu ajabu wakijaribu kukatiza bahari kwenda Spain kutoka Afrika magharibi.Kila siku utasikia wengine wamezama baharini,wengine wameenda kumwagwa jangwani na kadhalika.Hua mara nyingine hujiuliza hivi moyo kama wakufunga safari hizi za kufa nakupona ukiwekwa katika kitu kingine si tungekua mbali Afrika? Cha ajabu siku hizi bongo unakuta Wachina wakiuza mpaka machungwa wakati sisi tukijaribu sana kukimbia. Nikiangalia wasenegali wanavyozamia siachi kujiuliza maswali mengi tu. Hivi Watanzania karibu tutarudi katika maswala ya kuzamia meli kwenda Ulaya?
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nadhani tunahitaji kubadili mitazamo yetu. Tumeonewa kiasi cha kutosha. Tumedhihakiwa vya kutosha. Tumedharauliwa vya kutosha. Tumedharau vyetu vya kutosha. Tumejidharau vya kutosha. Tuamke sasa tubalike. Kila mmoja afanye kazi hiyo kwa dhati. Najua Kitururu u mmoja wa wanaharakati wanaohitajika sasa. Mambo yatabadilika.
Habari hii imenigusa.
Post a Comment