Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

USHUJAA wa KUKOPA!

>> Friday, April 25, 2008

Kukopa ni kazi ngumu, kwa sababu mkopo unakuja na kukutengenezea kasifa wengine wawezako kukaweka ndani ya sentensi kama:JAMAA kwa kukopa hata SERIKALI za AFRIKA hazioni ndani.

Kama si mzoefu, kijasho kitakutoka wakati unafanya maandalizi ya kukopa.

Ukizoea kukopa , unaweza kukopa kisirisiri pia au hata unaweza kukopa sehemu za siri za mwenzio.

Lakini....
....kukopa na staili yako ya kukopa , inategemea tu na ulivyoathirika kisaikolojia fulani.

Swali:

  • Hivi unakumbuka serikali ya Marekani a.k.a USA ndio miongoni mwa serikali zinazodaiwa mikopo sana duniani?
  • Unakumbuka inasemekana sasa hivi MAREKANI haiwezi kumkoromea CHINA kwa vitendo kutokana na CHINA kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kukopesha Marekani?

Staili yako ya kukopa , hutegemea sana kuathirika kwako kisaikolojia bado kuna kuhakikishia kuwa wewe unacho au huna.

Staili ya fundi viatu nje ya duka kumkopa mwenye duka, inaweza ikawa ya upole na unyenyekevu kuliko staili ya huyo mwenye duka kumkopa fundi viatu nje ya duka lake , ingawa wote wamechacha.

Swali:
  • Unajua unabadilika sauti wakati unakopa?
  • Unajua unabadilika mwendo ukisha katashauri kumfuata umtongoze na lolote liwe a.k.a mwendo wa kumsogelea unayetaka kumkopa?

Lakini...
..inawezekana mkopaji aliye shujaa si yule aliyezoea kukopa.

Kukopa ni kitendo unaweza kukipamba kwa kusema umeazima.
Naweza kukubishia ukisema kuwa hujawahi kukopa halafu ukashindwa kunibishia ingawa kijiweni wewe ndiye usiokosa chumvi watu wakihitaji chai.

DUH!
NAACHA!

Baadaye , kesho , kesho kutwa au siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda iwe hivyo!
Si inasemekana hata nikifa ni mapenzi ya MUNGU?

Nakasikiliza kawimbo haka , kaitwako- To the Ceiling kalikopigwa na ISAAC BLACKMAN. Anza nako WIKIENDI ukipenda.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP