Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KABLA HUJAWEKA MAUA KABURINI KWA UMFAHAMUYE.

>> Monday, April 14, 2008

Tunakutana, kuzozana, kupendana au hata kupigana, lakini wakati kila mmoja akianza kivyake, hatuchukulii kuwa ndio inaweza kuwa mara ya mwisho kuonana.

Hakuna ajuaye nini kitatokea sekunde ijayo, ila tunazungumzia kesho tutafanya nini.

Hakuna awezaye yote, lakini, kila siku tunategemewa kufanya yote.

Hakuna azikwaye na mali zake, lakini hatuachi ubahiri na kujilimbikizia.

Tunajua hakuna ajuaye yote, lakini hatuachi kumdharau asiyejua au aitwaye mjinga.

Swali:

  • Ushamwambia unayempenda kuwa unampenda ?
  • Ushamsamehe unayemchukia?
  • Unasubiri useme marehemu alikuwa mtu mzuri?


Lakini....
  • Hivi marehemu lazima asamehewe?
  • Kujilazimisha kumsamehe mtu hata kama moyo hautaki, imo?

DUH!

USITISHIKE!

Niko mawazoni tu!

JUMATATU NJEMA!
Msikilize kidogo Nina Simone akikuambia IF U KNEW

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 11:00 am  

Kama unao wasomaji wanaopitia hapa angalau kila siku, mmoja wao ni mimi (japo hupita kimya kimya).

Huwa naondoka hapa na mawazo. Mawazo endelevu. Ama kweli kibaraza hiki ni murua. Nimeona leo nisipite kimya kimya, nikutie moyo kwa kazi njema unayoifanya.

Simon Kitururu 3:11 pm  

@Bwaya:Asante sana Mkuu!Kijiweni kwako vilevile mimi si mgeni.Napitia kila nikipata nafasi.

Nashukuru bado tuko baadhi ya watu ambao tunapenda kusoma maandishi fulani.Kuna watu huwa wananiambia kuwa:kwa jinsi maisha yalivyo kuwa magumu, si rahisi mtu kupata muda wa kusoma watu wameandika nini.Walijaribu kunnishauri niifanye blog hii iwe ya picha pekee.

Mimi huwa na jibu kuwa - vile vile kuna watu walidai ukitaka kuficha pesa zako ,ficha kwenye kitabu au maandishi, ukiibiwa ,utajua aliye iba si Muafrika.

Nikabisha kwa kusema kuwa , ukificha kwenye maandishi , mimi nitakuibia. Mzee Bwaya , wasomaji wa vitabu na mtandaoni bado tupo!Siku njema!

Anonymous 10:23 am  

kwakweli kaka yangu umesema umefikiri sana hakuna ujumbe mkuu kuliko huu.tupendaneni washikaji!!!

Simon Kitururu 11:53 am  

@anony:Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP