Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NDOTO nzuri, INAWEZA kumchafulia SHUKA mvulana!

>> Thursday, April 17, 2008

Nami hushiriki katika kushawishi watu waote vitu vikubwa na kuvifanyiakazi vitimie.

Lakini....
.....Ndoto zangu zote zingetimia, ningekuwa bilionea , halafu ningeshakufa miaka kadhaa kabla sijabalehe , kwa sababu ndoto nyingine huitwa majinamizi au kwa kiswahili kingine kigumu, huitwa NDOTO MBAYA:

Watu hutukania kulala, ingawa kwa mwaka inawezekana ukawa umetumia miezi sita kulala.
Waliozubaa katika kugombania ubwabwa wa maisha, huambiwa au kutukaniwa kuwa wana ubongo uliolala.

Kulala bomba, kama hupati majinamizi!

Ukilala vizuri , ni rahisi kufanikisha majambo kutokana na utulivu wa akili yako na uwezo wako wakukabili jambo baadaye kama utafanikiwa kuamka. Kulala , si kuna watu wanadai ni nusu ya kifo?

Lakini...
..... nahisi wengine tunalala vizuri au vibaya na kupitiliza kulala mpaka yale maamuzi mazuri tunachelewa kuanza kuyafanyiakazi .

Nafikiri wengine tunalala zaidi , ndio maana ndugu , jamaa na hausigeli wa nyumba ya jirani, wanajiuliza:

  • Mbona hatuoni jamaa afanyalo?
  • Mbona hatuoni hata baiskeli ya swala au ile mashine ya kukoboa pale sehemu sehemu?

Lakini.....

Martin Luther King Jr alisimulia ndoto yake na pia alitabiri kuwa atafariki kabla ya kuona ndoto yake ikitimilika.

Lakini....
...... ndoto yake inatimilika!
Si unaona mpaka Barrack Obama anagombea Urais katika nchi ambayo watu weusi walikuwa wananunuliwa kama KIFUNGU cha EMBENG'ONG'O miaka michache iliyopita?

Nisikufiche sijui sana maswala ya kulala wala ya NDOTO!

Si unajua tena wakati nimelala huwa nakua nimelala, na sifanyii kauchunguzi spidi ya udenda utokavyo mdomoni wakati nimelala ni kilomita ngapi kwa saa kabla haujagonga mto.

Lakini nasikia......
...inasemekana, ukilala kikawaida, unatumia angalau masaa mawili kila siku kuota.

Kumbuka pia , inasemekana kuwa ukilala , kwa wanaume sehemu za uume huweza kusimama na wenyeuke kinukta huweza kuvimba kiaina pia!

DUH!
Nakiri kuacha kuongelea swala nisilolielewa vizuri!

Nacho jua tu ni kwamba!

Ndoto hutimia hata kama ndoto nyingine zitatimia dakika kadhaa tu baada ya mimi na wewe kufa, kufariki au hata kukata roho.

Kama sisi si wachoyo.....
  • Tutimize tu, zile ndoto za kupanda miti ambayo tunauhakika itachukua miaka mia kukua, lakini ikikua itakuwa msaada kwa kizazi kijacho.

  • Tusisite tu ,kufanyia kazi zile ndoto za kupigania haki ya masikini kusikilizwa na serikali yao na matakwa yao kufanyiwa kazi mpaka umasikini uwe ni jina limaanishalo:umasikini ni ile hali ya mtu kujilimbikizia maswala asiyoyahitaji.

  • Tusisite kujaribu kufanyia kazi ile ndoto binafsi ya kuwa na maisha uyatakayo binafsi hata kama ni vigumu kueleweka jichoni mwa ndugu , jamaa, jamii au hata mchumba.

Swali:
  • Unakumbuka uliota nini jana?
  • Hivi masikini na matajiri huota ndoto tofauti?
  • Wanawake na wanaume je?

Ni kweli si ndoto zote nazikumbuka kama nikumbukavyo msosi baadaye kidogo baada ya kuamka..

DUH!

Naacha!
Inawezekana naota tu!
Si unajua tena?

AU?

NAKUTAKIA kila la kheri katika kufanyia kazi ndoto zako!
SIKU NJEMA!
Tulia na WAZIRI wa UTAMADUNI wa BRAZIL , Gilberto GIL
akija na kibao Imagine


Au Mpate tu katika kibao Aquele Abraço


1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

John 9:56 am  

Je, unajua tafsiri ya "embeng'ong'o" kwa Kiingereza? Nakushuru.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP